WAKALA wa huduma za Misitu  nchini  katika 
halmashauri ya wilaya ya Singida,amefanikiwa kukamata magunia ya mkaa 311 yenye
thamani ya zaidi ya shilingi 5.2 milioni, ambayo yamevunwa kinyume na sheria.
Meneja wa wakala huyo wilayani Singida bwana Hashimu Kativo,
amesema magunia hayo wameyakamata  mapemawiki hii katika msako mkali
unaoendelea wa kuwakamata wafanyabiashara na watu wengine wanaouza  mazao
ya misitu na nyuki kinyume na sheria za  nchi.
Amesema  magunia hayo yamekamatwa katika kijiji cha Tupendane
kata ya Mang’onyi baaada ya kukuta magunia hayo yakiwa yamekusanywa  bila
kuwa na kibal cha kuvuna wala leseni ya kununua na kuuza mkaa.
Hata  hivyo amefafanua kuwa wamiliki wa mkaa huo waliweza
kutoroka kwenda kusikojulikana.
Bw Katiyo amesema katika ukamataji huo, pia wameharibu matanuru
sita makubwa ambayo yalikuwa yakitumika kuchoma mkaa kwa ajili ya kuuza.
0 comments:
Post a Comment