MWANASIASA MKONGWE AZUNGUMZIA MAKUNDI YA URAIS NDANI YA CCM‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
kingungePichani ni mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombare(Habari na jamiiblog)
Mwanasiasa  mkongwe nchini,Kingunge Ngombare Mwiru ametamka ya kwamba Chama Cha Mapinduzi(CCM) kamwe hakiwezi kuepuka makundi ya  urais kupitia chama hicho wakati kikielekea katika hatua za ukingoni za kulipata jina la mgombea atakayepeperusha bendera ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa hata miaka ya nyuma yalikuwepo.


Kauli ya mwanasiasa huyo inakuja wakati kamati kuu ya  chama hicho ikikutana mjini Dodoma kuandaa ajenda za mkutano wa halmashauri kuu ya CCM  huku ajenda ya jina la nani atakayekipa ushindi mwaka huu katika nafasi ya urais ikitajwa kutawala katika mkutano huo.

Mwanasiasa huyo alitoa kauli hiyo juzi wakati akihojiwa katika kipindi cha uzalendo kinachorushwa na luninga ya ITV wakati akizungumzia makundi ya urais ndani ya CCM kuelekea uchaguzi  mkuu.

Akihojiwa katika kipindi hicho alisema kuwa CCM hakiwezi kwenda kwenye uchaguzi  mkuu bila  ya kuwa na makundi kwa kuwa makundi hayo yalianza tangu mwaka 1995 hadi sasa.

“Hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi wa kidemokrasia bila ya kuwa na makundi,mwaka 1995 kila mgombea alikuwa na kundi lake  na mwaka 2005 tulikuwa na makundi hata mwaka huu unayo makundi”alisema Mwiru

Alisema kuwa  katika mfumo wa kidemokrasia  ndani ya chama unaruhusu makundi kwa kuwa kila mgombea anakuwa na kundi lake ambalo linamjenga na kutoa ushawishi katika harakati mbalimbali.

Alisema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya makundi ya urais ya mwaka 1995 na ya mwaka 2015 kwani miaka hiyo  makundi yalikuwa ni ya kawaida tu tofauti na sasa  ambapo  baadhi ya wanachama wamekuwa na mitizamo hasi .

Mwanasiasa huyo alisisitiza kuwa mbali na makundi hayo mwisho wa siku ni lazima apatikane mgombea mmoja ambaye atakubalika nje ya CCM.

“Mwisho wake ni lazima apatikane mmoja kupitia vikao  vya CCM na anayekubalika na wengi ndani ya CCM ndiye atakayekubalika nje ya CCM hiyo ndiyo demokrasia”alisisitiza Mwiru

    

HAPPY BIRTHDAY MO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. DSC01228-Edit
MODEWJI BLOG TEAM : Thanking you for being a great boss just isn't enough for your special day! Thank you for inspiring us to be our best! Happy birthday, boss!
And below is a small gift from us!
IMG_9643  
Please join us to wish him a Happy Birthday by follow him on his twitter @moodewji and instagram @moodewji
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa