Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwanasiasa mkongwe nchini,Kingunge Ngombare Mwiru ametamka ya kwamba Chama Cha Mapinduzi(CCM) kamwe hakiwezi kuepuka makundi ya urais
kupitia chama hicho wakati kikielekea katika hatua za ukingoni za
kulipata jina la mgombea atakayepeperusha bendera ya urais katika
uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa hata miaka ya nyuma yalikuwepo.
Kauli ya mwanasiasa huyo inakuja wakati kamati kuu ya chama hicho ikikutana mjini Dodoma kuandaa ajenda za mkutano wa halmashauri kuu ya CCM huku ajenda ya jina la nani atakayekipa ushindi mwaka huu katika nafasi ya urais ikitajwa kutawala katika mkutano huo.
Mwanasiasa
huyo alitoa kauli hiyo juzi wakati akihojiwa katika kipindi cha
uzalendo kinachorushwa na luninga ya ITV wakati akizungumzia makundi ya
urais ndani ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu.
Akihojiwa katika kipindi hicho alisema kuwa CCM hakiwezi kwenda kwenye uchaguzi mkuu bila ya kuwa na makundi kwa kuwa makundi hayo yalianza tangu mwaka 1995 hadi sasa.
“Hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi wa kidemokrasia bila ya kuwa na makundi,mwaka 1995 kila mgombea alikuwa na kundi lake na mwaka 2005 tulikuwa na makundi hata mwaka huu unayo makundi”alisema Mwiru
Alisema kuwa katika mfumo wa kidemokrasia ndani
ya chama unaruhusu makundi kwa kuwa kila mgombea anakuwa na kundi lake
ambalo linamjenga na kutoa ushawishi katika harakati mbalimbali.
Alisema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya makundi ya urais ya mwaka 1995 na ya mwaka 2015 kwani miaka hiyo makundi yalikuwa ni ya kawaida tu tofauti na sasa ambapo baadhi ya wanachama wamekuwa na mitizamo hasi .
Mwanasiasa
huyo alisisitiza kuwa mbali na makundi hayo mwisho wa siku ni lazima
apatikane mgombea mmoja ambaye atakubalika nje ya CCM.
“Mwisho wake ni lazima apatikane mmoja kupitia vikao vya CCM na anayekubalika na wengi ndani ya CCM ndiye atakayekubalika nje ya CCM hiyo ndiyo demokrasia”alisisitiza Mwiru
0 comments:
Post a Comment