Diwani
mteule (CCM) kata ya Minyughe (wa tatu kushoto mwenye suti ya bluu)
Samweli Daniel Sadiki, pamoja na wakazi wa kijiji cha
Minyughe,wakiangalia gari aina ya fuso T.662 CBB la kampuni ya Pepsi
lililosombwa na maji ya mvua katika mto Saiwa.
Gari
aina na fuso T.662 CBB la kampuni ya Pepsi mjini Singida, likiwa
limeangushwa na kusombwa na maji ya mvua katika mto Saiwa wa kijiji cha
Minyughe wilaya ya Ikungi. Gari lililokuwa linasambaza soda katika
vijiji vya kata ya Minyughe lipo mtoni hapo kwa zaidi ya wiki moja,baada
ya kushindikana kutolewa mtoni hapo. Hali hiyo imesababishwa na mto huo
kutokuwa na daraja hali inayochangia pia kuhatarisha maisha ya wananchi
na mali zao.
Baadhi
ya wakazi wa kata ya Minyughe tarafa ya Ihanja,wakivuka mto Saiwa ambao
unadaiwa kutokuwa na daraja, jambo ambalo ni hatari kwa wananchi na
mali zao.
Landrover
110 likiwa limekwama kwenye mto Saiwa kutokana na mchanga wa mto huo
kujaa maji na kusababisha magari kukwama.Hali hiyo inachangiwa na mto
huo mkubwa kutokuwa na daraja.
Wakazi
wa kata ya Minyughe wakisaidiana kuvuka mto Saiwa baada ya maji ya mvua
kupungua.Imedaiwa kuwa mto huo ambao hufurika maji wakati mvua
zinaponyesha,hauna daraja hali inayohatarisha maisha ya watu na mali
zao.Hata hivyo,mhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani
Singida, injinia Haruna Mbagalla,amesema ujenzi wa daraja katika mto
huo,unatajariwa kuanza mapema januari mwakani.(Picha zote na Nathaniel
Limu).
0 comments:
Post a Comment