Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Singida, Martha Mosses Mlata, akishiriki
kutekeleza agizo ya rais Dk. John Pombe Magufuli la Watanzania wote
kufanya usafi katika maeneo yao, kama sehemu ya maadhimisho ya sherehe
za Uhuru kutimiza miaka 54, kwa kufanya usafi kwenye chuo cha wasioona
cha mjini hapa. Pamoja na kufanya usafi chuoni hapo, Mlata alitoa msaada
wa vifaa mbalimbali ikiwemo viti vya plastiki 150.Thamani ya msaada
huo, ni zaidi ya shilingi 6.3 milioni.
Mbunge
wa viti maalum mkoani Singida, Martha Mosses Mlata, akikabidhi msaada
wa vifaa mbalimbali wenye thamani ya zaidi ya shilingi 6.3 milioni kwa
uongozi wa Chuo cha wasioona cha mjini hapa. Msaada huo ni sehemu ya
maadhimisho ya sherehe za Uhuru kutimiza miaka 54.(Picha na Nathaniel
Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MBUNGE
wa viti maalum (CCM) mkoani Singida,Martha Mosses Mlata, (9/12/2015)
ametumia zaidi ya saa tatu kufanya usafi katika Chuo cha Watu Wasioona
kilichopo Manispaa ya Singida.
Mlata
ambaye alifuatana na baadhi ya wana CCM wa Manispaa ya Singida,
alifanya usafi huo ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais Dk.John Pombe
Magufuli kama sehemu ya maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 54 ya
Uhuru.
Mbunge
huyo alisema kuwa anamuuga mkono Rais Magufuli kwa kuhimiza usafi wa
mazingira kitendo ambacho pamoja na mambo mengine,kitapunguza uwezekano
wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko ukiwemo kipindupindu
“Tabia
hii ya kufanya usafi kwenye maeneo yatu na yale mengineyo, inapaswa iwe
endelevu kutokana na faida zake kuwa nyingi.Pia mazingira yakiwa
masafi,yanapelekea kuvutia zaidi”,alisema mbunge Mlata.
Pamoja
na kufanya usafi sehemu mbalimbali za chuo hicho ikiwemo maeneo ya
vyoo,Mlata alitoa msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo vya kufanyia
usafi, viti 150 vya plastiki na mazulia.Vifaa hivyo vina thamani ya
zaidi ya shilingi 6.3 milioni.
0 comments:
Post a Comment