Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP.Thobias Sedoyeka.
Na Nathaniel Limu, Singida-Mo Blog
Jeshi
la polisi mkoani Singida,limefanikiwa kukamata mkulima na mkazi wa
Kibaoni Iddy Issah (33), anayedhaniwa kuwa ni jambazi sugu baada ya
kulipiga risasi moja mguu wake wa kulia, wakati alipojaribu kutoroka.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Singida, ACP Simon Haule,alisema mtuhumiwa
huyo amekamatwa Januari tatu mwaka huu saa 7.20 usiku katika baa ya
Leaders iliyopo kata ya Kindai tarafa ya Unyakumi manispaa ya Singida.
Alisema
siku ya tukio askari polisi walipokuwa kwenye doria katika mitaa ya
kata ya Kindai, walipata taarifa za kiintelijensia kuwa mtuhumiwa yupo
baa ya Leaders maeneo ya Kibaoni.
“Baada
ya polisi hao kupata taarifa hizo,walifika haraka kwenye baa hiyo na
kujaribu kumkamata mtuhumiwa.Lakini alipambana nao huku akitaka
kumnyang’anya silaha mmoja wa askari polisi hao,hata hivyo,hakuweza
kufanikiwa”,alisema Haule.
Kaimu
kamanda huyo,alisema baada mtuhumiwa kushindwa kupora silaha,
alifanikiwa kukimbia akitaka kutoroka ndipo askari mmoja alifyetua
risasi mbili hewani, ili kumwongofya aweze kusimama.Hakuweza
kusimama,kitendo kilichomlazimisha askari kumjeruhi mguu wa kulia.
Kuhusu
tuhuma zinazomkabili mtuhumiwa, Haule alisema amefunguliwa kesi
SI/IR/4412/2015 ya kuvunja nyumba usiku na kumwimbia raia wa kigeni
kutoka China, shilingi 17,442,000.
“Mwaka
jana pia alifunguliwa kesi no.SI/1R/4722/2015 ya kuvunja nyumba usiku
na kuiba shilingi 200,000 mali ya raia wa kigeni kutoka Korea. Ana kesi
nyingine no.SI/1R/4723/2015 ya kuvunja nyumba usiku na kuiba fedha na
simu vyote vikiwa na thamani shilingi 3,101,000.Makosa hayo yote
yanaangukia chini ya kifungu cha sheria namba 294 (2) na 296 (a) vya
kanuni ya adhabu”, alifafanua.
Alisema
kwa sasa mtuhumiwa Iddy amelazwa wodi namba tatu katika hospitali ya
mkoa mjini hapa chini ya ulinzi mkali, na hali yake inaendelea vizuri.
Haule alisema baada ya upelelezi zaidi kukamilika,mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
0 comments:
Post a Comment