Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAIMU Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani hapa, Ephraim
Kaphilimbi amesema agizo jipya la serikali la kutonunua dawa nje ya
Bohari Kuu ya Dawa (MSD) limeongeza ugumu wa upatikanaji wa dawa katika
wilaya yake.
Aidha, alisema muda MSD inaochukua kujibu maombi yao ni tatizo kubwa
katika kuhakikisha kwamba hospitali zote za serikali wilayani humo zina
dawa za kutosha.
Alikuwa akijibu hoja za wananchi na wadau wa afya waliokuwa wakisema
kwamba ukosefu wa dawa, na kuzuiwa kupata matibabu katika hospitali
mbili za misheni wilayani ni kikwazo kwao katika kujiunga na Mfuko wa
Afya ya Jamii.
Miongoni mwa waliolalamikia tatizo hilo ni madiwani Mohamed Juma,
Ramadhani Mohamed na kiongozi wa dini maarufu kwa jina Shehe Jumanne.
“Ukosefu wa dawa ni tatizo kubwa na suala hili ni kubwa kwa kuwa
limeanzia mbali ni suala la kitaifa,” alisema Kaimu Mganga Mkuu huyo na
kuongeza kwamba sehemu kubwa ya mkanganyiko wa sasa wa dawa ni kutokana
na maagizo hayo kwamba dawa zote zinunuliwe MSD.
Alisema, serikali inasema imeingiza fedha MSD moja kwa moja, lakini
dawa hazifiki wilayani na majibu ya maswali kwanini hazijaja huwa
yanakatisha tamaa.
Kwa maelezo yake, kutokana na mazingira hayo kwa sasa, Halmashauri haziruhusiwi kununua dawa nje ya maagizo ya serikali.
Alisema, pamoja na dawa kuwa tatizo wilaya hiyo inakabiliwa na
ukosefu wa hospitali ya wilaya na zile zinazodhaminiwa zimesimamisha
huduma za CHF kutokana na kuidai Halmashauri ya Mkalama fedha nyingi.
Hata hivyo, ilifafanuliwa katika kikao hicho kwamba ukosefu wa dawa
ni tatizo kwa kuwa halmashauri husika zinaweza kukopa dawa NHIF wakati
wanafanya kukamilisha mipango ya kusubiri dawa za MSD.
CHANZO ; HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment