Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Singida, Festo Kang’ombe ametaka kuwepo na
nguvu ya ushawishi katika kupata wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii
(CHF) na si kuwalazimisha wananchi na kusababisha wakimbilie porini kwa
sababu za michango.
Alisema hivyo wakati akifungua mkutano wa siku ya wadau katika
wilayani hapa, ikiwa ni sehemu ya upitishaji wa mchakato wa kutungwa kwa
sheria ndogo na kutengenezwa hati kwa lengo la kuwezeshwa kuendeshwa
kwa mpango wa CHF wilayani humo.
Mchakato huo unaokwenda hatua kwa hatua, unatarajiwa kukamilishwa wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Alisema, pamoja na uzuri wa mpango huo ambao ni wa hiari, wananchi
wanatakiwa kushawishiwa na si kulazimishwa kwa kutumia mabavu, ili
wajiunga na CHF.
Kang’ombe alisema, wilaya ya Mkalama si ngeni katika utekelezaji wa
mpango wa CHF na kwamba muitikio mkubwa utakaowezesha kuimarisha huduma
za afya wilayani hapo utatokana na nguvu za hoja na wala si hoja za
nguvu.
Alisema, wilaya hiyo mpya ilikuwa awali ikitekeleza mpango huo chini
ya wilaya ya Iramba na ilionesha mafanikio makubwa tangu kuanzishwa
kwake mwaka 2004 ndio maana wilaya nyingi zilifika kujifunza.
Kang’ombe alisema, alipokuwa Ofisa Mipango katika wilaya ya Kahama
walifika kujifunza uendeshaji wa CHF, safari ambayo pia iliwafikisha
Igunga na Mbinga.
Alisema, taifa lenye wagonjwa haliwezi kusonga mbele na uwekaji wa
nguvu za pamoja utawezesha matatizo ya sekta ya afya yaliyopo kwa sasa
kuondoka.
CHANZO ; HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment