Mwana
CCM, Martha Mosses Mlata (kushoto) akirejesha fomu za kugombea nafasi
ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida kwa Katibu msaidizi CCM mkoa wa
Singida, Adamu Makulilo leo.Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Singida,iliachwa wazi na Mgana Izumbe Msindai aliyetimkia CHADEMA baada
ya kushindwa kwenye kura za maoni wakati wa kinyang’anyiro za kura za
maoni (nafasi ya ubunge) ndani ya CCM.
Mwanyekiti
wa jumuiya ya wazazi (CCM) mkoa wa Singida, Yusuph Mwandami Gwayoka
(kushoto) akikabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti wa CCM mkoa
wa Singida na Katibu msaidizi CCM mkoa wa Singida, Adamu Makulilo.Picha
na Nathaniel Limu.
Na Nathaniel Limu, Singida
MBUNGE
wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida, Martha Mosses Mlata ni miongoni
mwa wana CCM sita ambao wamejitokeza kuomba kuziba nafasi iliyoachwa
wazi na Mgana Izumbe Msindai ya mwenyekiti wa CCM mkoa aliyetimkia
CHADEMA muda mfupi baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa kura za maoni
(CCM) kugombea ubunge.
Wana
CCM wengine waliochukua fomu hadi leo jioni toka zoezi la uchukuaji
fomu lianze Januari sita mwaka huu asubuhi,ni Juma Hassan Kilimba,
Mohammed Hamisi Missanga, Narumba Barnaba Hanje, Shafii Juma Mtaturu na
Yusuh Mwandami Gwayoka.
Katibu
msaidizi wa CCM mkoa wa Singida,Adamu Makulilo,alisema hadi sasa
aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iramba Juma Hassan Kilimba,Martha Mlata na
aliyemaliza muda wake wa ubunge wa jimbo la Singida magharibi mwaka
jana,Mohammed Hamisi Missanga,wameisha rejesha fomu zao.
Adamu alisema zoezi hilo la utoaji wa fomu bado linaendelea na linatarajiwa kukoma januari 10 mwaka huu saa kumi jioni.
“Nitumie
fursa hii kuwaomba wana CCM wajitokeze kwa wingi na hasa wale
watakaojipima na kubaini wanao uwezo wa kuvaa viatu vilivyoachwa na
Mgana Msindai,ili kuleta upinzani wa kweli utakaosaidia CCM kupata
mwenyekiti atakayemudu kasi iliyopo hivi sasa nchini.Ada ya fomu ni kama
bure kabisa, kwa sababu tunatoza fomu ‘buku’ tu (shilingi
10,000)”,alisema katibu msaidizi huyo.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hii kwenye viwanja vya CCM mkoa,Mlata alisema
kuwa safari hii ni zamu ya mwanamke kuongoza chama tawala mkoani hapa,na
kwamba mwanamke huyo si mwingine isipokuwa ni yeye (Mlata).
Alisema
amejikagua na kujitathimini na kubaini kwamba anao uzoefu wa kutosha
kuwatumikia wana CCM na wananchi kwa ujumla katika nafasi hiyo ya
mwenyekiti CCM mkoa.
“Kupitia
nafasi mbalimbali nilizozipata ikiwemo ya ubunge wa viti
maalum,nafahamu vyema Chama Cha Mainduzi kinavyoongozwa,nazijua
changamoto ya chama chetu kuanzia ngazi ya chini ya tawi hadi mkoa.Kwa
ukweli huo,mimi ni chaguo sahihi kupewa nafasi iliyoachwa wazi na kaka
yangu Msindai”,alisema.
Mlata
aliyesema endapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Singida,atatumia nguvu zake zote amoja na wanachama wengine,kurejesha
umoja na mshikamano miongoni mwa wana CCM,ili mkoa uendelee kuwa wa CCM
chama cheye sera zinazotekelezeka.
“Nitashirikiana
na wana CCM wenzangu kukiimarisha chama na kuhakikisha CCM inawajengea
mazingira mazuri wananchama wake ili waweze kuboresha hali zao za
kiuchumi.Tatizo linalosababisha mwanachama ye yote wa chama cho chote
cha saisa kuhama hama,ni umaskini tu.Lakini mtu kama ana uwezo mzuri
kiuchumi,huyo sio rahisi kumurubuni au kumdanganya”,alisema Mlata.
Kwa
upande wake Yusuph Mwandami Gwayoka, alisema kuitia nafasi yake ya
mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa,anayo uzoefu wa kutosha wa kumudu
nafasi ya mwenyekiti CCM mkoa.
“Mimi
nimejipanga vema kushindana na wana CCM wenzangu katika kuwania nafasi
hii ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida. Niwaase tu wagombea wenzangu
kwamba tunakwenda kushindana na wala hatuendi kugombana.Kwa hali
hiyo,kabla na baada ya matokeo kutangazwa,tuendelee kudumisha umoja na
mshikamano na ikiwezekana,ushirikiano tulio nao,tuuboreshe
zaidi”,alifafanua Mwandami.
MO BLOG
0 comments:
Post a Comment