Tigo yatoa visima 12 vya maji kwa vijiji 12 Singida

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akikata utepe katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akifungua moja ya bomba katika kisima   katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
 Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia) akifungua bomba katika moja ya kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo pembeni yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mtinko  katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida  Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. 

Singida, Aprili 27th 2016:  Kampuni ya simu ya Tigo leo imekabidhi visima 12 vya maji  vyenye thamani ya 174m/- kwa vijiji 12 mkoani  Singida  ikiwa ni kuchangia juhudi za serikali  za kupunguza  uhaba wa maji safi na salama uliopo nchini.
Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano  iliyofanyika kwenye kijiji cha Mtinko wilayani Singida  mkoani Singida, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata  alisema ufadhili huo  umo kwenye mikakati ya kampuni ya kusaidia  jamii katika kunyanyua hali zao za maisha.
 Vijiji vitakavyonufaika kutokana na ufadhili huo pamoja na wilaya zake kwenye mabano ni Lulumba (Iramba), Kisana (Iramba), Kisonzo (Iramba), Songambele (Iramba), Kinyeto (Singida Vijijini) na  Damankia (Ikungi). Vingine ni  Muungano (Ikungi), Ighuka (Ikungi), Kamenyanga (Manyoni), Sasajila (Manyoni), Mtinko (Singida Vijijini) and Kinampanda (Kinampanda).
 “Msaada huu ni sehemu ya uwekezaji wa Tigo kwenye miradi ya kijamii  ambayo inaleta tija kubwa kwa jamii. Tuna imani kwamba kupitia visima hivi, Tigo inasaidia  kutatua uhaba mkubwa wa maji  katika eneo hili la mkoa wa Singida  ambalo kwa kiwango kikubwa  limekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua katika kipindi cha miaka mine  iliyopita,” alisema Lugata.
 Aidha aliongeza kuwa uhaba wa maji  miongoni mwa  wilaya nyingi za Singida  umesababisha wakiazi wake  kupoteza muda mwinmgi kutafuta  bidhaa hiyo muhimu, jambo ambalo  Tigo inaamini  kuwa hivi sasa litafikia ukomo kutokana na upatikanaji wa visima hivyo.
 Makabidhiano ya visima hivyo yalihudhuriwa na kushuhudiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge  ambaye aliishukuru Tigo kwa ufadhili huo uliopatikana kwa wakati mwafaka akisema kwamba visima hivyo vitapunguza kwa kiwango kikubwa  uhaba sugu wa maji  uliolikumba eneo hilo  na kuchangia kukua ustawi wa jamii  kijamii na kiuchumi.
 Hata hivyo, alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo  kuchangia kwenye juhudi kama hizo. Waziri Lwenge alisema, “Tunatoa shukrani za dhati kwa Tigo kwa kutuunga mkono kwenye juhudi zetu za kutatua  uhaba wa maji uliopo Singida na hata kwenye mikoa mingine nchini. Tuna imani visima hivi 12  vitasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hili linaloikabili jamii kwa sasa”.


MWIGULU,SENDEKA WASHIRIKI MAZISHI YA CHRISTINA LISSU MKOANI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akitoa heshima zake za mwisho mapema leo kabla ya mazishi, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lisu,Wilayani Ikungi mkoani Singida.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida,Bi Martha Mlata akitoaa heshima zake za mwisho mapema leo kabla ya mazishi, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lissu,Wilayani Ikungi mkoani Singida. 
Msemaji wa chama cha CCM,Ole Sendeka, Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba wakimpa pole Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA),Mh Tundu Lissu,ambao waliwasili wilayani Ikungi mkoani Singida kushiriki Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lissu.
 Msemaji wa chama cha CCM,Ole Sendeka akimpa pole Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA),Mh Tundu Lissu kwa kufiwa na dada yake
 Msemaji wa chama cha CCM,Ole Sendeka akitoa neno la pole kwa Wafiwa,ndugu,jamaa na marafiki kabla ya kufanya maziko, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lissu,Wilayani Ikungi mkoani Singida.

Michuzi Media



MBUNGE CHADEMA AFARIKI DUNIA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Christina-Mugwai-LissuNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chadema kutoka Mkoa wa Singida, Christina Lissu Mughwai amefariki dunia kwa ugonjwa wa kansa.
Christina ambaye ni dada wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), alifariki dunia jana   katika Hospitali ya Aga Khan,   Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Lissu katika kundi la mtandao wa kijamii la WhatsApp wa wabunge wa Chadema, Christina  alikuwa akisumbuliwa na   kansa tangu mwaka jana.
“Waheshimiwa nawasalimu kutoka Kibondo. Nina habari zisizokuwa njema. Dada yangu na aliyekuwa Mbunge wetu wa Viti Maalum, Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Aga Khan.
“Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa cancer (kansa) tangu mwaka jana. Niko nje ya Dar es Salaam na ndiyo kwanza taarifa hizi zimenifikia, sina taarifa zaidi juu ya mipango ya mazishi…tutawaarifu baada ya kushauriana na familia,”alisema Lissu.
Zitto atuma salamu
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe katika  salamu zake za rambirambi alizotuma katika ukurasa wake wa Facebook, alisema alipata kufanya kazi na Christina na kwamba aliipenda kazi yake, hivyo atamkumbuka daima.
“Christina Mughwai Lissu hatunaye. Nilibahatika kufanya kazi na dada Tina nikiwa Waziri Kivuli wa Fedha na yeye akiwa Naibu Waziri Kivuli. Tina ni msomi mzuri aliyependa kazi yake na ni mtu mwenye utulivu wa fikra.
“Natoa pole kwa familia nzima ya Lissu kwa msiba mkubwa uliowapata. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi,” alisema Zitto.
Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda (Chadema) alipiga simu chumba cha habari MTANZANIA akieleza kusikitishwa na taarifa hizo za kifo cha Christina.
“Ni rafiki yangu mpambanaji, alijua kupangilia hoja zake bungeni, alikuwa akinipa moyo kabla sijawa mbunge.
“Aliniambia kupigania haki za wanyonge si kazi ya siku moja inahitaji ujasiri na kujitoa kwa niaba yao. Ametangulia kamanda Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi Amina,” alisema.
Naibu Katibu Mkuu Bara (Chadema), Salum Mwalimu, alipopigiwa simu aliomba apewe muda  awasiliane na viongozi wenzake wa chama hicho kwa sababu hakuwa na taarifa zozote kuhusu kifo hicho.
“Ndiyo kwanza taarifa hizo nazisikia kwako, nipe muda kidogo niwasiliane na wasaidizi wangu   na viongozi wengine, nitakupa taarifa,” alisema Mwalimu.
CHANZO:MTANZANIA. 

WATUMISHI 3 WASIMAMISHWA KAZI IRAMBA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAIMU Mkuu wa Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, Christopher Ngubiagai, ameagiza kusimamishwa kazi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watumishi watatu wa halmashauri hiyo kwa tuhuma mbalimbali, ikiwamo matumizi mabaya ya madaraka.
Ngubiagai ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, mkoani humo alitaja tuhuma nyingine kuwa ni kushindwa kutoa ushauri makini na kusababisha upotevu wa fedha na nguvu za wananchi katika ujenzi wa bweni la wasichana la shule ya sekondari Kinyangiri wilayani Mkalama.
Aliwataja watumishi hao kuwa ni David Malegi, Mhandisi Msaidizi Ujenzi, Hashim Ndwata (Fundi Sanifu) na aliyekuwa Mratibu wa Mradi huo, Jeremiah Lubeleje ambaye kwa sasa amehamishiwa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Alieleza kuwa mradi huo wa ujenzi wa bweni la wasichana ulianza Septemba 6, mwaka 2011 wakati wilaya ya Mkalama ikiwa haijagawanywa kutoka wilaya mama ya Iramba.
Ngubiagai alisema wafadhili wa mradi huo, Ubalozi wa Japan walitoa hundi ya Sh milioni 133.7 kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo ambapo halmashauri ilipewa jukumu la kusimamia, kutoa ushauri wa kitaalamu, kununua na kuweka vitanda na magodoro ujenzi utakapokamilika.
“Ujenzi wa hosteli hiyo ulikuwa ukamilike Aprili 18, mwaka 2012 lakini hadi hivi leo ( zaidi ya miaka minne) haujakamilika na jengo limekaa bila kutumika, huku wasichana waliopaswa kulitumia wakitembea kilometa 14 kwenda na kurudi hali inayowaathiri kitaaluma,” alisema Ngubiagai.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa licha ya ujenzi huo kutokamilika kama ambavyo mkataba ulielekeza, uongozi wa halmashauri ya Iramba pia umeshindwa kukabidhi bweni hilo kwa halmashauri ya wilaya ya Mkalama.
Kutokana na hali hiyo, alisema njia pekee ni kuwasimamisha kazi wahusika wa mradi huo ili uchunguzi wa kina ufanyike na ikithibitika wamehusika na tuhuma hizo hatua za ukiukwaji maadili ya utumishi wa umma zichukue mkondo wake.
Kusimamishwa kwa watumishi hao watatu kunafanya idadi ya waliosimamishwa katika halmashauri hiyo hadi sasa kufikia tisa. Februari mwaka huu watumishi sita wa Idara ya Afya nao walisimamishwa kwa tuhuma ya upotevu wa zaidi ya Sh milioni 145.2 za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
CHANZO: HABARI LEO
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa