MASWALI YA TUNDU LISSU YAMPA KIGUGUMIZI KATIBU WA CCM.




Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Mh.Tundu Lissu akiwa na wapambe wake nje ya mahakama ya mkoa, mahali kesi yake ya kupinga matokeo yaliyompa ubunge inasikilizwa.
Badhi ya wasikilizaji wa kesi ya Mh. Tundu Lissu wakiwa wamejazana katika madirisha ya mahakama ya mkoa wa Singida kusikiliza kesi hiyo.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na. Nathaniel Limu
‘MVUA’ ya maswali katika kesi ya mlalamikiwa wa kwanza  Tundu Lissu  ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge wa jimbo la Singida Mashariki, yamesababisha aliyekuwa Katibu wa CCM Singida vijijini, Cosmas Kasangani, kupandwa na hasira na  kushindwa kujibu maswali ipasavyo.
Ilimlazimu Wakili  Godfrey Wasonga aliyewasilisha maombi ya kupinga ushindi wa Tundu, aiombe mahakama kuu inayosikiliza kesi hiyo, imruhusu ampe mteja wake ushauri nasaha ili aweze kuacha woga na hasira,kitendo ambacho kingeharibu lengo lao la kutaka matokeo ya uchaguzi  ushindi huo utenguliwe.
Baada ya Mahakama Kuu kukubali ombi hilo, Wasonga alimfuata Kasangani kizimbani na kumpatia ushauri nasaha  ambao ulizaa matunda kwa shahidi huyo, kutulia na kuanza kujibu maswali ya Tundu Lissu.
Aidha, Jaji Mosses Mzuna anayesikiliza kesi hiyo, alimtoa hofu Kasangani ambaye kwa sasa ni Katibu wa CCM Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, kwamba endapo atachoka kusimama, anaweza akawa anajibu maswali akiwa ameketi na pia anaruhusiwa kunywa maji, wakati wo wote.
Kasangani ambaye ni shahidi wa  10 katika kesi hiyo inayovuta hisia za wakazi wengi wa Mkoa wa Singida, katika kikao cha juzi alianza kutoa ushahidi wake akiongozwa na wakili wa CCM, Wasonga.
Kasangani ambaye alikuwa akitoa ushahidi wake kwa kujiamini, aliiomba mahakama kuwa mlalamikiwa wa kwanza Tundu Lissu alikuwa na mawakala 10 kila kituo cha kupigia kura, jambo ambalo ni kinyume na taratibu za uchaguzi.
Akifafanua zaidi,alisema katika vituo 124 vya jimbo la Singida mashariki, Tundu alikuwa na mawakala watano ndani ya kila kituo na wengine watano nje ya kituo.
Kasangani alisema katika barua za wakala hao wa Tundu ambazo alifanikiwa kuzinasa, zilikuwa za kutoka vyama vya TLP, NCCR – Mageuzi, APPT maendeleo, CUF na CHADEMA.
Alisema barua hizo zilikuwa zinafanana mno karibu kwa kila kitu na kuonekana dhahiri zimeandaliwa na kuandikwa na mlalamikiwa wa kwanza, Tundu Lissu
Katibu hyo wa CCM  aliiambia mahakama hiyo iliyofurika wasiklizaji, kuwa vyama vya siasa vya TLP, NCCR – Mageuzi, APPT maendeleo havikuwa na mgombea ubunge katika jimbo la Singida mashariki, kwa hivyo havikustahili kuweka mawakala.
Barua hizo zilizoandikwa kwa anuani ya vyama vya TLP, APPT maendeleo, NCCR Mageuzi, CUF na CHADEMA, zilisababisha mabishano makali ya kisheria kati ya mlalamikiwa kwa kwanza Tundu Lissu akisaidiwa na mawakili watatu, ambao wanasimamia mwanasheria mkuu wa serikali na msimamizi wa uchaguzi na wakili wa waleta maombi.
Tundu na wenzake walikuwa wanapinga barua hizo kupokelewa na mahakama kuu kama vielelezo katika kesi hiyo, kwa madai hazikubaliki kisheria.
Hata hivyo, wakili wa waleta maombi, Wasonga aliweza kushinda katika mabishano hayo na mahakama kuu ikazipokea barua hizo na kuwa vielelezo halali katika kesi hiyo.
Katika hatua nyingine wakati kesai hiyo inaendelea, jaji Mzuna alikemea tabia iliyojitokeza kwa mawikili hao  kuanza kutupiana vijembe kwa kutumia lugha ambayo haikubaliki kisheria.
Baada ya hapo, Tundu Lissu alianza kumuuliza shahidi Kasangani maswali kama ifuatavyo:-
Tundu, Shahidi katika barua hizo ulizo nazo, hebu angalia ya kwanza kama imeandikwa kwa kalamu au imeandikwa kwa mashine.
Kasangani; zimeandikwa kwa mashine na sio kwa mkono.
Tundu, Je barua ya kwanza ni ya chama gani na ina jina la Tundu Lissu mahali popote au saini yake?
Kasangani; barua hii ni ya APPT maendeleo, haina jina lako wala saini yako.  Isipokuwa ina saini ya Selemani Alli Ntandu, Katibu wa chama hicho.
Tundu; shahidi hebu angalia vizuri barua ya pili inayofuata, mwambie jaji ni ya chama gani na imeandikwa kwa kalamu au mashine.
 Kasangani, mheshimiwa jaji, barua hii ni ya TLP, imeandikwa kwa mashine na imesaini na katibu wa TLP wilaya Athumani Nkii.
Tundu; Je shahidi, barua hiyo ya TLP ina jina au saini yangu mahali popote?
Kasangani, Haina.
 Barua zote zilizokuwa zinalalamikiwa na Kasangani kuwa ziliandikwa na Tundu Lissu kwa lengo la kujipatia ushindi, hazikuwa na jina la Tundu na zote ziliandikwa kwa mshine/kompyuta.
 Aidha, katika ushahidi wake Kasangani,alisema askari polisi D. 9979 Paulo aliyekuwa anasimamaia kituo kimoja katika kijiji cha Ikungi, aliacha kazi yake na kuanza kumpigia kampeni Tundu siku ya kupiga kura (31/10/2010).
 Tundu alimpatia Kasangani shahada kutokakwa mkuu wa polisi nchini Saidi Mwema na ya Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Celina Kaluba ambazo zote zinampongeza polisi huyo, kwa utumishi wake uliotukuka.
 Baada ya Kasangani kuzisoma kwa sauti, Tundu alimuuza, je kati yako na  mkuu wa polisi nchini Saidi Mwema, nani anamfahamu au anafahamu zaidi utendaji kazi wa askari D.9979 Pulo?.
Kasangani, alinyamaza kwa muda na baada ya kukazaniwa na Tundu, alijibu kwa kifupi,‘sijui’.
Wakati Tundu akiendelea kuporomosha mvua ya maswali ya Kasangani, Kasangani alimwomba jaji Mzuna kwamba amechoka na hawezi tena kuendelea kujibu maswali.
Jaji Mzuna, alimwambia kuwa avumilie na kuendelea na kazi ya kujibu maswali ili kazi hiyo iishe siku hiyo.Alimtaka akae kwenye fomu kama amechoka kusimama.
Hata hivyo, Kasangani amabye kwa wakati huo alionyesha wazi kuishiwa pumzi, alisisitza kuwa hana nguvu tena nguvu ya kuendelea kujibu maswali.
Kesi hiyo iliahirishwa na (jana) (30/3/2012) saa tatu asubuhi, ilitarajiwa kuendelea kwa Kasangan kujibu maswali yaTundu Lissu.

MADUKA MANNE MKOANI SINGIDA YATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO.





Picha mbalimbali zinazoonyesha maduka manne yaliyoko jirani na soko kuu mjini Singida yaliyougua moto usiku wa kuamkia leo (21/3/2012). Kila kilichokuwepo ndani kimeteketea.Taarifa juu ya chanzo cha moto huo zitatolewa leo mchana na Jeshi la Polisi.
(Picha na Nathaniel Limu). 

WALIMU SHULE ZA MSINGI IRAMBA WATISHIA KUFANYA MAANDAMANO IWAPO HATAREJESHEWA MAKATO YAO.




Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzani (CWT) mkoa wa Singida Allan Jumbe akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa salamu zake za mwaka mpya wa 2012.
Jengo la CWT mkoa wa Singida. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Walimu wote wa shule za msingi wilayani Iramba mkoa wa Singida wameonya kwamba iwapo hawatarejeshewa zaidi ya shilingi 27 milioni walizokatwa kimakosa  kama malipo ya pango la nyumba miaka kumi iliyopita, watafanya maandamano makubwa na ya aina yake kushinikiza marejesho hayo.
Wamedai kwamba kama hawatarejeshewa fedha hizo hadi mwishoni mwa mwezi huu, wataacha kufanya kazi na kwenda makao ya wilaya ambayo ni New Kiomboi, na kufanya maandamano hayo.
Akitoa salaam za CWT za mwaka mpya wa 2012 kwa walimu wote wa mkoa wa Singida kupitia vyombo vya habari Mwenyekiti wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Singida Allan Jumbe amefafanua kuwa zaidi ya miaka kumi iliyopita, walimu wengi wa wilaya ya Iramba, walikatwa kwa makosa fedha za pango la nyumba (house rent).
 Jumbe amesema wakati wanakatwa fedha hizo, walimu hao walikuwa wamepanga nyumba za watu binafsi na walikuwa wakilipa pango la nyumba hizo kwa fedha zao.
Hawakuwa wamepanga nyumba za serikali kwa hiyo hawakustahili kukatwa fedha za pango na mwajiri wao.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Manyoni, kwa madai kwamba kwa kipindi chote cha mwaka jana, hapakuwa na tatizo.
Habari kwa hisani ya Mo Blog

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA SINGIDA YAITAKA JAMII KUFICHUA WEZI WA MAJI.


Meneja Mtendaji wa mamlaka ya maji safi na maji taka (SUWASA) Singida mjini Mhandisi Isaac Nyakonji akitoa taarifa yake wakati wa ufunguzi wa wiki ya maji.
Diwani wa kata ya Mwankoko jimbo la Singida mjini Hamisi Kulungu akizungumza kwenye ufunguzi wa wiki ya maji jimbo la Singida mjini.
Mwenyekiti wa bodi ya SUWASA Martin Churi akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi wa wiki ya maji Singida mjini.
Mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya maji diwani wa kata ya Mwankoko Hamisi Kulungu akipanda mti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo ya wiki ya maji.
Kikundi cha uhamasishaji cha kijiji cha Mwankoko kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa wiki ya maji Singida mjini.
Kisima cha majaribio kilichochimbwa mwaka 2006 katika kijiji cha Mwankoko. Kisima hicho kimeendelea kumwaga maji kama inavyoonekana usiku na mchana toka mwaka 2006 hadi sasa bila kutumika.
Kisima kilichochimbwa hivi karibuni katika kijiji cha Mwankoko na inadaiwa kina uwezo wa kuzalisha lita zaidi ya laki moja kwa saa. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Wakazi wa Singida mjini wamehimizwa kujenga utamaduni wa kufichua watu wanaojiunganishia maji kiholela bila idhini ya mamlaka ya maji safi na maji taka (SUWASA), ili waweze kuchukiliwa hatua kali za kisheria.
 Wito huo umetolewa na diwani wa kata ya Mwankoko (CCM) jimbo la Singida mjini Hamisi Kulungu, wakati akizungumza kwenye halfa ya uzinduzi wa wiki ya maji  katika manispaa ya Singida.
 Amesema tabia ya kujiunganishia huduma ya maji inalenga kuihujumu SUWASA  ili isiweze kutoa huduma bora kwa wakazi wa Singida mjini jambo ambalo sio zuri.
 Akifafanua Kulungu amesema tabia hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa SUWASA ishindwe kufikia lengo lake la kukusanya mapato.
 Aidha, amewataka pia wawafichue watu wanaochepusha dira za maji kwa lengo la kujipatia maji ambayo hawayalipii.
 Kwa upande wake Meneja wa SUWASA Mhandisi Isaac Nyakonji, amesema madhumuni makubwa ya maadhimisho ya wiki ya maji mwaka huu ni kutoa fursa kwa wananchi kuielewa kikamilifu programu ya maendeleo ya sekta ya maji ili waweze kushiriki katika utekelezaji wake.
Katika hatua nyingine, Mhandisi huyo amesema jumla ya miti 1,800 itapandwa kipindi chote cha wiki ya maji kwenye maeneo ya burudani na Unyankindi.
 Amesema miti itakayopandwa ni miti ya asili ambayo inastahimili ukame  tofauti na miti ya kisasa.
Picha kwa hisani ya Mo Blog

Welcome to Singida Region Tanzania


Singida is one of the regions of Tanzania. The region is bordered to the North by Shinyanga Region, to the Northeast by Manyara Region, to the East by Dodoma Region, to the Southeast by Iringa Region, to the Southwest by Mbeya Region and to the West by Tabora Region. It is one of the poorest regions in Tanzania. Singida is itself a region, a district, and a town.
It is accessible from Arusha through Babati and Kateshi in Manyara RegionDar es salaamIringa andMbeya through Dodoma and TaboraShinyanga and Mwanza through Nzega in Tabora Region. Although not all the roads are passable all the year round, they expected to be so in the near future when the connections to ArushaDodoma and Mbeya will be tarmac. Otherwise the connection to Shinyanga,Mwanza and Tabora via Nzega is passable all the year round.

Geographical Location

Singida region is located below the equator between latitudes 3052’ and 7034’. Longitudinally the region is situated between 33027’ and 350 26’ east of Greenwich. To the north, it shares borders with Shinyanga RegionArushaManyara and on the east borders Dodoma.To the south it shares borders with Iringa and Mbeya while on the west there is Tabora Region.
Singida region has a total surface area of 49,438 sq. kms out of which 95.5 sq.kms or 0.19 percent are covered by water bodies of Lake Eyasi, Kitangiri, Singidani, Kindai and Balengida. The remaining 49,342.5 sq.km is land area. Singida region is deemed to be neither small no big. It is the 13thin size and occupies about 5.6 percent of the Tanzania mainland’s total area of 881,289sq.km. Climate

Districts

Singida Region is administratively divided into 4 districts: IrambaManyoniSingida Rural and Singida Urban.

Town

In Singida town (i.e. Singida municipal district) and Singida Rural District, the main tribe is the Nyaturu. The town is also home to immigrants from different parts of Tanzania. Iramba district belongs to Nyiramba tribe and Manyoni district belongs to Gogo and few of Nyaturu tribes.
The Photo below featured one of the Chief Saidi Gwao's wife Bibi Nyamwagele of Samumba. Gwao was chief of Singida South around 1940s, after he died his brother Chief Mange Gwao took over the crown until after Tanzania independence, when chief leadership was abolished
Source Wikipedia 
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa