Meneja Mtendaji wa mamlaka ya maji safi na maji taka (SUWASA) Singida mjini Mhandisi Isaac Nyakonji akitoa taarifa yake wakati wa ufunguzi wa wiki ya maji.
Diwani wa kata ya Mwankoko jimbo la Singida mjini Hamisi Kulungu akizungumza kwenye ufunguzi wa wiki ya maji jimbo la Singida mjini.
Mwenyekiti wa bodi ya SUWASA Martin Churi akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi wa wiki ya maji Singida mjini.
Mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya maji diwani wa kata ya Mwankoko Hamisi Kulungu akipanda mti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo ya wiki ya maji.
Kikundi cha uhamasishaji cha kijiji cha Mwankoko kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa wiki ya maji Singida mjini.
Kisima cha majaribio kilichochimbwa mwaka 2006 katika kijiji cha Mwankoko. Kisima hicho kimeendelea kumwaga maji kama inavyoonekana usiku na mchana toka mwaka 2006 hadi sasa bila kutumika.
Kisima kilichochimbwa hivi karibuni katika kijiji cha Mwankoko na inadaiwa kina uwezo wa kuzalisha lita zaidi ya laki moja kwa saa. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Wakazi wa Singida mjini wamehimizwa kujenga utamaduni wa kufichua watu wanaojiunganishia maji kiholela bila idhini ya mamlaka ya maji safi na maji taka (SUWASA), ili waweze kuchukiliwa hatua kali za kisheria.
Wito huo umetolewa na diwani wa kata ya Mwankoko (CCM) jimbo la Singida mjini Hamisi Kulungu, wakati akizungumza kwenye halfa ya uzinduzi wa wiki ya maji katika manispaa ya Singida.
Amesema tabia ya kujiunganishia huduma ya maji inalenga kuihujumu SUWASA ili isiweze kutoa huduma bora kwa wakazi wa Singida mjini jambo ambalo sio zuri.
Akifafanua Kulungu amesema tabia hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa SUWASA ishindwe kufikia lengo lake la kukusanya mapato.
Aidha, amewataka pia wawafichue watu wanaochepusha dira za maji kwa lengo la kujipatia maji ambayo hawayalipii.
Kwa upande wake Meneja wa SUWASA Mhandisi Isaac Nyakonji, amesema madhumuni makubwa ya maadhimisho ya wiki ya maji mwaka huu ni kutoa fursa kwa wananchi kuielewa kikamilifu programu ya maendeleo ya sekta ya maji ili waweze kushiriki katika utekelezaji wake.
Katika hatua nyingine, Mhandisi huyo amesema jumla ya miti 1,800 itapandwa kipindi chote cha wiki ya maji kwenye maeneo ya burudani na Unyankindi.
Amesema miti itakayopandwa ni miti ya asili ambayo inastahimili ukame tofauti na miti ya kisasa.
Picha kwa hisani ya Mo Blog
Picha kwa hisani ya Mo Blog
0 comments:
Post a Comment