Baadhi ya wanachama wa Singpress wakiwa mkutano mkuu na kufikia uamuzi wa kusamehe madeni kwa wenzao walioazima vifaa vya klabu
 Katibu mtendaji wa Singpress, Bw. Abby Nkungu akieleza kwa wadau wa habari safari ndefu ya kalbu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002
Singida
Desemba 12,2012.
MGOGORO  mkubwa unaiandama Klabu ya wanahabari mkoa Singida (Singpress),  kufuatia mwenyekiti wake Seif Takaza kuruhusu baadhi ya wanachama  kufutiwa madeni yenye thamani ya Sh. 1,961,600.
Madeni dhidi ya wanachama hao ambao huko nyuma pia waliwahi kula  fedha za waandishi, yametokana na kuazima vitendea kazi, vilivyotolewa masaada na baraza la habari nchini (MCT).
Vifaa  hivyo vilivyotolewa kwa klabu zote nchini miaka minne iliyopita ni  kamera aina ya sonny kwa ajili ya video na picha mnato (zote digitali),  kompyuta za mezani na kinasa sauti kimoja.
Bei  ya kukodi kwa siku ilikuwa Sh. 2,500 (kinasa sauti) Sh. 3,000 (picha  mnato) na Sh.5,000 (video), wakati kompyuta haikuwa kwenye mpango wa  kuazimishwa, lakini ilikuwa kwa mmoja wa viongozi, zaidi ya miaka  miwili.
Kamera  mbili ikiwemo ya video na picha mnato pia kompyuta, vilikuwa vipya  wakati vinaazimwa, lakini viliporejeshwa vilikuwa havifai, wakati kinasa  sauti mpaka sasa hakijulikani kilipo.
Katika  mkutano huo, mwandishi wa jeshi la polisi mkoa Singida, Shabani Msangi,  Paschal Tantau na wadaiwa sugu, walijipanga vema kudhoofisha jitihada  ya uongozi uliotaka madeni hayo yalipwe.
Kufuatia  mvutano mkali uliosababisha wajumbe wengi kutoka nje kwa hasira,  mwenyekiti Takaza alivuruga zaidi alipoamuru upigaji kura na wajumbe  wachache waliokuwa ndani,  wakashinda.
Mkutano  huo pia ulipitisha deni la Sh. 200,000 za pango alizokuwa anazodaiwa  mwanachama Jumbe Ismaelly na Sh. 56,000 dhidi ya fundi mlango wa chuma  Evarest Thomas, wazirejeshe mara moja.
Wanachama  waliofutiwa madeni hayo na kiasi chao ni Doris Meghji (Sh. 90,000),  Elisante Mkumbo (Sh. 25,000), Jumbe Ismaelly (Sh.1,231,600), Hillary  Shoo (Sh. 615,000) na fundi mlango Evarist Thomas (56,000).
Waliofutiwa madeni hayo baadhi ni wadaiwa sugu, baada ya miaka ya nyuma kula fedha  za rambirambi na mwingine kula fedha za umoja wa waandishi na wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini (AJM).
Aidha  tabia ya wanachama wakorofi kupenda vurugu hadi kuchangia madeni hayo  kufutwa, inaweza kuiingiza klabu kwenye mgogoro mkubwa, baada ya kutulia  tangu uongozi mpya uingie madarakani 2011.
"Unaona  sasa tabia ya kuingiza wanachama bila kufuatiliwa wasifu wao huko  walikotokea imeanza kutugharimu...klabu ilishatulia, ona vurugu hizi,  mtu anasema hadi anagonga meza utadhani amegombana, mimi najiuzulu  ,"alisema mmoja wa  viongozi wanaounda kamati ya utendaji.


1 comments:
Andikeni ukweli kwa manufaa ya umma, sio kusema uongo katika mitandao Aibu sana kwa chombo hiki na mnauhakika kiasi gani na hayo mlioyaweka hapo.
Post a Comment