Home » » Mgana Msindai apania kufufua michezo mkoani Singida na kuwataka wadau kutoa ushirikiano.

Mgana Msindai apania kufufua michezo mkoani Singida na kuwataka wadau kutoa ushirikiano.



Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Izumbe Msindai akizungumzia kufufua michezo wakati akihutubia wakazi (hawapo kwenye picha) wa kata ya Aghondi jimbo la Manyoni magharibi. Mkutano huo wa hadhara ulifanyika katika kijiji cha Kamenyange.Wa kwanza kulia ni mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi, John Paulo Lwanji na anayefuata ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Manyoni.(Picha na Nathaniel Limu).
Mwenyekiti wa CCM Mkowa wa Singida Mgana Izumbe Msindai, amedai kwamba CCM, serikali ya Mkoa na wadau mbalimbali,  kwa pamoja watashirikiana ili kufufua michezo kwa lengo la kurejesha heshima ya mkoa katika sekta ya michezo.
Msindai maarufu kwa jina la CRDB benki inayomjali mteja, ameyasema hayo wakati akizungumza na wana-CCM na wananchi kwa ujumla wa kata ya Aghodi, Kata ya Sajaranda jimbo la Manyoni Magharibi.
Amesema mkoa wa Singida katika miaka ya nyuma, ulikuwa ukifanya vizuri sana kwenye mashindano ya michezo mbalimbali, ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu, netiboli na riadha.
Msindai amesema lakini katika miaka ya hivi karibuni, michezo mkoani Singida imeporomoka kwa kasi ya  kutisha.
Amesema tatizo la kuporomoka kwa michezo ni lazima litafutiwe ufumbuzi wa kudumu, kwa vile michezo ina faida nyingi.
Kwa hali hiyo, amesema mlango wa ofisi yake utakuwa wazi wakati wote kwa mtu/watu wenye maoni, ushauri na mapendekezo ya namna nzuri, itakayosaidia.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa