Mkuu
wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi, ameiagiza idara ya kilimo na
mifugo kuangalia uwezekano wa kuanzisha siku maalumu ya sherehe za
wakulima ngazi za kata ili pamoja na mambo mengine, wakulima wengi zaidi
waweze kutumia fursa hiyo kujifunza kilimo bora.
Mlozi
ametoa changamoto hiyo wakati akizungumza kwenye kilele cha sherehe za
wakulima wa halmashauri ya wilaya ya Singida zilizofanyika katika kijiji
cha Masweya tarafa ya Ilongero.
Amesema
utamaduni wa kuendelea kufanya sherehe za wakulima mjini Dodoma
kunawanyima fursa wakulima wengi na hasa wadogo kuonyesha mazao yao na
pia kujifunza mbinu bora za kilimo.
Mlozi
amefafanua kuwa, kama tutasogeza maonyesho ya wakulima hadi ngazi ya
kata, faida zake ni nyingi mno kuliko kufanyia mahali ambapo wakulima
wetu wengi hawawezi kufika. Faida mojawapo ni kwamba wakulima
watajifunza mbinu bora za kilimo na kwa njia hiyo, malengo ya kilimo
kwanza, yatafikiwa.
Katika
hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya Mlozi amewataka wakulima kutumia vizuri
mazao watakayovuna msimu huu na kuhakikisaha wanaweka chakula cha
kutosha familia kwa kipindi chote cha mwaka.
CHANZO : MO BLOG
0 comments:
Post a Comment