WILAYA ya Iramba mkoani Singida imelazimika
kuagiza zaidi ya dozi laki nne za chanjo ya ugonjwa wa kideri
moja kwa moja toka kiwandani, kwa ajili ya kusambaza kwa wafugaji wa
kuku.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kubainika kuwa
dawa na chanjo nyingi zinazonunuliwa na wananchi kwenye maduka
binafsi ya kilimo na mifugo zinakuwa zimechakachuliwa na kusababisha kuku kufa.
Akizungumza kwenye mafunzo ya
ufugaji bora wa kuku, Mkuu wa Wilaya hiyo Yahaya Nawanda amesema
baada ya kubaini tatizo katika chanjo hizo, wameona vyema kuagiza moja
kwa moja toka kiwandani zinakotengenezwa na kuzimbaza kwa wananchi
wanaofuga kuku Vijijini.
Bwana Nawanda amesema tayari mpango
huo umeanza kutekelezwa na dozi hizo za chanjo zaidi ya laki nne
zinatarajiwa kuwa zimewasili katika Wilaya ya Iramba kabla ya
mwisho wa mwezi huu.
Ufugaji wa kuku wa asili ni moja shughuli kuu za
kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Singida ambapo inakadriwa kuwa hadi kufikia
mwishoni mwa mwaka jana zaidi ya kuu milioni mbili walikuwa wanafugwa.
0 comments:
Post a Comment