Home » » Timu ya Minga bingwa mpya kombe la MO 2013/2014

Timu ya Minga bingwa mpya kombe la MO 2013/2014

 Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP. Geofrey Kamwela (wa kwanza kulia) wakifurahia jambo na OCD wa wilaya ya Singida, Mohammed Mwinyipembe (katikati) na msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida mjini, Duda Mughenyi wakati mechi ya fainali ya ligi kombe la MO
 Msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida mjini, Duda Mughenyi akitoa taarifa ya ligi ya kombe la mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Dewji iliyomalizika mwishoni mwa Juma.
 Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, ACP.Geofrey Kamwela akimkabdhi kombe la ubingwa wa ligi ya Mo, kapteni wa timu ya Minga ya manispaa ya Singida, Shaban Juma.
 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Minga wakifurahia baada ya kunyakua ubingwa wa ligi ya kombe la MO.
Baadhi ya wapenzi wa soka waliokuwa wakifuatilia mechi ya fainali ya kombe la mbunge wa Singida mjini,Mohammed Dewji iliyofanyika mwishoni mwa Juma kwenye uwanja wa Namfua.
Timu ya soka ya kata ya Minga Manispaa ya Singida imetawazwa mabingwa wa kombe la Mbunge wa Jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO) kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 baada ya kuichapa Mungumaji goli 2-1 kwenye mechi kali na ya kusisimua iliyofanyika kwenye uwanja wa Namfua jijini Singida.
Hata hivyo mechi hiyo ilivunjika dakika tano kabla ya kuisha baada ya timu ya Mungumaji kugomea kuendelea na mechi hiyo kwa madai kuwa mwamuzi wa mchezo huo alikuwa hawatendei haki katika maamuzi yake.
Mechi hiyo ilivunjika baada ya Mwamuzi Sarah Bogi kuwatoa nje kwa kadi nyekundu Yahaya Juma wa Minga na Hamisi Hamisi wa Mungumaji kwa kitendo cha cha kupigana uwanjani.
Mchezo huo ambao ulihudhuriwa na wapenzi wengi zaidi wa soka ikilinganishwa na mechi zote zilizochezwa kwenye ligi hiyo iliyoanza septemba mosi mwaka huu magoli mawili ya Minga yalifungwa na Shaban Juma,wakati lile la kufutia jasho la Mungumaji lilifungwa na Hamisi Hamisi.
Mgeni rasmi katika mechi hiyo ya fainali alikuwa Kamanda Polisi Mkoa wa Singida, ACPGeofrey Kamwela amesema wachezaji wa timu hizo zilizofanikiwa kucheza fainali wameonyesha vipaji vya hali ya juu.
“Kwa kweli vijana wameonyesha wazi kama wataendelezwa wanaweza kufika mbali katika mchezo wa soka, wamenivutia mno na mimi nitaangalia uwezekano wa kuendeleza mchezo wa soka ili vijana waweze kupata fursa ya kuonyesha vipaji vyao kwa manufaa yao na ya mkoa pia”,amesema Kamwela.
Kwa upande wake Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Duda Mughenyi amesema MO ameanza kufadhili ligi hiyo toka mwaka 2003 hadi sasa.
Amesema lengo kuu la ligi hiyo limebaki kuwa lile lile la kuibua vipaji ili pamoja na mambo mengine vijana waweze kujiajiri na kuajiriwa.
“Nitumie fursa hii kuwaomba na wadu wengine wa michezo kufufua na kuendeleza michezo mbalimbali katika Manispaa ya Singida ili vijana na watu wengine waweze kuonyesha vipaji vyao kwa manufaa ya wahusika,wilaya na Mkoa wa Singida”,amesema Duda.
 
NA BLOG YA SINGIDA

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa