Mkuu
wa wilaya ya Ikungi,Manju Msambya, akizungumza kwenye mahafali ya 48 ya
shule ya msingi ya Mang’onyi.Wa kwanza kushoto ni meneja mahusiano wa
kampuni ya madini ya Shanta na anayefuatia ni mwenyekiti wa kamati ya
shule ya msingi ya Mang’onyi, Andrea Andalu.
Mkuu
wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Manju Msambya (wa pili kulia)
akikata utepe kuzindua choo chenye matundu 40 cha shule ya msingi
Mang’onyi kilichojengwa na kampuni ya Shanta.Wa kwanza kulia ni afisa
elimu wilaya ya Ikungi Gerald Kivuyo.Wa kwanza kushoto ni meneja
mahusinao wa kampuni ya madini ya Shanta,Credo Simbaye na anayefuata ni
mkuu wa shule ya msingi ya Mang’onyi, Adamu Mwekwa.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Manju Msambya akigawa vyeti kwa mmoja wa wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo.
Jengo la ofisi ya kijiji cha Mang’onyi kilichojengwa kwa msaada ya kampuni ya madini ya Shanta.
Jengo
la kituo cha kisasa cha polisi kata ya Mang’onyi kinachoendelea
kujengwa kwa msaada ana kampuni ya madini ya Shanta.Anayeonyesha jengo
hilo la kituo cha polisi,ni meneja Ardhi na Makazi wa kampuni ya madini,
Elisante Kamuya.
Vyumba vya Choo vilivyojengwa na Kampuni ya madini ya Shanta.
Jengo
la choo cha shule ya msingi cha zamani cha shule ya msingi Mang’onyi
wilaya ya Ikungi ambacho hakifai kwa matumizi tena.(Picha na Nathaniel
Limu).
Na Nathaniel Limu, Mang’onyi
Kampuni
ya madini ya Shanta Singida imetumia zaidi ya shilingi 23.6 milioni
kugharamia ujenzi wa choo cha matundu 40 katika shule ya msingi
Mang’onyi jimbo la Singida mashariki.
Hayo
yamesemwa juzi na Meneja Mahusiano wa kampuni ya madini Shanta,Credo
Simbaye wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya choo hicho
iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mang’onyi.
Amesema
kwamba uamuzi wa kampuni ya Shanta kutoa msaada huo wa ujenzi wa choo
ni kuinusuru shule hiyo kufungwa kutokana na kukosa choo.
“Baada
ya mamlaka husika kutaka kuifunga shule hii kongwe kwa muda usiojulika
kutokana na kukosa kabisa choo kamati ya shule ilileta ombi kwetu
tusaidie kuijengea choo cha matundu 40 ili isifungwe na wanafunzi zaidi
ya elfu moja wakakosa masomo ombi hilo tulilipokea kwa mikono
miwili”,alisema Simbeya
Meneja
Mahusiano huyo amesema pamoja na Shanta bado haijaanza shughuli zake za
uchimbaji madini iliona upo umuhimu mkubwa kujenga choo kwa shule hiyo
ili wanafunzi wasikatishe masomo kwa tatizo la choo.
“Unapowekeza
katika biashara ya madini au maliasili yo yote ile kimsingi unakuwa
umekubali pia kuwa mdau wa maendeleo ya wananchi katika eneo
husikajukumu mojawapo ni kuhakikisha kwamba msukumo wa maendeleo
yanayotarajiwa unapata nguvu za pamoja”amesema Simbaye.
Aidha
amesema pia hivi sasa wapo kwenye maandalizi ya kuchimba kisima kirefu
cha maji kitakachosaidia kupunguza uhaba mkubwa wa maji unaochangia
wakazi wa kata ya Mang’onyi kuchangia maji na mifugo.
“Kama
nilivyosema awali kwamba Shanta haijaanza kuchimba madini lakini hilo
halijazuia kampuni kutoa misaada ili kutatua kero mbalimbali
zinazowakabili wananchi wa kata ya Mang’onyi.
Simbaye
amesema kwa sasa wanajenga chumba cha darasa katika shule ya msingi
Mlumba kituo cha kisasa cha polisi kata ya Mang’onyi,vijana 210 wamepata
ajira za muda na kampuni imeendelea kutoa magari kwa ajili ya
kusafirisha wagonjwa kuwapeleka kituo cha afya Ikungi na zahanati ya
kijiji cha Mwau.
“Wito
wangu kwa wananchi wa wilaya ya Ikungi na hususan wa kata ya Mang’onyi
,nawaomba waamini kwamba,mradi wa dhahabu wa Shanta Singida,utakapoanza
utafungua ukurasa mpya wa maendeleo kwa wilaya ya Ikungi na mkoa wa
Singida,hivyo hawana budi kuunga mkono”,alisema meneja Simbaye.
chanzo: Mo Blog
0 comments:
Post a Comment