Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Ni Katibu wa TSD Mkoa wa Singida,Bwana Samweli Ole
Saitabau(aliyesimama) akitoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa haki za
walimu wa wilaya ya Manyoni ambao bado haapandishwa madaraja yao.
Ni Baadhi ya wanachama wa CWT Wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Katibu Muu wa CWT,Bwana Ezekiah Oluoch .
Ni Baadhi ya wanachama wa CWT Wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Katibu Muu wa CWT,Bwana Ezekiah Oluoch .
WALIMU
447 wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya wilaya ya
Manyoni,Mkoani Singida hawajapandishwa madaraja yao mbalimbali kutoka
mwaka 2014/2015 mpaka sasa hali ambayo imepunguza ari ya utendaji wao wa
kazi za kila siku.
Katibu
wa Chama Cha Walimu (CWT) Wilaya ya Manyoni, Nelea Nyang’uye aliyasema
hayo kwenye taarifa ya kamati ya utendaji ya chama hicho aliyotoa kwa
Naibu katibu mkuu CWT,Ezekiah Oluoch aliyekuwa na ziara ya siku moja
wilayani Manyoni iliyolenga kusikiliza kero pamoja na kuzitafutia
ufumbuzi.
Aidha
Nelea alifafanua kwamba kati ya walimu hao,walimu 390 ni walimu wa
shule za msingi na kwamba walimu 276 licha ya kuwa na sifa za
kupandishwa madaraja lakini mpaka wamefikia hatua ya kugota na bila
kupandishwa na walimu 114 wanastahili kupandishwa kwa utaratibu wa
kawaida.
Kwa
mujibu wa katibu huyo wa CWT,kwa upande wa idara ya elimu sekondari kuna
walimu 9 waliogota na walimu 50 wanastahili kupandishwa kwa utaratibu
wa kawaida lakini mamlaka zinazohusika zimeshindwa kushughulikia
wilayani hapa.
Kuhusu
malipo ya fedha za likizo,Nyang’uye aliweka bayana kuwa kwa kipindi cha
mwezi disemba,mwaka jana Halmashauri ya wilaya ya Manyoni ilitarajia
kupokea shilingi milioni 30 lakini fedha walizopokea ni shilingi milioni
21 na hivyo kuwa na upungufu wa shilingi milioni saba.
Hata
hivyo msemaji huyo wa chama alisisitiza kwamba fedha hizo za nauli ya
likizo hupelekwa kidogo sana na kibaya zaidi fedha hizo hupelekwa wakati
likizo ikiwa imeshaanza au inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea
walimu wwenye haki ya kulipwa kuanza kukopa.
“Nauli
za likizo kuletwa kidogo mno na zinaletwa wakati likizo ikiwa imeanza
au inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea walimu wenye haki ya
kulipwa kuanza kukopa,kwa mfano nauli ya mwezi disemba,mwaka jana
iliyoletwa kwa idara ya elimu ya msingi ni shilingi 23,000,000/= na
idara ya elimu sekondari ni shilingi milioni saba”alisisitiza katibu
huyo wa CWT.
Nyang’uye
hata hivyo alionyesha masikitiko yake kutokana na Tume ya Utumishi wa
Walimu(TSD) wilaya ya Manyoni kushindwa kushughulikia mashauri ya
kinidhamu kwa wakati na hivyo kuchukua muda mrefu sana na kutoa mfano wa
shauri moja la walimu wawili waliosimamishwa kazi tangu mwaka 2013
mpaka sasa hawajuia hatma yao.
Picha na Michuzi Media
0 comments:
Post a Comment