|
|
|
Kampuni ya simu ya Tigo imefungua duka jipya Singida ambalo
limepunguza adha kwa wateja wa kampuni hii ambao walikuwa wanatafuta huduma kwa
wateja umbali mrefu toka kwa makazi yao
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo Mkurungezi wa Tigo
Kanda ya Kaskazini Bw.George Lugata alisema uzinduzi wa duka hili ni moja ya
mipango ya kampuni ya Tigo kusogeza huduma karibu na wateja wake.
"Kampuni ya tigo
imeangalia fursa zilizopo katika eneo la Singida ambapo kwa pamoja tumeiona ni
jinsi gani tunaweza kusaidiana na wakulima na wafanya biashara kuweza kufanya
huduma mabalimbali za kibenki kwa kutumia simu za mkononi"Alisema Lugata.
Lugata alisema kuwa duka hilo linategemea kuhudumia wateja wapatao
mia tatu kwa siku wakipata huduma mbalimbali ikiwemo huduma za kuunganishwa
kwenye intaneti, usajili wa laini za simu na kurudisha laini zilizopotea pia
kununua simu za kisasa.
Kwa upande wa katibu wa mkuu wa wilaya ya Singida mjini Mhe.Saidi Amani alipongeza hatua za Tigo za ufunguzi wa duka hili kwa
kuwa utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wa wilaya ya Singida.
Tigo Tanzania ina jumla
ya maduka (46) nchini, na duka hili linamaanisha kwamba tunaongeza ubora wa
huduma zetu katika maeneo zaidi. Wateja wetu watakao tembelea duka hili wataweza kufurahia na huduma
zetu mbali mbali matumizi ya smartphones, modemu za intaneti, Tigo Pesa, Muziki
wa Tigo na Facebook ya bure inayotolewa na kampuni.
0 comments:
Post a Comment