Home » » Afungwa jela miaka 120 kwa kumiliki nyara za serikali

Afungwa jela miaka 120 kwa kumiliki nyara za serikali

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


WASHITAKIWA sita waliokuwa wanakabiliwa na makosa mawili ya kumiliki vipande 53 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 149. 3 na uwindaji haramu kinyume na sheria wamehukumiwa kwenda jela miaka 120 na kulipa faini ya Sh bilioni 1.4 .
Waliokumbwa na adhabu hiyo ni Eliud Selema Mayunga (38) mkazi wa kijiji cha Kiombo, Ramadhani Said maarufu “Biladuka” (47) mkazi wa Itigi, na Leonard Oscar maarufu “Sunzu” (31) mkazi wa Karangari, wilayani Manyoni.
Wengine ni Philemon Michael maarufu “Kanyonga” (31) mkazi wa Kitaraka Itigi, Iddi Waziri au “Issah Ustadh” (30) mkazi wa kijiji cha Kiombo na Jimmy Charles Lyimo (39) mfanyabiashara wa Tabora.
Mwanasheria wa Serikali, Petrida Mutta alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida, Joyce Minde kuwa mnamo Machi 31 mwaka 2014 muda usiojulikana, washitakiwa walikamatwa wakiwa na vipande hivyo nyumbani kwa Iddi Waziri.
Mutta aliiomba Mahakama itoe adhabu kali kutokana na vitendo vya uwindaji na biashara za nyara za serikali kuendelea kushamiri.
“Vitendo hivi haviwezi kufumbiwa macho kwa sababu vikifumbiwa macho, fahari ya nchi hii ya kuwa na wanyama pori itatoweka.”
Washtakiwa ambao wakili wao Josephat Raphael Wawa hakuwepo mahakamani, kila mmoja kwa nafasi yake, aliiomba Mahakama impe adhabu nafuu kutokana na kuwa kosa lao la kwanza.
Akitoa hukumu, Hakimu Minde alisema kuwa upande wa Jamhuri umethibitisha bila kuacha shaka yoyote kwamba washtakiwa wanayo hatia kwa makosa yote mawili. Alisema, kwa kosa la kwanza kila mmoja atatumikia jela miaka 20 na kwa kosa la pili kila mmoja atalipa faini ya Sh milioni 248. 8 tu.
Chanzo Habari leo

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa