DC MTATURU AZINDUA MRADI WA UTAMBUZI NA USAJILI WAKAZI UNAOENDESHWA NA NIDA



Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mradi wa utambuzi na usajili wakazi waishio Wilayani hum
Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji Kata, Waratibu elimu Kata, na Maafisa kilimo ngazi ya Tarafa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa utambuzi na usajili wakazi waishio Wilayani humo
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Bw Dandala Mzunguor akiwatambulisho waratibu kutoka Nida kwa ajili ya kutoa elimu ya namna ya kuendesha zoezi la utambuzi na usajili kwa wakazi

DC MTATURU: SERIKALI ITAVISAIDIA VIKUNDI VITAKAVYO KUWA TAYARI KUJIHUSISHA NA KILIMO CHA UMWAGILIAJI


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza umakini kwa wananchi waliojitokeza kwenye Kikao cha Mafunzo ya namna bora ya kushiriki katika kilimo chambogamboga na matunda kupitia umwagiliaji
Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayub Sengo akiwasihi wananchi kutumia njia za kisasa katika kilimo cha umwagiliaji na kufuata taratibu wanazoelekezwa na wataalamu wa kilimo
Baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali sawia na wajumbe washiriki kwenye mafunzo hayo wakifatilia kwa makini Muelimishaji
Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya RIWADE Mhandisi Ayubu Massau, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Moses Msai Mratibu wa RIWADE mkoa wa Singida na Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayub Sengo
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe wakifatiliakwa makini mafunzo ya namna bora ya kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia Gree House
Kutoka Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Hassan Tati, Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya RIWADE Mhandisi Ayubu Massau, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Moses Msai Mratibu wa RIWADE mkoa wa Singida na Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ayub Sengo
Dc Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kufunga mafunzo hayo

Na Mathias Canal, Singida

Uongozi wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida umeahidi kuvisaidia vikundi mbalimbali ambavyo vitakubali kujihusisha na kilimo cha mbogamboga na matunda (Perishable Crops) sambamba na kilimo hicho kwa kutumia Kitalu Nyumba (Green House).

Kauli ya serikali imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati akifunga mafunzo kwa wajasiriamali, wakulima na wafugaji yaliyoendeshwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya Right Way For Development (RIWADE) kwenye ukumbi wa Mikutano katika Shule ya Sekondari Ikungi na kuhudhuriwa na watu 115 ambao wanatokea katika Kata 24 kati ya Kata 28 zilizopo Wilayani humo.

Katika Mafunzo hayo jumla ya Vikundi 39 vimehudhuria ambavyo vimetakiwa kujishughulisha zaidi kukimbia kilimo cha mazoea ambacho wakulima hulima msimu mmoja hadi mwingine na hatimaye kujihusisha na kilimo cha umwagiliaji ambacho kinatumia muda mchache kukamilika na kuanza kwa mavuno.

DC Mtaturu amevitaka vikundi hivyo kwa pamoja kutumia vyema fursa ya Makao makuu ya serikali kuhamia Mjini Dodoma kwani itakuwa taswira chanya katika kukuza soko la mazao yao pasina kupata ugumu wa uuzaji.

Amesema kuwa Mkoa wa Singida mara nyingi umekuwa ukitajwa kama mkoa masikini nchini Tanzania kati ya mikoa 10 ambayo ipo mkiani katika maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya wananchi wenyewe kutofanya ubunifu katika kilimo chao jambo ambalo linasababisha uzalishaji mdogo na kupelekea kipato kuendelea kuwa duni ilihali maandalizi ya mashamba ni makubwa.

Mtaturu amesema kuwa wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa serikali katika kukamilisha adhma yake katika uwekezaji na Tanzania ya viwanda kwani endapo watakubali kulima kilimo cha kisasa na kuwa na uzalishaji mkubwa itakuwa rahisi kwa serikali kuanzisha viwanda vya kusindika mazao.

Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya RIWADE ambayo imesajili kwa lengo la kiwasaidia vijana wasio na ajira waweze kufanya kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Mazingira Mhandisi Ayubu Massau alisema kuwa wananchi wanapaswa kufikia kilimo cha kuachana na kuuza mazao yao kwa madalali badala yake kuuza moja kwa moja kwa mtumiaji jambo ambalo litatoa fursa chanya ya mafanikio makubwa katika pato la mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo amepigia chepuo zaidi kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House) na kusema kuwa ndicho kilimo pekee chenye uwezo wa kuwatoa wananchi kwenye kadhia ya umasikini kwani kilimo hichp kupitia umwagiliaji wa kisasa unatumia maji machache na matokeo yake ni makubwa kama wakulima watafuata taratibu zote za utunzaji wa shamba.

Massau alisema kuwa umefika wakati wa wananchi kuachana na vyama vya kufa na kuzikana badala yake kujihusisha zaidi na vyama vya kujikwamua kiuchumi kupitia vikundi mbalimbali.

Naye Moses Msai ambaye ni Mratibu wa RIWADE mkoa wa Singida alisema kuwa wakulima wanapaswa kutambua kuwa sekta pekee yenye uwezo wa kuajiri watu wengi na kuwatoa kwenye lindi la umasikini ni Sekta ya Kilimo hivyo ni vyema kufanya kilimo cha kisasa kwani ndicho kitakacho wanufaisha wananchi.

Ametoa fursa kwa wananchi kujiunga na RIWADE kwani watapata fursa ya kuunganishwa na wataalamu ili kuelekezwa namna bora ya kulima kilimo cha umwagiliaji.

Hata hivyo Mjasiriamali na mkulima aliyeshika nafasi ya Kwanza kanda ya kati katika sekta ya kilimo Hassan Tati aliwasihi wakulima hao waliopatiwa mafunzo kuwa mafanikio kwenye kilimo ni makubwa endapo wakulima watafuata taratibu za kilimo na kuwasikiliza wataalamu.

Tati amesema kuwa hakuna ajira nzuri duniani kama kuwekeza kwenye kilimo lakini amewasihi wananchi kuing'ang'ania Asasi ya RIWADE kwani ni taasisi muhimu kwa kila mmoja kwa kujitolea kutoa mafunzo ya kilimo na ufugaji.

Rais Dkt. Magufuli ni kiongozi mkali- Bashe

.


Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini kupitia tiketi ya CCM Hussein Bashe amesema Rais Dkt. John Magufuli siyo 'dikteta' kama baadhi ya watu wanavyosema bali ni kiongozi mkali anayeshuhulikia mambo ambayo ambayo yalikuwa yamezoeleka nchini.

Akizungumza katika kipengele cha Kikaangoni kinachoonyeshwa na ukurasa wa East Africa Facebook, ameweka bayana kwamba kwa watu ambao walizoea kupiga dili kwa sasa hivi wamekwama mdiyo maana wanasema ni dikteta.

“Rais Dkt. John Magufuli siyo 'dikteta' kama maana halisi ya dikteta ilivyo , ila ni kiongozi ambaye ni mkali ambaye anapingana na mambo ya kufanya mambo kwa mazoeza 'Business as usual' waliokuwa wamezoea kupiga dili bandarini kwa siku mtu alikuwa anapata laki moja au mbili sasa hiyo imekoma” Amesema Bashe.

Aidha kuhusu baadhi ya wananchui kulalamika kwamba pesa hazionekani mtaani, Mbunge Bashe amesema kipendi alipoingia katika uongozi Rais Benjamin Mkapa wananchi walilalamika kwamba pesa zimepotea ila baada ya muda uchumi ukaimarika hivyo kwa sasa wananchi waipe muda serikali ya Rais Dkt John Magufuli.

Kuhusu jitihada za kuleta maendeleo Jimboni Bashe ameeleza namna aambavyo ameanza kusaidia vijana ambapo baadhi ya vijana wanaofanya kazi ya kushona wamepelekwa Moshi kujifunza namna ya kutengeneza viatu vya ngozi kwa kuwa Jimboni anatarajia kujenga kiwanda kidogo cha ngozi.

Pamoja na hayo Bashe amewataka wawekezaji ambao wanataka kwenda kuwekeza katika jimbo lake kwenda kwa kuwa watapatiwa ushirikiano wa kutosha na eneo la ardhi tayari lipo.

WATU 283 WAJITOKEZA KUPIMA VVU/UKIMWI KWENYE MKESHA WA MWENGE WILAYANI IKUNGI


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikimbia na baadhi ya watumishi wa Wilaya yake ishara ya kuukabidhi Mwenge wa uhuru Manispaa ya singida mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani Ikungi
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi Hassan Tati akizungumza wakati wa kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kupima Virusi Vya Ukimwi
Wananchi wa Manispaa ya Singida wakiusubiri Mwenge wa Uhuru kwa shauku kubwa muda mchache kabla ya kuwasili katika eneo lao ukitokea Wilaya ya Ikungi

MWENGE WA UHURU WAPITA KATIKA MIRADI 9 WILAYANI IKUNGI



Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe akimkabidhi Mwenge wa uhuru  mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Kulia).
 Wananchi wakifatilia kwa karibu makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka Wilayani manyoni kuhamia Wilayani Ikungi
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Lucia vitalis Kamafa kutoka Manyara akiuhifadhi mwenge huo kwenye sehemu yake ya kuhifadhiwa

MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOANI SINGIDA NA ISHARA YA UHURU WA TANGANYIKA


MWENGE wa Uhuru baada ya kuwasili mkoani Singida Mwenge huu ni ni kitu mfano wa kikombe chenye mpini mrefu na utambi ambacho aghalabu huwasha na kukimbizwa katika kusheherekea au kutukuza tukio fulani
Askari wa Jeshi la Polisi wakiulinda Mwenge ishara ya kuwasili muda mfupi kabla ya kukabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Singida

Kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe tayari kwa ajili ya kumulika Miradi 18 katika Wilaya hiyo

DC IKUNGI AITAKA KAMPUNI YA SHANTA GOLD MINE KUWALIPA FIDIA WANANCHI WALIOFANYIWA TATHIMINI ILI KUPISHA UCHIMBAJI WA DHAHABU


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kilichohudhuriwa na Wawakilishi wa kampuni ya Shanta Gold Mine Ltd, Wananchi wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi
Wananchi wawakilishi kutoka Kijiji Cha Mlumbi na Uongozi wa kikosi kazi wakijadili jambo nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya kabla ya kuingia kwenye kikao
Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mine Ltd Philbert Rweyemamu akielezea namna ambavyo watawalipa wananchi 67 ndani ya wiki hii

MKOA WA SINGIDA WAPATWA NA KISHINDO CHA BURUDANI YA MSIMU WA TIGO FIESTA USIKU WA JANA


Msanii Ben Pol akiwa jukwaani  kuwapagawisha   wakazi   wa   Singida   kwenye  tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika  uwanja wa  Namfua  usiku  wa  kuamkia     jana.


Dj D Ommy akiwa katika kuhakikisha kuwa kila burudani inayotolewa na wasanii inakuwa katika utaratibu maalum katika usiku wa Tamasha la Tigo Fiesta mkoani Singida katika viwanja vya Namfua usiku wa jana.


FID Q akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta mkoani Singida katika viwanja vya Namfua usiku wa jana












JUX akiwaburudisha wapenzi wa muziki waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Namfua mkoani Singida wakati wa  tamasha la Tigo Fiesta usiku wa jana


Niki wa pili akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa jana Mkoani Singida 


Malkia wa Uswazi Snura akiwa na madancer wake katika kuwapagawisha wakazi wa Singida katika usiku wa Tigo Fiesta usiku wa jana katika viwanja vya Namfua 
Maelfu ya wakazi wa SIngida waliojitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha kubwa la burudani Tigo Fiesta lilifanyika katika viwanja vya Namfua mkoani humo usiku wa jana.

Serikali imetoa kauli kuhusu hali ya chakula nchini


Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Serikali imetoa kauli kuhusu hali ya chakula nchini na kusema kuna chakula cha kutosha pamoja na ziada ya asilimia 123. 

Ziada hiyo ya chakula inatokana na uzalishaji wa msimu wa mazao mwaka 2015/2016 ambao unapelekea upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2016/2017.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba leo mjini Dodoma alipokuwa akitoa kauli ya Serikali kuhusu hali ya chakula nchini.

“Takwimu zinaonesha upatikanaji na mahitaji ya chakula nchini ni wa kuridhisha kwa kiwango cha utoshelevu wa ziada kwa asilimia 123” Dkt. Tizeba.

Katika kufafanua hali hiyo, Dkt. Tizeba amesema kuwa kulingana na takwimu zilizopo hali ya upatikanaji na mahitaji ya chakula nchini inautoshelevu wa ziada kwa asilimia 123 ambapo nafaka ni asilimia 113 na mazao yasio ya nafaka ni asilimia 140 ambapo viwango vya ziada  kwa mazao yote ya chakula ni tani 3,013,515.

Dkt. Tizeba ameongeza kuwa Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA) inauwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 246,000 ambapo kufikia Septemba 6, ilikuwa na akiba ya tani 67,506.920 za chakula kinachojumuisha mahindi, mpunga na mtama.

Pia  amesema kuwa Serikali inaendelea na mpango wake wa kuiongezea NFRA uwezo wa kuhifadhi chakula katika kanda sita baada ya kupata mkopo wa dola za Kimarekani million 55 kutoka Serikali ya Poland ambazo zitatumika kujenga vihenge vyenye uwezo wa kihifadhi tani 190,00 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 60,000.
Kuhusu muda wa Serikali wa kutoa vibali vya kuuza chakula nje ya nchi, Dkt Tizeba amesema kuwa lengo ni kutoa nafasi kwa Serikali kukamilisha taarifa ya tathimini ya awali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2015/2016 na hali ya upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2016/2017.
Mbali na hayo, Dkt Tizeba amesema  kuwa katika kuboresha hali ya usalama wa chakula  nchini, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inapitia upya mfumo wa utoaji wa vibali vya kusafirisha chakula nje ya nchi ili kuwezesha ufuatiliaji wa karibu kuliko ilivyo sasa.
Aidha, Dkt. Tizeba amesema kuwa utoaji wa vibali vya kusafirisha mazao nje umejitokeza baada ya kuona chakula kinasafirishwa nje bila kufuata utaratibu maalumu ambapo wafanyabiashara wa nchi jirani walijihusisha kununua vyakula vikiwa bado mashambani kabla ya kuvunwa.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuhifadhi chakula cha kutosha kwa matumizi katika kaya ambapo ameitaka sekta binafsi kuendelea kushiriki katika kutoa masoko ya kununua na kuuza mazao katika maeneo yenye uhaba.
Kuhusu hali ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi inayoikabili dunia ikiwamo upungufu wa mvua , Dkt Tizeba amesema kuwa Serikali itaendelea na juhudi za kuhimiza na kupanua kilimo cha umwagiliaji mashambani kwa kuimarisha miundombinu iliyopo na uvunaji wa maji ya mvua ili kuongeza uzalishaji wa mazao wenye tija. 
Hata hivyo, Serikali inaendelea kuhamasisha na kuelimisha wafanya biashara kuuza unga nje ya nchi badala ya mahindi au mchele badala ya mpunga ili kuendana na Sera ya kuendeleza Viwanda nchini na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa