Mbunge
wa Jimbo la Nzega Mjini kupitia tiketi ya CCM Hussein Bashe amesema Rais Dkt.
John Magufuli siyo 'dikteta' kama baadhi ya watu wanavyosema bali ni kiongozi
mkali anayeshuhulikia mambo ambayo ambayo yalikuwa yamezoeleka nchini.
Akizungumza
katika kipengele cha Kikaangoni kinachoonyeshwa na ukurasa wa East Africa
Facebook, ameweka bayana kwamba kwa watu ambao walizoea kupiga dili kwa sasa
hivi wamekwama mdiyo maana wanasema ni dikteta.
“Rais
Dkt. John Magufuli siyo 'dikteta' kama maana halisi ya dikteta ilivyo , ila ni
kiongozi ambaye ni mkali ambaye anapingana na mambo ya kufanya mambo kwa
mazoeza 'Business as usual' waliokuwa wamezoea kupiga dili bandarini kwa siku
mtu alikuwa anapata laki moja au mbili sasa hiyo imekoma” Amesema Bashe.
Aidha
kuhusu baadhi ya wananchui kulalamika kwamba pesa hazionekani mtaani, Mbunge
Bashe amesema kipendi alipoingia katika uongozi Rais Benjamin Mkapa wananchi
walilalamika kwamba pesa zimepotea ila baada ya muda uchumi ukaimarika hivyo
kwa sasa wananchi waipe muda serikali ya Rais Dkt John Magufuli.
Kuhusu
jitihada za kuleta maendeleo Jimboni Bashe ameeleza namna aambavyo ameanza
kusaidia vijana ambapo baadhi ya vijana wanaofanya kazi ya kushona wamepelekwa
Moshi kujifunza namna ya kutengeneza viatu vya ngozi kwa kuwa Jimboni
anatarajia kujenga kiwanda kidogo cha ngozi.
Pamoja
na hayo Bashe amewataka wawekezaji ambao wanataka kwenda kuwekeza katika jimbo
lake kwenda kwa kuwa watapatiwa ushirikiano wa kutosha na eneo la ardhi tayari
lipo.
0 comments:
Post a Comment