Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akihutubia wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Tigo 4g LTE zilizofanyika jana mkoani singida ambapo sasa 4G LTE imeweza kufika mikoa 23 |
Wafanyakazi wa Tigo wakiwa tayari kuhudumia wateja wa Mkoa wa Singida mara baada ya uzinduzi wa Tigo 4G LTE |
Mteja akiangalia simu zenye uwezo wa 4G LTE |
Singida, Mei 22, 2017-Wateja wa Tigo mkoani Singida hivi sasa wanaweza kufurahia kuunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi kufuatia kampuni hiyo kupanua huduma yake ya 4G LTE katika mji huo uliopo katikati ya Tanzania. Teknolojia ya 4G ina takribani kasi ya mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G ambayo inapatikana hivi sasa katika soko.
Kwa mujibu wa Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba ni kwamba upanuzi wa huduma hiyo unafuatia mafanikio yaliyopatikana baada ya kuizindua katika mji mingine mikubwa nchini.
Komba alisema kwa kuifanya huduma ya 4G kupatikana Singida, “Tigo kwa mara nyingine tena imeonesha kujikita kwake katika kuboresha mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kidijitali na inavyoongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu katika soko hili.”
Alitangaza kuanza kwa enzi mpya za kidijitali katika historia ya mawasiliano ndani ya Singida akibainisha kwamba Tigo 4G LTE itahakikisha kunakuwepo uwezo mkubwa na muhimu katika kuwaunganisha wateja ndani ya mkoa huo.
“Singida ni kituo muhimu kibiashara kwa mikoa ya kati na kaskazini mwa Tanzania. Tunaamini kwamba wakazi wa Singida, jumuiya ya kibiashara na wadau wataufurahia huduma Tigo 4G LTE na hivyo kuzifanya shughuli zao kwa njia ya mtandao kuwa rahisi zaidi.”
“Mawasiliano ya simu ni nguzo muhimu kwa jamii iliyoendelea. Kwa hiyo mtandao wa 4G utachangia katika maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo elimu, fedha na huduma za afya na hali kadhalika kukuza uchumi na biashara”, alisema Komba.
“Kama mnavyojua, Tigo imekuwa mstari wa mbele katika kuzisaidia jamii zinazotuzunguka, na mfano mzuri ukiwa ni uchimbaji wa visima 12 ambavyo tulivitoa kama msaada kwa vijiji vya Singida mwaka jana,” Komba alibainisha.
Aliongeza kwamba gharama ya vifurushi vya 4G LTE ni sawa na ile ya vifurushi vya 3G na kufafanua kuwa wateja wanachotakiwa ni kuwa na kifaa kinachowezesha 4G LTE ama simu ya kisasa (Smartphone) au modemu ikiwa na kadi ya simu ya 4G LTE ili kuwawezesha kupata muunganisho na 4G LTE. Alieleza kuwa wateja wanaweza kubadilisha au kununua kadi ya simu ya 4G LTE kutoka katika duka la Tigo la huduma kwa wateja lililopo Singida Mjini.
Akizungumzia uwekezaji katika mtandao, Komba alisema kwamba Tigo imewekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu ya kisasa, ikilenga kusaidia katika maendeleo endelevu ndani ya mkoa.
Alihitimisha kwa kusema, “Mipango imo njiani katika kupanua huduma kwa ajili ya mikoa iliyobakia ili hatimaye kuisambaza nchi nzima.”
Kwa upande wake, Meneja wa mkoa wa Singida wa kampuni ya Tigo, Raymond Royer alibainisha umuhimu wa huduma ya 4G na mchango wake katika kuboresha huduma za uwanda mpana wa simu za mkononi.
Royer alisema, “Katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo ongezeko kubwa la idadi ya wateja pamoja na matumizi ya data; simu za kisasa idadi yake imeongezeka kwa asilimia 90 na hivyo kubadilisha namna tunavyowasiliana.”
Aliongeza, “Kwa hiyo teknolojia ya Tigo 4G LTE inampatia mteja faida mbili za data zilizo na kasi kubwa na kupunguza ucheleweshaji. Ni nguvu ya mabadiliko ambayo itaboresha mtindo wa maisha ya kidijitali kwa wateja wetu.”
Mtandao wa 4G LTE unamaanisha kasi kubwa katika kurambaza (Surf) na kupakua mada kutoka katika intaneti na kupiga miito ya mawasiliano ya kuonana (Skype). Kwa kiwango kikubwa inaboresha uzoefu wa wateja katika kutiririsha video au kufanya mikutano. Hali kadhalika inaweza kuhifadhi zana nyingi kama vile mkutano wa video, muonekanao wa hali ya juu, blogu za video, michezo na kutiririsha video kutoka katika mitandao ya kijamii.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment