Wanawake
wa Vijiji vya Merya na Ikugha katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida
wameushukuru Mwenge wa Uhuru kwa kuwafungulia mradi ambao umewaepusha
kutembea umbali mrefu kutafuta maji ya kutumia ambayo si safi wala
salama huku wakiyachangia na mifugo yao.
Wanawake
hao wametoa pongezi hizo mara baada ya kiongozi wa mbio za mwenge wa
uhuru Amour Hamad Amour kufungua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 49 utakaohudumia vijiji hivyo ambao umegharimiwa na
shirika la saving International, halmashauri ya Singida pamoja na
michango ya wananchi.
Wamesema
kabla ya kupatikana mradi huo wanawake wa vijiji hivyo wamekuwa
wakifuata maji umbali mrefu sana kiasi cha kushindwa kutekeleza shughuli
nyingine za kuzalisha mali.
“Tulikua
tunatembea mpaka tunachoka, tunaamua kupumzika njiani kwanza ndio
tuendelee na safari ya kuleta maji nyumbani, yani tunashukuru sana
kwakweli”, ameongea Bi Greta Senge Mkazi wa kijiji cha Ikugha.
Aidha
wameongeza kuwa mradi huo utawapatia maji safi na salama kwakuwa maji
waliyokuwa wakiyafuata umbali mrefu hapo awali yalikuwa machafu na si
salama.
“Yani
tulikuwa tunachota maji ambayo unakuta ng’ombe anakunywa hapohapo,
wakati mwingine anajisaidia na inabidi uchote hivyo hivyo, kwakweli
tunaushukuru sana mwenge kutufungulia mradi huu, tulikua tunaumwa
matumbo kila mara”, ameongeza Rehema Lazaro.
Wameongeza
kuwa mradi huo utapunguza magonjwa ya tumbo na macho ambayo yamekuwa
yakiwasumbua mara kwa mara hukua wakiridhia kulipia kiasi cha shilingi
50 kwa lita 20 za maji ili kupata fedha za kutunza mradi huo.
Kwa
upande wake kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour
ameitaka jumuiya ya watumia maji ya mradi huo kuutunza mradi huo ili
utoe maji kwa wingi na muda huo kutokanana kuonekana ni hitaji la
muhimu.
“Nimefika
hapa na kushuhudia akina mama wengi mnamiminika na ndoo ili mpate maji,
hii ni ishara kuwa mradi huu ni muhimu hivyo basi jumuiya ya watumia
maji hakikisheni mda wote maji yanatoka na sio kupanga masaa ya kutoa
maji au mvua ikinyesha tu mnayafunga, hapana” amesisitiza Amour.
Amesema
mradi huo usimamiwe vizuri kusiwe na upendeleo au ubaguzi wowote
kwakuwa maendeleo hayo hayana ubaguzi wa rangi, dini, itikadi za kichama
au makabila.
Amour
amesema jumuiya hiyo ihakikishe miundombinu ya mradi huo inatunzwa ili
kuepusha kuwarudisha akina mama hao katika shida waliyokuwa wakiipata
awali huku akiwashauri kuangalia namna ya kuipatia mifugo maji pamoja na
kuweka taratibu nzuri za mapato na matumizi ya mradi huo.
Wakati
huo huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amezindua mradi wa
umwagiliaji mbogamboga kwa njia matone wa ekari 25 wenye thamani ya
shilingi milioni 326 katika kijiji cha Msange.
Akisoma
taarifa ya mradi huo Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Singida
Adam Mngale amesema mradi huo ulianzishwa mwaka 2012 na hadi sasa una
wanachama 32 ambao wananufaika kwa kujiongezea kipato kutokana na kulima
misimu miwili yani kiangazi na masika.
Mngale
amesema malengo ya mradi huo ni kuongeza eneo la uzalishaji hadi
kufikia ekari 1400, kupanua miundombinu ili waweze kutumia kutumia bwawa
la suke na lililoko eneo jirani katika umwagiliaji na kutumia kiwanda
cha kusindika mbogamboga kilichoko Msange kusindika mazao yao.
0 comments:
Post a Comment