Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mzee
maarufu na mwenyeji wa Msange Bi Greta Musa Nyonyi akichangia hoja
katika semina ya kupinga Ukeketaji iliyofanyika katika Kata ya Msange
Wilayani Singida.
Mratibu
wa Mradi wa Kupinga Ukeketaji (WOWAP) Nasra Suleiman akizungumza na
washiriki wa semina ya kupinga Ukeketaji iliyofanyika katika Kata ya
Msange Wilayani Singida.
Afisa
Maendeleo ya Jamii kata ya Msange Magni Oisso akichangia hoja katika
semina ya kupinga Ukeketaji iliyofanyika katika Kata ya Msange Wilayani
Singida.
Washiriki
wa semina ya kupinga ukeketaji iliyoandaliwa na Mradi wa WOWAP
wakifuatilia kwa umakini filamu fupi ya Ukeketaji iliyofanyika katika
Kata ya Msange Wilayani Singida.
Mzee
wa Kimila Hosea Mnyambi akichangia hoja katika semina ya kupinga
Ukeketaji iliyofanyika katika Kata ya Msange Wilayani Singida.
Elimu
sahihi juu ya madhara ya ukeketaji ya muda mfupi na mrefu inatakiwa
itolewe kwa jamii kabla ya kuwachukulia hatua baadhi yao wanaoendelea
kufanya vitendo vya ukeketaji licha ya uwepo wa sheria kali.
Rai
hiyo imetolewa mapema leo na Mratibu wa Mradi wa Kupinga Ukeketaji
(WOWAP) Nasra Suleiman katika semina ya kupinga Ukeketaji iliyofanyika
katika Kata ya Msange Wilayani Singida, kwa ushirikiano wa Ofisi ya
Ustawi wa Jamii Mkoa wa Singida na mradi huo kwa ufadhili wa shirika la
WAAF-Japan.
Mratibu
huyo amesema nguvu ya sheria itasaidia kuondoa ukeketaji endapo
wananchi wengi watakuwa na uelewa wa kutosha juu ya madhara ya ukeketaji
na kuamua kwa hiyari kuachana na mila hiyo.
“Sheria
isiwe nguvu pekee ya kupambana na ukeketaji, tukifanya hivyo itafikia
kipindi tutakwama kwa kiasi kikubwa kwa kuwa watu wataendelea kukeketa
kwa kificho ili wasikamatwe, lakini kila mwana jamii akiwa na elimu ya
kutosha ya madhara hayo, nguvu ya sheria itatumika tu kwa wachache watao
kaidi”, amesisitiza Nasra.
Ameongeza
kuwa Watendaji wa kata na vijiji wana uwezo mkubwa wa kubadilisha
mtazamo na mila ya ukeketaji kwa kuelimisha wananchi wao hasa baada ya
semina zinazoandaliwa na miradi au mashirika Fulani kwakuwa zinawajengea
uwezo ili waweze kutoa elimu sahihi na mbinu za kuelimisha.
Nasra
amesisitiza kuwa jukumu la elimu lisiachwe kwa sekta binafsi kama mradi
wake wa WOWAP pekee bali liwe jukumu la jamii nzima huku akifafanua
kuwa elimu inayotakiwa kutolewa ni ile inayoelezea madhara ya ukeketaji
na sio kuwakataza kwa kigezo cha kutii sheria pekee.
Naye
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Msange Magni Oisso amesema katika kata
hiyo ukeketaji umekufanyika kwa siri sana kwa kuogopa mkono wa sheria
huku wahanga wakiwa watoto wachanga na wale waliomaliza kliniki.
Oisso
amesema kumekuwa na usiri mkubwa huku wakeketaji wakibadili mbinu namna
za kujificha wasigundulike kwa jamii ambayo elimu imeanza kuwafikia
baadhi yao.
Aidha
amependekeza kuwa ili kukomesha ukeketaji moja ya njia ni kutoa elimu
katika vituo vya kutolea huduma za uzazi na mtoto ili mtoto aweze
kunusurika pia elimu itolewe shuleni kwa ngazi zote kuanzia darasa la
awali hadi la saba.
Akichangia
mada katika semina hiyo mzee maarufu na mwenyeji wa Msange Bi Greta
Musa Nyonyi amesema elimu ni bora zaidi kuliko kuwaogopesha wanajamii
kwa kutumia sheria kwakuwa watatafuta namna ya kutekeleza azma yao kwa
usiri ili kukwepa mkono wa sheria na sio kuacha.
Greta
ameongeza kuwa kwa sasa kutokana na kuwa wakeketaji wamebainika kuwa
wanakeketa watoto wachanga na hugundulika wakienda kliniki baadhi yao
wanabadili mbinu na kusubiri mtoto amalize kliniki ndipo anakeketwa.
Naye
Mzee wa Kimila Hosea Mnyambi amesema yeye amekulia katika familia ya
wakeketaji na wamekuwa wakirithishwa mbinu za ukeketaji kizazi hadi
kizazi ila kutokana na kuwepo kwa sheria, dini kuhubiri madhara ya
ukeketaji, mila hiyo wameiacha.
Amesema
wachache wanaoendelea kufanya vitendo hivy o ha wanawake wamekuwa
wakifanya kwa usiri mkubwa huku akina baba wakiwa hawana taarifa ya
kinachoendelea na endapo mtoto anafariki hudanganywa ugonjwa uliopelekea
kifo cha mtoto.
Mzee
Mnyambi amesema elimu iendelee kutolewa hasa kwa kutumia vyombo
vinavyoaminika mfano vyama vya siasa, dini na vikundi vya kuweka na
kukopa pamoja na kuiweka agenda ya ukeketaji kwa vikao vya Kata na
vijiji.
0 comments:
Post a Comment