Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu wa Chama Cha Mpira wa miguu wilaya ya Manyoni (MADIFA) Joshua Msemakweli (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi wa timu pamoja na wachezaji wa timu zilizoshiriki mchezo wa fainali katika kata ya Sanjaranda.
MASHINDANO
ya ligi ya kombe la Diwani wa kata Saranda, Tarafa ya Kilimatinde,
wilayani Manyoni, Mkoani Singida yamefikia tamati kwa timu ya soka ya
ILALOO FC kuwa mabingwa wa kombe hilo kwa mwaka huu wa 2017 baada ya
kuifunga timu ya Saranda FC kwa jumla ya magoli 2-1.
Ligi
hiyo iliyoanza kuchezwa juni, 29 mwaka huu kwa makundi mawili
yaliyokuwa yakivitumia viwanja vya michezo vya Shirika la reli Tanzania
(TRC) ilizishirikisha jumla ya timu sita za kata hiyo ambazo ni pamoja
na Saranda FC, Ilaloo FC, Irucha, Mlimani A, Mlimani B na Mhegahega FC.
Akitangaza
matokeo ya mashindano hayo, Katibu wa Chama Cha mpira wa miguu wilaya
ya Manyoni (MADIFA), Joshua Msemakweli aliwataka vijana hao kuwekeza
kwenye mchezo wa soka kwa kuamini kwamba michezo ni afya na michezo ni
ajira.
“Mashindano
ngazi ta kata ya Saranda yalishirikisha timu sita kutoka katika vijiji
na vitongoji,ambavyo ni Kijiji cha Saranda ambapo ndipo makao makuu ya
kata pia Ilaloo na Irucha zipo Kijiji cha Saranda Kijiji cha Saranda
kilikuwa na timu tatu”alifafanua Msemakweli.
Kwa
upande wake muandaaji wa kombe hilo ambaye pia ni diwani wa kata ya
Saranda,Joseph Ndahani aliyataja baadhi ya malengo ya michezo hiyo kuwa
ni kuhakikisha wanakuza pamoja na kuvitangaza vipaji wa vijana wa kata
hiyo kupitia sekta ya michezo.
Naye
Mwalimu wa timu ya soka ya Ilaloo FC ambao ndiyo mabingwa wa kombe
hilo, Rashid Juma alikishukuru kituo hiki kwa kuweza kufika katika Kata
hiyo na kuwawezesha kusikika maana haijawahi kutokea bahati kama hiyo
kwa vituo vingine kufika huko.
0 comments:
Post a Comment