Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Mkoa wa Singia Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na Meya wa Manispaa ya
Singida Gwae Chima Mbua kabla ya kuanza kwa baraza Maalumu la madiwani
wa Manispaa ya Singida kujadili hoja za Mkaguzi wa Fedha za Serikali.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Singida Bravo Kizito Lyampembile akifungua baraza
Maalumu la madiwani wa Manispaa ya Singida kujadili hoja za Mkaguzi wa
Fedha za Serikali.
Baadhi
ya Viongozi wa Manispaa ya Singida wakifuatilia baraza Maalumu la
madiwani wa Manispaa ya Singida kujadili hoja za Mkaguzi wa Fedha za
Serikali.
Madiwani wa manispaa ya Singida wakifuatilia baraza Maalumu la madiwani
wa Manispaa ya Singida kujadili hoja za Mkaguzi wa Fedha za Serikali.
Madiwani
wa manispaa ya Singida wakiwa wamesimama kuridhia hoja katika baraza
Maalumu la madiwani wa Manispaa ya Singida kujadili hoja za Mkaguzi wa
Fedha za Serikali.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema hatavumilia kuona
halmashauri inafanya uzembe na kupata hati chafu ya Mkaguzi na Mdhibiti
wa Fedha za Serikali kwakuwa itamchafua yeye na taswira ya uongozi wote
wa Mkoa wa Singida.
Dkt
Nchimbi ametoa kauli hiyo mapema jana wakati wa baraza maalumu la
madiwani wa Manispaa ya Singida la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti
wa Hesabu za serikali ambazo amesema hoja nyingi zimetokana na uzembe.
Amesema
licha ya kuipongeza Manispaa ya Singida kwa kupata hati safi, uwepo wa
hoja umedhihirisha kuwa kuna baadhi ya watendaji wanafanya kazi kwa
uzembe na kutofuata taratibu na sheria hivyo wajirekebishe haraka.
Dkt
Nchimbi ameongeza kuwa hoja nyingi zinajitokeza kwa kukosa umakini na
watendaji kufanya kazi kwa mazoea hali ambayo ikiendelea inaweza
kuipelekea manispaa kupata hati isiyoridhisha hivyo kupata hati safi
kuwaongezee nguzu ya kuboresha utendaji kazi wao.
Aidha
amewashauri wakuu wa idara na watumishi wengine kuitendea haki manispaa
yao kwa kuchapa kazi kuwa wadilifu na kufuata sheria kwani wakifanya
hivyo wataepuka hoja zisizo za lazima na kuharakisha maendeleo.
Dkt
Nchimbi amewasisitizia matumizi ya muda kuwa yenye tija ambapo amelaani
kitendo cha kutumia muda mwingi kwenye vikao ambavyo havina tija bali
watumie muda kidogo kwenye vikao na muda mwingi kutatua kero za
wananchi, huku akiahidi kufuatilia matumizi ya muda unaotumika kwenye
vikao.
Ameongeza
kuwa watendaji wote wanapaswa kubadilika na kuendana na kasi ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Hapa kazi tu ili waweze kupunguza
hoja na kufuta zile zisizo za lazima.
Kwa
upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Lutambi amewaasa
watendaji kuitumia vema dhamana ya utumishi wa umma kwa kuhakikisha
wanaleta mabadiliko ya kimaendeleo.
Dkt
Lutambi ameongeza kuwa watumishi wa umma wanapaswa kufahamu kuwa
jutendaji wao ukilega lega athari yake inamkumba mwananchi kwakuwa
atachelewa kupata maendeleo, hivyo bidii katika utumishi umma ni muhimu.
Amewasisitizia
kuwa mikakati na malengo ya maendeleo ya kimkoa na kitaifa haitaweza
kufikia endapo watendaji hawatakuwa waadilifu na wakiendekeza uzembe
hivyo wajitume kwa bidii kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.
Naye
Diwani Viti maalumu Magreth Malecela amemshukuru Mkuu wa Mkoa Dkt
Nchimbi kwa kuwapa vyeti ambavyo vilitolewa kwa madiwani wote waliopata
mafunzo ya usimamizi wa ruzuku na miradi ya serikali.
Malecela
ameongeza kuwa ushirikiano na ushauri wanoaupata kutoka kwa Dkt Nchimbi
utaisaidia manispaa kuwa na maendeleo huku akiahidi kwa niaba ya
madiwani wenzake kuwa watafuata maelekezo na ushauri kwa manufaa ya
manispaa ya Singida.
0 comments:
Post a Comment