Katibu
Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida Beatus Chowaji
akisoma bango mara baaa ya kuzindua mradi wa Faida Mali unaoshirikiana
na shirika la AMDT katika kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida.
Mkurugenzi wa Shirika la AMDT Michael Kayombo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Faida Mali wenye lengo la kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida kulima kibiashara.
Baadhi
ya wadau waliohudhuruia uzinduzi wa mradi wa Faida Mali wenye lengo la
kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida kulima kibiashara.
Mkurugenzi
wa mradi wa Faida Mali mkoa wa Singida Tom Silayo akisoma taarifa ya
mradi huo kwa wajumbe waliohudhuria uzinduzi wa mradi utakaowasaidia
wakulima kulima alizeti kibiashara.
Mtendaji
Mkuu wa Chama cha wasindikaji wa Mbegu za alizeti Tanzania Daud Musa
Mwasantaja akiwahakikishia wakulima wa alizeti upatikanaji wa soko
katika uzinduzi wa Mradi wa Faida Mali.
Wauzaji
wa pembejeo ambao sio waaminifu wamepewa onyo kali na endapo atabainika
yeyote anayewalaghai wakulima na kuwauzia pembejeo ambazo sio hali
hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.
Katibu
Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida Beatus Chowaji
ametoa onyo hilo wakati akizindua mradi wa Faida Mali unaoshirikiana na
shirika la AMDT katika kuwasaidia wakulima wa alizeti Mkoani Singida ili
kulima zao hilo kibiashara zaidi.
Chowaji
amesema kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya wakulima ambao hukumbana
na wauzaji wa pembejeo ambao sio waaminifu na kuwalaghai kwakuwa
wakulima hao hawana elimu na uelewa hasa wa viuatilifu au mbegu ambazo
ni halisi.
Ameongeza
kuwa mkono wa serikali ni merfu na utawabaini popote walipo hivyo
waache mara moja kwani kwa kufanya hivyo wanakirudisha nyuma kilimo cha
alizeti ambacho ni tegemeo kwa ajili ya uchumi wa viwanda Mkoani
Singida.
“Singida
tuna Viwanda vya kuamua mafuta ya alizeti vikubwa viwili, vya kati
vitatu na vidogo 115 na kufanya jumla ya viwanda vya alizeti kuwa 120,
vyote hivyo vinategemea alizeti ya mkulima, lakini pia mkulima anakuwa
na matarajioa makubwa, hao wauzaji pembejeo wasio waaminifu
hatutawavumilia, tena waache mara moja”, amesisitiza Chowaji.
Aidha
amelipongeza shirika la AMDT kupitia mradi wa Faida mali kwa kuuchagua
Mkoa wa Singida ili kuboresha kilimo cha alizeti hasa kwa ajili ya
mkulima mdogo.
Chowaji
amesema viwanda vya alizeti Mkoani Singida hufanya kazi kwa miezi
minane kwa mwaka badala ya mwaka mzima kutokana na kuwa alizeti
inayozalisha bado haitosheleshi viwanda hivyo kufanya kazi mwaka mzima.
Amesema
matumaini makubwa ya serikali mkoani hapa ni kuwa mradi huo utasaidia
kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kuifanya Singida ya Viwanda kuwa
bora zaidi pamoja na kuliboresha zao lenyewe la alizeti kwa kutumia
pembejeo za kisasa zaidi.
Chowaji
amewataka wakulima wote wa alizeti kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiunga
katika vikundi ili waweze kufikiwa kwa urahisi na kunufaika, pia waache
kilimo cha mazoea kwakuwa alizeti ni biashara kubwa ambayo itawakomboa
kiuchumi na kukupa pato la mkoa wa Singida.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Shirika la AMDT Michael Kayombo amesema
shirika hilo kupitia Mradi wa Faida mali utahakikisha unasaidia
upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wadogo wa alizeti Mkoani singida.
Kayombo
ameongeza kuwa mradi utaboresha huduma za ugani kwa kutoa taarifa
sahihi na mapema juu ya kilimo cha alizeti kwa wakulima na taarifa hizo
zitatolewa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno hivyo kuwafikia mapema.
Amreongeza
kuwa watahakikisha wakulima wanapata soko la uhakika la zao hilo ndani
na nje ya mkoa wa singida pamoja na kuhakikisha bei ya zao hilo ni yenye
kumnufaisha mkulima na sio kumdidimiza zaidi.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Chama cha wasindikaji wa Mbegu za alizeti Tanzania
Daud Musa Mwasantaja amesema viwanda vya alizeti bado vina uhitaji
mkubwa wa alizeti kwa kuwa viwanda vyao vimekuwa vikiendeshwa chini ya
malengo kutokana na mbegu hizo kuwa chache.
Mwasantaja
amesema wana imani kuwa mraadi wa Faida Mali utasaidia kuongeza
uzalishaji wa alizeti hivyo kuwasaidia kuongeza pia uzalishaji katika
viwanda vyao.
Ameongeza
kuwa watatoa ushirikiano wa kutosha na hivyo wakulima wasiwe na
wasiwasi walime zao hilo kwa wingi watapata wateja na kwa bei ambayo ni
nzuri.
Nao
wakulima walioshiriki uzinduzi wa maradi huo wamesema mradi huo umekuja
muda muafaka kwakuwa na wao wanatamani kupata faida kutokana na kilimo
hicho kwakuwa baadhi bado wanalima kwa mazoea na kwa kutumia mbegu
ambazo hazizalishi kwa wingi.
0 comments:
Post a Comment