MO ALIPOFIKA SINGIDA KWA AJILI YA KUPIGA TAFU KAMPENI ZA URAIS

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

IMG_4146
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akisalimiana na mmoja wa madiwani waliofika kumpokea mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Singida mjini pamoja na wasaidizi wake.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_4126
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akiwa ameambatana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli, January Makamba ambaye pia ni mmoja wa wanakamati wa timu ya ushindi ya kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli, wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Singida mjini.
IMG_4130
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akilakiwa kwa furaha na watoto wanaoishi kwenye eneo la uwanja wa ndege Singida mjini.
IMG_4131
Watoto wakimpokea kwa shangwe aliyekuwa Mbunge wao jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Singida mjini kwa ajili ya kuhudhuria kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli pamoja na kumuombea kura kwa wana Singida.
IMG_4137
Pichani juu na chini ni Mohammed Dewji akibadilishana mawazo na watoto waliojitokeza kumpokea uwanjani hapo.
IMG_4142
IMG_4150
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akiagana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli ambaye pia ni mmoja wa wanakamati wa timu ya ushindi ya kampeni za Dkt. Magufuli, January Makamba kabla ya kuelekea kwenye viwanja vya Peoples Singida mjini ulipofanyika mkutano wa kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli. Kulia ni Msaidizi wa MO, Duda Jumanne.
IMG_4157
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akipata picha ya ukumbusho na wanaSingida wanaoishi karibu na maeneo ya uwanja wa ndege wa Singida mjini.

DK MAGUFULI, CHILOLO WAISAMBARATISHA NGOME YA TUNDU LISSU SINGIDA MASHARIKI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi katika Jimbo la Manyoni, mkoani Singida, wakati wa mkutano wa kampeni. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akitoa ahadi mbalimbali kwa wananchi kuhusu elimu ya bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, utaratibu utakaoanza mwakani endapo wananchi wakimpa ridhaa ya kuongoza nchi.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiombewa dua na Imamu wa Msikiti wa Puma,Ramadhan Khamis Jimbo la Singida Magharibi, baada kujinadi kwa wananchi waliouzuia msafara wake uliokuwa ukitoka wilayani Manyoni kwenda Singida Mjini
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Jimbo la Singida Mashariki, Diana Chilolo, akipongezwa na Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli baada ya kusaidia kumnadi wakati wa mkutano wa kampeni katika jimbo hilo lililokuwa linaongozwa na Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Chilolo alimsambaratisha Lowassa na Tundu Lissu kwamba hawastahili kuwa viongozi kwani hata katika majimbo yao hakuna maendeleo waliyoyafanya. Pia alisema afya ya Lowasa haimruhusu kuongoza nchi..
 Wananchi wa Ikungi wakishangilia wakati Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli  akihutubia katika mkutano wa kampeni katika Jimbo la Singida Magharibi 
 Mtoto Salum Juma akiwa amembeba mdogo wake Thabit huku wakiwa na bendera za CCM wakati wa kampeni katika Jimbo la Bahi, Dodoma.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wananchi wakishangilia walipomzuia  Dk Magufuli katika Kijiji cha Kintinku, wilayani Manyoni.

 Wananchi wakishangilia walipomzuia  Dk Magufuli katika Kijiji cha Kintinku, wilayani Manyoni.

 Mama Mkazi wa Manyoni akishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni
 Mkazi wa Manyoni,  mkoani Singida, akishangilia huku akiwa na mwanawe baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni
 Dk. Magufuli akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika kutano wa kampeni mjini Manyoni, Singida leo.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mkazi wa Manyoni akimshikilia mtoto ili amuone Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni mjini Manyoni
 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la ManyoniMashariki , Daniel Mtuka wakati wa mkutano wa kampeni mjini Manyoni.
 Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia CCM Mkoa wa Singida, akijitambulisha kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Manyoni..PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kupitia CCM, Nyalandu akiwasalimia wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Manyoni
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Manyoni
 Wananchi wa Itigi jimbo jipya la Manyoni Magharibi wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli
 Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni mjini Itigi, Manyoni
 Dk Magufuli akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Manyoni Magharibi kupitia CCM, Yahya Masale
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Tunda Man akitumbuiza katika mkutano wa kampeni Ikungi Jimbo la Singida Mashariki
 Dk Magufuli (wa sita kushoto) akiwa jukwaani akiangalia wakati msanii Tunda Man akitumbuiza katika mkutano wa kampeni mjini Ikungi, Singida Mashariki
 Temba na Chege wakitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni Ikungi Jimbo la Singida Mashariki
 Kikundi cha TOT kikitumbuiza wakati wa mkutano huo
 Mzee akijikinga jua kali kwa kutumia bango lenye picha ya Dk Magufuli
 Wasanii wa ngoma za asili Jimbo la Singida Mashariki wakiangalia picha za Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ikungi
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Jimbo la Singida Kaskazini, Diana Chilolo akimpigia debe mgombea ubunge Jimbo la Singida Mashariki kupitia CCM,Jonathan Njau na Dk Magufuli wakati wa kampeni mjini Ikungi.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Dk Magufuli akimnadi kwa wananchi Mgombea ubunge Jimbo la Singida Mashariki, Jonathan Njau wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ikungi leo
 Dk Magufuli akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Magharibi, Eribaliki Kingu wakati wa mkutano huo wa kampeni mjini Ikungi.
Mkazi wa Kijiji cha Puma, mkoani Singida, akishangilia alipokuwa akikimbilia kumuona Dk Magufuli aliyezuiwa barabarani na wananchi wa eneo hilo ili awahutubie.

DK. JOHN POMBE MAGUFULI: NITASHIRIKIANA NA MASHIRIKA YA DINI KATIKA SUALA ZIMA LA AFYA KWA JAMII‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida wakati akiwaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.
Dk. Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inazisaidia taasisi mbalimbali hasa za mashirika ya dini ambazo zinaendesha hospitali katika kupata vifaa, Ruzuku, na ajira kwa wafanyakazi ili kuimarisha huduma za kiafya kwa jamii.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE IKUNGI -SINGIDA)
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Singida Mashariki Jonathan Njau wakiwapungia wananchi mikono kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi leo.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida Diana Chilolo akimpigia debe Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi.
????????????????????????????????????
Mmoja wa wasanii walikokuwa wakitumbiuza katika mkutano huo akiwa ameshikilia bango lenye picha ya mgombea ubunge wa jimbo la Singida Mashariki Ndugu Jonathan Njau katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Mnadani Ikungi leo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya akina mama wakiwa wamekaa kandokando ya mkutano huo huku mmojawapo akiwa ameshilikilia picha ya Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea huyo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakiwa wameshikilia vipeperushi vyenye ujumbe wa kampeni za mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli huku wakimsikiliza wakati alipokuwa akihutubia katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mgombea Ubunge wa jimbo la Singida Magharibi Lazaro Nyalandu akipmigia debe Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani ambapo amewaambia wananchi wa jimbo hili kujifikiria mara bili na kuchagua mbunge kupitia CCM ili waweze kusonga mbele kwa maendeleo kutokana na kudorora kwa muda mrefu kwa sababu ya kukwamishwa na mbunge kupitia upinzani aliyeshindwa kuwaletea maendeleo kwa muda wote wa miaka mitano.
????????????????????????????????????
Kada wa Chama cha Mapinduzi kutoka mkoani Tabora aliyejiunga na CCM hivi karibuni akitokea Chadema Mtemi Nyanda akimpigia debe Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Kundi la TOT likitumbuiza katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Chege na Temba kutoka TMK Family wakitumbuiza katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Msanii Msami pamoja na kundi lake wakitumuiza katika mkutano huo uliofanyika Ikungi kwenye uwanja wa Mnadani mkoani Singida.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wana CCM wakifurahia jambo wakati Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia .
????????????????????????????????????
Burudani zikiendelea.
????????????????????????????????????
Msafara wa Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuliukiwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgombea ubunge wa jimbo la Singida Magharibi Mh. Lazaro Nyalandu katika mkutano wa kampeni uliofanyika Manyoni.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakiwa na shamrashamra wakati wakimpokea Dk. John Pombe Magufuli hayupo pichani alipowasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Manyoni mkoani Singida
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Manyoni Daniel Mtuka katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Manyoni kushoto ni Kapteni John Chiligati aliyestaafu na kumwachia kijiti mgombea huyo.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya uchaguzi mgombea ubunge wa jimbo la Manyoni Daniel Mtuka katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Manyoni
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa akisalimiana na Mh. Lazaro Nyalandu mgombea ubunge wa jimbo la Singida Magharibi.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Bahi Mh. Omary Ahmed Badwel katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Bahi.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa kulia na mgombea ubunge wa jimbo la Bahi Mh. Omary Ahmed Badwel katika mkutano wa kampeni uliofanyika Babati
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa