Zoezi la kuhuisha taarifa za benki NMB Singida lazorotesha shughuli za uzalishaji.


Zoezi linaloendelea la wateja wa NMB tawi la Singida limesababisha foleni kubwa kitendo kinachochangia wateja kupoteza muda mwingi kuwasilisha taarifa zao mpya. Hata hivyo wateja wa NMB walipewa takribani mwaka mzima kuhuisha taarifa zao lakini wengi wamesubiri hadi tarahe ya mwisho kukamilisha zoezi hilo. (Picha na Nathaniel Limu).
Picha Zote kwa Hisani ya MO BLOG

KIBAKA ANAYETUHUMIWA KUIBA SIMU AKILA KICHAPO KIKALI KUTOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.


 Kijana anayedhaniwa kuwa ni kibaka katika eneo la soko kuu mjini Singida, akisulubiwa kwa kupigwa na mateke na mawe baada ya kutuhumiwa kumwibia simu ya mkononi msichana (kulia) anayemshikilia.
Kijana huyo akipaa baada ya kupigwa ‘mtama’ kwa tuhuma ya kukwapua simu ya mkononi ya msichana (wa pili kulia).
Picha Na Singida Yetu

Raia wa Rwanda apoteza maisha katika ajali ya gari mkoani Singida.


Gari aina ya nissan presage axis C.6017 A, mali ya Abbakari  Bakudikiza (32) raia wa Rwanda baada ya kupata ajali kwenye kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida na kupelekea Abbakari kufariki dunia papo hapo. Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na mke wake raia wa Sweden Videl Ruze ambaye alipata majeraha kichwani na amelazwa hospital ya mkoa na hali yake inaendelea vizuri. Wanandoa hao ambao wameoana miezi sita iliyopita, walikuwa wakitoa Dar-es-salaam kuelekea Rwanda.

Mwanaume raia wa Rwanda Abbukari Bakudukiza (32) amefariki dunia hapo hapo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria na mke wake kupata ajali. Ajali hiyo imetokea baada ya kupasuka tairi la mbele na kuacha njia na kisha kupinduka.
Mke wa Abbakari raia wa Sweden ambaye alikuwa akiendesha gari hilo ni Videl Ruze (35).
Gari la familia hiyo ni Nissan presage axis C.6017 A.
Akizungumza na Singida Yetu Blog mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dk. Suleiman Muttani, amesema kuwa
ajali hiyo mbaya, imetokea  katika eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida.
Amesema Abbakari amefariki kutokana na kuvunja damu nyingi baada ya kupata majeraha makubwa kichwani.
  Dk.Muttani amesema Videl aliyekuwa akiendesha gari hilo yeye amepata michumbuko sehemu za kichwani na amelazwa wodi namba tano, katika hospitali ya mkoa mjini Singida na hali yake inaendelea vizuri, huku mwili wa Abbakari ukihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa.
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi aliyemtembelea majeruhi Videl wodini amesema kuwa majeruhi Videl amedai kuwa katika safari yao hiyo ya kutoka Dar-es-salaam wakielekea Rwanda njiani walipata pancha mara mbili.
“Majeruhi huyo amesema kuwa wameoana na Mnyarwanda huyo miezi sita iliyopita na kwa sasa ana mimba changa. Amedai walipoanza kuteremka mteremko wa Kisaki, ndipo tairi la mbele lilipobasti na kupelekea kushindwa kulimudu gari hilo”,alisema.
Mlozi amesema kuwa tayari amekwisha wasiliana na ubalozi wa Rwanda nchini na ndugu wa Abbakari wapo njiani kuja kuchukua mwili wa marehemu.
Kwa upande wa mwanamke huyo kutoka Sweden, amesema pia amewasiliana na ubalozi wa Sweden nchini na wao wanafanya utaratibu wa kuja kumwona majeruhi huyo.

Watatu wapoteza maisha mkoani Singida katika ajali ya basi kutokana na uzembe wa dereva na mwendo kasi.


Abiria mmoja raia wa nchini China, ambaye jina lake halikufahamika mara moja ambaye amevunjika mguu wa kushoto akipewa huduma za matibabu mara baada ya ajali ya basi la Green star lililogonga lori la mbao katika eneo la kijiji cha Isuna wilaya ya Ikungi.
Baadhi ya majeruhi wakiwa nje ya maabara ya hospitali ya mkoa wa Singida,wakisubiri kupata matibabu.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Singida,wakiwa nje ya maabara ya hospitali ya mkoa,kuwaona majeruhi wa ajali ya basi la Green star iliyotokea jana (10/3/2013) katika kijiji cha Isuna wilaya ya Ikungi.(Picha na Nathaniel Limu).
Watu watatu wamefariki dunia baada ya basi T.939 BRA aina ya Yutong, lililokuwa likitokea Dar-es-salaam likielekea Kahama mkoani Shinyanga, kugonga kwa nyuma lori T.268 CCC likivuta tela T.931 CBU aina ya Scania.


Watu hao waliofariki kwenye ajali hiyo ni dereva wa basi hilo Yassin Ramadhani (39) na msaidizi wake (utingo) Mansory Mohamed (30).
Wafanyakazi hao wa basi hilo wamefariki wakiwa wanapatiwa matibabu kwenye maabara ya hospitali ya mkoa mjini Singida.
Mwingine aliyefariki kwenye ajali hiyo ni mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na miaka mitano ambaye alifariki papo hapo kwenye eneo la tukio, hata hivyo,jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa alimesema ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Nkuhi tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi katika barabara kuu ya Dodoma – Mwanza.
Amesema pia katika ajali hiyo, jumla ya abiria 20 wakiwemo raia watano kutoka China na Uganda, walijeruhiwa na wamelazwa katika hospitali ya mkoaya mjini Singida wakipatiwa matibabu.
Sinzumwa ametaja raia kutoka China waliojeruhiwa ni Pisha Leng (45) amevunjika mguu wa kushoto, Changshing Chang (43) na Guongrung Gang na wote wanafanya kazi katika kampuni ya CCCC iliyopo Nzega mkoani Tabora.
Ametaja raia wengine kutoka Uganda kuwa ni Swahibu Semgenyi (50) amevunjika mguu wa kulia, Everine Mbine (33) na Tusime Aneti (33) na wote ni walimu kutoka chuo cha Uganda.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo kutaka kulipita lori lambao ambalo lilikuwa mbele.
Kamanda Sinzumwa ametumia fursa hiyo, kuwakumbusha madereva wa vyombo vya moto kujenga utamaduni wakuchukua tahadhari wakati wote ili kupunguza uwezekano wakutokea kwa ajali zinazosababisha vifo na uharibifu wa mali.
Picha kwa hisani ya Audiface blog..
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa