Home » » NSSF yashauriwa kusaidia wasanii.

NSSF yashauriwa kusaidia wasanii.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
index 
Meneja  wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso.

Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii( NSSF) Mkoa wa Ruvuma  limeshauriwa kuinua maisha ya wasanii kwa kuwaunganisha na mfuko huo ili kuhakikisha maisha ya wasanii yanaboreshwa.
Akizungumza katika kikao kati ya wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara, Katibu Mkuu wa Wizara Wizara hiyo Prof  Elisante Ole Gabriel  amesema kuwa mfuko huo uangalie  namna ya kukusanya wasanii na kuwaweka pamoja ili waweze kujiunga.
“kwa upande wa wasanii wao ni jeshi kubwa tutafute namana ya kuwasajili kama wanachama rasmi wa NSSF ili waweza kutambulika katika ajira rasmi” alisema Prof Gabriel.
Prof Gabriel alisema kuwa  wasanii wanachangamoto nyingi zinazo wakabili ambazo zinarudisha nyuma kada yao moja wapo ikiwa ni hiyo ya kutokuwa wanachama wa mifuko ya Jamii.
Kwa upande wake Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso amesema lengo la mfuko huo ni kudumisha maisha ya watanzania walio katika sekta zote hivyo basi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkoa wanaangalia namna ya kuwainua  wasanii hao kupitia mikopo itolewayo na mfuko huo.
Ameongeza kuwa shirika lake limejipanga kikamilifu kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu ya tano hivyo basi elimu ya kujiunga na mfuko huo itaendelea kutolewa kwa wananchi .
“Wasanii wanaweza kuitangaza nchi yetu vizuri sana  kama tu jamii itaamua kuwatambua na sanaa ikawa ni ajira kamili kama ajira nyingine.”Alisema Bw. Wisso
Aidha aliwasisitiza viongozi wa wasanii pamoja na Maafisa Utamaduni kuwahamasisha wadau wao kuingia katika mfuko huo wa jamii kwani ni dhamana ya maisha yao.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa