Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Meneja  wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso.
Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
Shirika la Taifa la Hifadhi ya 
Jamii( NSSF) Mkoa wa Ruvuma  limeshauriwa kuinua maisha ya wasanii kwa 
kuwaunganisha na mfuko huo ili kuhakikisha maisha ya wasanii 
yanaboreshwa.
Akizungumza katika kikao kati ya 
wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara, Katibu 
Mkuu wa Wizara Wizara hiyo Prof  Elisante Ole Gabriel  amesema kuwa 
mfuko huo uangalie  namna ya kukusanya wasanii na kuwaweka pamoja ili 
waweze kujiunga.
“kwa upande wa wasanii wao ni 
jeshi kubwa tutafute namana ya kuwasajili kama wanachama rasmi wa NSSF 
ili waweza kutambulika katika ajira rasmi” alisema Prof Gabriel.
Prof Gabriel alisema kuwa 
 wasanii wanachangamoto nyingi zinazo wakabili ambazo zinarudisha nyuma 
kada yao moja wapo ikiwa ni hiyo ya kutokuwa wanachama wa mifuko ya 
Jamii.
Kwa upande wake Meneja wa NSSF 
Mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso amesema lengo la mfuko huo ni kudumisha 
maisha ya watanzania walio katika sekta zote hivyo basi kwa kushirikiana
 na Ofisi ya Mkoa wanaangalia namna ya kuwainua  wasanii hao kupitia 
mikopo itolewayo na mfuko huo.
Ameongeza kuwa shirika lake 
limejipanga kikamilifu kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu
 ya tano hivyo basi elimu ya kujiunga na mfuko huo itaendelea kutolewa 
kwa wananchi .
“Wasanii wanaweza kuitangaza nchi
 yetu vizuri sana  kama tu jamii itaamua kuwatambua na sanaa ikawa ni 
ajira kamili kama ajira nyingine.”Alisema Bw. Wisso
Aidha aliwasisitiza viongozi wa 
wasanii pamoja na Maafisa Utamaduni kuwahamasisha wadau wao kuingia 
katika mfuko huo wa jamii kwani ni dhamana ya maisha yao.
0 comments:
Post a Comment