mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu (kulia) akimpokea waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba alipofanya ziara ya kikazi wilaya ya Manyoni jana |
Waziri Nchemba akisalimiana na mbunge Nyalandu (kulia) |
Waziri wa kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali kuingia ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima wa Tumbaku Manyoni |
Mbunge Lazaro Nyalandu kulia akiwa na waziri wa Kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba wakati akisaini kitabu cha wageni ofisi ya mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida |
Waziri Nchemba akiingia ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima wa Tumbaku manyoni |
Wakulima wa Tumbaku wakisalimiana na waziri Nchemba |
Baadhi ya madiwani wakulima wa Tumbaku manyoni wakimpokea waziri Mwigulu Nchemba |
Baadhi ya wakulima wa Tumbaku wakiwa ukumbi wa mkutano kati yao na waziri Nchemba |
Mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu akitambulisha viongozi mbali mbali kabla ya mkutano wa wakulima wa Tumbaku kuanza |
Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akizungumza na wakulima wa Tumbaku wilaya ya manyoni mkoa wa Singida jana |
Wakulima wa Tumbaku wakitoa kero zao kwa waziri Nchemba (hayupo pichani) |
Wabunge wakisikiliza kero za wakulima wa Tumbaku |
waziri wa Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu wakati akieleza kilio cha wakulima wa Tumbaku wilaya ya Manyoni wakati wa mkutano wa waziri Nchemba na wakulima wa Tumbaku uliofanyika ukumbi wa CCM Manyoni jana
WAZIRI wa kilimo
,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu
Nchemba amefuta michango hewa
iliyokuwa ikichangiwa na wakulima wa Tumbaku kwa
UNION kwa kupitia kitengo
cha AMIS huku akiagiza serikali
ya wilaya ya Manyoni kuwachukulia hatua kali aofisa
ushirika mkoa Andru Msafiri na
afisa ushirika Wilaya hiyo Bw Alfred Sekiete iwapo
watabainika kuhusika deni la bilioni 7
ambalo wanadaiwa benki wakulima wa
tumbaku.
Waziri Nchemba
alilazimika kutoa maagizo
hayo baada ya
wakulima wa zao hilo la
Tumbaku kulalamikia utaratibu mbaya wa
baadhi ya viongozi wa UNION na APEX
pamoja na baadhi ya maofisa
ushirika kujinufaisha kupitia mgongo wa
wakulima hao.
Akitoa agizo
hilo jana mjini Manyoni wakati wa
mkutano wa pamoja kati yake na wakulima wa
Tumbaku na viongozi mbali
mbali wa Serikali ya
wilaya ya Manyoni na wabunge
wanaotoka wilaya ya Maeneo yanayolimwa Tumbaku mkoani
Singida.
Waziri Nchemba
alisema kuwa baadhi
ya mambo ambayo serikali ya Rais Dr John Magufuli haipendi
kuona ni pamoja na wakulima kubebeshwa mizigo mikubwa ambayo
kimsingi haiwasaidii kupiga hatua kimaendeleo
zaidi ya kuwatesa .
Alisema
inashangaza kuona wakulima
hao kuendelea kuumizwa na
viongozi wachache ambao wamegeuza
wakulima ni kichaka cha wao
kujificha kujinufaisha kupitia wakulima.
“ Mambo ya ajabu sana
hiki kitu kinaitwa AMIS ni
kuwatoza wakulima michango ya ajabu
ajabu eti wakulima
kutozwa dola 1200 kwa ajili
ya kusafirisha Tumbaku toka Dar
es Salaam kwenda UNION pia wanachangia dola 10 kwa kutunza
kumbukumbu zao ,dola 3 kupakia na kushusha mara mchango kwa ajili ya ADMIN mambo ya ajabu kabisa wakulima
wanahusika vipi na malipo maadmin yani
wanatumia lugha za kijanja kijanja kuwaibia
wakulima ADMIN wa makundi kama yale ya Whatsap kwa wakulima tena…sasa kuanzia leo natangaza kufuta michango hii isiyo na maelezo ya kutosha na
kuagiza kujipanga upya kwa kuwashirikisha wakulima na taarifa hiyo ndani ya siku 7 niipate “
Waziri chemba
alisema kuwa kabla ya kuanza
kuwatoza wakulima hao michango
ni vizuri makubaliano ya michango
hiyo yafanyike upya kwa
kuwashirikisha wakulima na sio
kuendelea kutumia taratibu za
zamani ambazo ni mzigo kwa
mkulima.
Kuhusu maafisa
ushiriki kudaiwa kukopa
benki kupitia mgongo wa wakulima
wa tumbaku na kupelekea
wakulima hao kudaiwa deni benki
la Tsh bilioni 7 aliagiza mkuu wa wilaya ya Manyoni kuagiza wakaguzi na wataalam wake kufanya
uchunguzi na iwapo itabainika kuwa maofisa
hao walihusika na deni hilo
hatua stahiki kuchukuliwa dhidi
Alisema ni kosa
kwa maofisa ushirika kukopa
kwa udhamini wa
wakulima wakati wao si
wazalishaji wa mazao hayo ya
kilimo na kuwa maeneo mengi
wakulima walikuwa wakiwalipia madeni
benki maofisa hao ambao huomba mikopo kupitia vyama vya msingi vya wakulima na wakati mwingine hushirikiana na
benki kutoa mkopo mkubwa ili nao waweze
kugawana .
Pia aliagiza
UNION kufanya kazi ya kuwasaidia
wakulima na sio
kuwakandamiza wakulima na kuwa maeneo
mengi nchini ambayo UNION wapo
kumekuwa na migogoro na kero nyingi kwa
wakulima na kuwa mazao ambayo wakulima hawana UNION kama Mahindi ,
mpunga na alizeti wakulima wanafanya
shughuli zao pasipo migogoro hivyo kuzitaka UNION zinazojihusisha na wakulima wa Tumbaku , Korosho ,pamba na mazao
mengine kujitathimini vinginevyo hazina maana kuwepo.
Aidha waziri Nchemba aliagiza benki ya CRDB kuwalipa pesa zao
zote wakulima wa Tumbaku ambao
wamemaliza madeni yao ya pembejeo na kuendelea
kuwadai wanaodaiwa na si vinginevyo .
Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro
Nyalandu alisema kuwa
kilio kikubwa cha
wakulima wa Tumbaku Manyoni ni uwepo
wa mtu kati katika kilimo hicho
hivyo kuwatesa wakulima hao na kuwa
UNION na APEX bado si ukombozi kwa wakulima wa
zao la Tumbaku kwani alisema wakulima wamekuwa wakilipwa asilimia 50 ya
mauzo ya mazao yao na benki ya CRDB na
asilimia 50 nyingine kushikiliwa na
benki kwa mkopo wa vyama vyao vya msingi hata kama mkulima husika hadaiwi.
0 comments:
Post a Comment