Mkoa wa Singida wazindua mradi wa pikipiki kwa ajili ya kudhibiti uhalifu
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Vicent Kone (mwenye suti nyeusi) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa jeshi polisi mkoa wa Singida muda mfupi kabla ya kuzindua mradi wa pikipiki kwa ajili ya wakaguzi wa tarafa mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Vicent Kone akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa pikipki kwa ajili ya ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida. Kushoto ni Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa na kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida,Mgana Msindai.
Baadhi ya askari wa jeshi la polisi mkoa wa Singida wakishuhudia uzinduzi wa mradi wa pikipiki kwa ajili ya ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Vicent Kone akijaribu kuendesha pikipiki za mradi wa ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singid Mgana Msindai akishuhudia tukio hilo.
Baadhi ya pikipiki 22 za mradi wa ukaguzi wa makosa ya uhalifu katika tarafa za mkoa wa Singida. Pikipiki hizo zimetolewa rasmi kwa ajili ya kukabidhiwa maafisa polisi wa tarafa za mkoa wa Singida.
Basi la Mtei lataifishwa kwa kubeba wahamiaji
WATU 12 raia wa Ethiopia wamehukumiwa na mahakama ya Wilaya ya Singida, kulipa faini ya Sh100,000 kila mmoja baada ya kukiri makosa mawili ya kuingia na kuishi ndani ya ardhi ya Tanzania bila ya kuwa na kibali halali.
Pia mahakama hiyo, imeamuru basi la Kampuni ya Mtei ya mjini Arusha lililokuwa limebeba Waethiopia hao kukamatwa na kutaifishwa kuwa mali ya Serikali.
Waethiopia hao ambao wote bado vijana wadogo na wengine ni wanafunzi wa shule na vyuo, ni pamoja na Ahmed Mohammed Mahamud, Tazana Walao, Mohammed Osman, Abraham Nirato Shango, Adinan Abdalah na Alamu Gabresekesie.
Weingine ni Muhidini Sufiani Ahmed, Tasfai Sutatu Kidisu, Yassin Mohammed Hassan, Afandi Aden Suleiman, Ayele Liranso Gafuche na Pakala Agore Mancha.
Baada ya mwendesha mashtaka mwanasheria wa Serikali Ahmed Seif kuwasomea makosa hayo mawili ya kuingia na kuishi nchini bila ya kuwa na kibali, washtakiwa wote kila mmoja kwa nafasi yake, walikiri kutenda makosa hayo.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Mwanasheria wa Serikali, Seif, aliiomba mahakama hiyo iwape adhabu kali washtakiwa ikiwa ni njia moja wapo ya kukomesha vitendo vya wahamiaji haramu kuingia na kuishi nchini bila ya kuwa na kibali chochote halali.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Kiongozi wa Mahakama ya Wilaya ya Singida, Flora Ndale alisema mahakama yake imezingatia yale yote yaliyoombwa na upande wa mashtaka na utetezi na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya kulipa faini ya Sh100,000 kila mshtakiwa.
Washtakiwa wote 12 walilipa faini hiyo.
Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Serikali Seif, washtakiwa hao walikamatwa Januari 17, mwaka huu alasiri katika eneo la Kijiji cha Kititimo nje kidogo ya Mji wa Singida wakiwa wametokea mkoani Arusha wakidai kwenda Afrika Kusini.
Mwananchi
ZAIDI YA MILLION 31.9 ZAGHARAMIA VIFAA LIGI YA MOHAMMED DEWJI, SINGIDA
Mwenyekiti
wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa
vya michezo kwa kiongozi wa tawi la Mitunduruni.
wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa
vya michezo kwa kiongozi wa tawi la Mitunduruni.
Foleni
ya viongozi wa matawi katika jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa
vya michezo kwa ajili ya timu zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa
kuanza Januari 20 mwaka huu.
ya viongozi wa matawi katika jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa
vya michezo kwa ajili ya timu zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa
kuanza Januari 20 mwaka huu.
Baadhi
ya wa viongozi ngazi za matawi jimbo la Singida mjini,wakimsikiliza kwa
makini mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida, Hamisi Nguli (hayupo
kwenye picha) wakati akitoa nasaha zake muda mfupi kabla ya kukabidhi
vifaa vya michezo.

ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la
Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kwa ajili ya kuendeleza mchezo
wa soka jimboni kwake. Picha zote na Nathaniel Limu
ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la
Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kwa ajili ya kuendeleza mchezo
wa soka jimboni kwake. Picha zote na Nathaniel Limu
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji,ametoa msaada wa vifaa
mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9
vitakavyotumika kwenye ligi ya kombe lake, inayotarajiwa kuanza kutimua
vumbi januari 20 mwaka huu.

Vifaa
hivyo ni pamoja na jezi pea 854,mipira 122,soksi pea 854 na cloves za
magolikipa 61.Vifaa hivyo ni kwa ajili ya timu zitakazoshiriki ligi
ngazi ya kitongoji katika jimbo la Singida mjini.Baada ya ligi
hiyo,itafuatwa na ligi ngazi ya kata ambayo atakuwa na vifaa vyake pia.

Akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,mwenyekiti wa CCM jimbo la
Singida mjini, Hamisi Nguli amepongeza mbunge Dewji kwa kuendelea kutoa
misaada mikubwa mbalimbali katika jimbo lake kwa lengo la kuendeleza
wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.

“Dewji
toka awe mbunge wa jimbo la Singida mjini,siku zote yupo karibu zaidi
na vijana. Amewasaidia mambo mengi makubwa ikiwemo kuwaendeleza
kimichezo na pia ametoa pikipiki kwa ajili ya vijana wa bodaboda
watakaojiunga katika vikundi”,alisema.

Awali
msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi,amesema msaada huyo wa vifaa,ni
mwendelezo wa Dewji kuhakikisha vijana wanatumia michezo kujiendeleza
kimaisha.
Kwa Hisani ya Sufiani Mafoto Blog
msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi,amesema msaada huyo wa vifaa,ni
mwendelezo wa Dewji kuhakikisha vijana wanatumia michezo kujiendeleza
kimaisha.
Kwa Hisani ya Sufiani Mafoto Blog
WEMA SEPETU NA WENZAKE WANOGESHA UZINDUZI WA KAMPENI YA KILIMO KWANZA KWADELO, KONDOA
Diwani Omary Kariati wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, baada ya kuwashili katika kata hiyo jana kuzindua Kampeni ya Kilimokwanza kwa Vijana wa Kata hiyo. Kutokana na juhudi za diwani huyo hivi sasa kata hiyo inayo matrekta 60 yanayotumika kwa kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo ya alizeti na ufuta.
Wasanii wa filamu, kutoka kushoto; Jacob Steven 'J B', Vicent Kigosi 'Ray', Irene Uwoya, Wema Sepetu na Single Mtambalike 'Rick Rich' walipowasili Kwadelo kwa ajili ya kushiri uzinduzi huo wa kampeni ya Kilimo Kwanza kwa vijana wa Kata hiyo.
Wazee wa Kwadelo wakati wakimsubiri kuwasili kwa diwani wao pamoja wasanii hao
Baadhi ya kinamama wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
Ray akipozi picha na wazee wa Kwadelo
Kariati akiwa na wasanii hao kwenye trekta kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo
Wema Sepetu akiungurumisha trekta ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni hiyo. Wapili Kulia ni Omary Kariati
Uwoya naye akilijaribu trekta kwenye uzindzi huo
KWADELO HOYEEEEEE! J B akihamasisha wakati wakiwa kwenye trekta la kilimo wakati wa uzinduzi huo
Treka likionyesha mfano wa ulimaji wa kisasa kwenye shamba la shule ya sekondari ya Kwadelo wakati wa uzinduzi huo
KITUKO: Panzi! Panzi! Panzi!, Wema Sepetu (shati ya kijani) akifunika uso wake kwa kipochi chake, huku akipiga kelele na kujiingiza katika kundi la wazee, kwa sababu ya kuogopa panzi aliyemdandia wakati wa shughuli za uzinduzi huo shambani
J B na Wema wakila mapozi shambani wakati wakienda sehemu ya uzinduzi
Wema akitangaza kuzindua kampeni hiyo
BAADAYE: Wasanii hao wakimkabidhi sh. 500,000 mmoja wa wananchi wa Kwadelo walioathirika na mafuriko. Kwa mujibu wa Diwani Kariati (wapili kushoto), fedha hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Meembe ambaye ni mzee wa heshima wa kata hiyo.
Diwani Kariati akikagua maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika moja ya vijiji vya Kata ya Kwadelo, kufuatia mvua zoinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini
Kariati akionyeshwa maeneo yaliyoathirika
Wazee wakiomba dua ya kheri baada ya shuguli za uzindizi wa Kampeni ya kilimo kwanza na kukagua maeneo ya walioathiriwa na mafuriko: Picha zote na Bashir Nkoromo
Mkuu wa wilaya ya Singida ahimiza watoto kupelekwa kupata chanjo za Rotarix na PCV 13.
Pichani Juu na Chini ni Mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi (katikati) akitoa chanjo ya Rotarix kwa mtoto muda mfupi baada ya kuzindua utoaji wa chanjo hizo.(Picha na Nathaniel Limu).
Baadhi ya watoto wakiwa wanasubiri kupata chanjo mpya za Rotarix inayokinga ugonjwa wa kuharisha na PCV inayokinga ugonjwa wa Nimonia.Uzinduzi wa chanjo hizo ulifanyika katika kituo cha afya cha Sokoine mjini Singida kwa ngazi ya wilaya ya Singida.
Na Nathaniel Limu
Serikali wilayani Singida imewahimiza viongozi na watendaji wote serikalini, vyama vya siasa, dini, taasisi na wadau wote, kushiriki kikamilifu kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi kuhusu chanjo mbili mpya za Rotarix na PCV 13.
Chanjo ya Rotarix, inakinga ugonjwa wa kuharisha na PCV 13 inakinga ugonjwa wa nimonia kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo Mwalimu Queen Mlozi wakati akizindua chanjo hizo mpya kwenye kituo cha afya cha Sokoine mjini Singida.
Amesema utafiti uliofanywa juu ya vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, imebainika magonjwa ya kuharisha na nimonia yana mchango mkubwa katika vifo hivyo.
Mlozi amesema kutokana na utafiti huo, serikali imeamua kuanzisha chanjo hizo mpya ili kudhibiti vifo hivyo vinavyotokana na kuharisha na nimonia.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘mtoto asiyechanjwa ni hatari kwake mwenyewe na wengine, mpeleke akapate chanjo’.
Mamia wakwama, wawili wafariki Singida Kutokana na Mvua Kubwa Zinazoedelea Kunyesha
Wananchi wakivuka kwa miguu katika Daraja la Manung’una, lililopo katika
Kijiji cha Msisi, Singida ambalo limekatika kutokana na mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha. Picha Gasper Andrew
--
MVUA zinazoendelea kunyesha mkoani Singida, zimesababisha maafa
makubwa baada ya watu wawili, mmoja akiwa raia ya China, kufariki dunia
kwa kusombwa na maji,huku mamia ya abiria wakikwama njiani baada ya
daraja linalounganisha mkoa huo na mingine kukatika.Kukatika kwa Daraja la Munung’una kwa siku mbili
sasa,kumesababisha msongamano mkubwa wa magari yanayokadiriwa kuwa
zaidi ya 300.

Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa
waliofariki dunia kutokana na mvua hizo ni Xue Hui (36),maarufu kwa
jina la Kevin na Mariamu Samweli(18), mkazi wa Kijiji cha Maluga ambao
walifariki dunia kwa nyakati tofauti baada ya kusombwa na maji.

Vifo vyao vimeongeza idadi ya watu waliofariki
dunia kutokana na mvua mkoani Singida kufikia sita katika siku tatu
zilizopita. Mvua za juzi, zilisababisha watu wanne wa familia moja
katika Wilaya ya Mkalama kupoteza maisha baada ya kuangukiwa na nyumba
ya tembe.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Ole Lenga alisema raia
huyo wa China, alifariki dunia juzi jioni katika Kijiji cha Gumanga
Wilaya ya Mkalama baada ya gari alilokuwa anasafiria kusombwa na maji...
“Mchina huo alikuwa na mtoto wake ambaye alinusurika kifo.”
Alisema
Mariamu alifariki dunia baada ya kusombwa na maji katika Mto Kiula
uliopo katika Kijiji cha Igonia. “Miili ya marehemu hao imehifadhiwa
kwenye chumba cha maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Singida.”
Abiria wakwama
Mvua hizo kubwa
zilizonyesha tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana, zilisababisha
daraja hilo la Munung’una lililopo katika Kijiji cha Msisi wilayani
Singida kuvunjika.
Mvua hizo kubwa
zilizonyesha tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana, zilisababisha
daraja hilo la Munung’una lililopo katika Kijiji cha Msisi wilayani
Singida kuvunjika.
Kutokana na athari hiyo, kumekuwa na msongamano
mkubwa wa magari baada ya mawasiliano kati ya Singida na mikoa ya kanda
ya ziwa na nchi jirani kukatika.
Baadhi ya wananchi walilalamikia uharibifu huo
wakisema umetokana na ujenzi wa daraja hilo kuwa wa kiwango cha chini.
Dereva, George Medadi akitokea Mwanza kwenda Dar es Salaam, alisema
daraja hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kujengwa chini ya kiwango.