Home » » ZAIDI YA MILLION 31.9 ZAGHARAMIA VIFAA LIGI YA MOHAMMED DEWJI, SINGIDA

ZAIDI YA MILLION 31.9 ZAGHARAMIA VIFAA LIGI YA MOHAMMED DEWJI, SINGIDA


Mwenyekiti
wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa
vya michezo kwa kiongozi wa tawi la Mitunduruni.

Foleni
ya viongozi wa matawi katika jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa
vya michezo kwa ajili ya timu zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa
kuanza Januari 20 mwaka huu.
Baadhi
ya wa viongozi ngazi za matawi jimbo la Singida mjini,wakimsikiliza kwa
makini mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida, Hamisi Nguli (hayupo
kwenye picha) wakati akitoa nasaha zake muda mfupi kabla ya kukabidhi
vifaa vya michezo.
Baadhi
ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la
Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kwa ajili ya kuendeleza mchezo
wa soka jimboni kwake. Picha zote na Nathaniel Limu

Mbunge
wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji,ametoa msaada wa vifaa
mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9
vitakavyotumika kwenye ligi ya kombe lake, inayotarajiwa kuanza kutimua
vumbi januari 20 mwaka huu.

Vifaa
hivyo ni pamoja na jezi pea 854,mipira 122,soksi pea 854 na cloves za
magolikipa 61.Vifaa hivyo ni kwa ajili ya timu zitakazoshiriki ligi
ngazi ya kitongoji katika jimbo la Singida mjini.Baada ya ligi
hiyo,itafuatwa na ligi ngazi ya kata ambayo atakuwa na vifaa vyake pia.

Akizungumza
kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,mwenyekiti wa CCM jimbo la
Singida mjini, Hamisi Nguli amepongeza mbunge Dewji kwa kuendelea kutoa
misaada mikubwa mbalimbali katika jimbo lake kwa lengo la kuendeleza
wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.

“Dewji
toka awe mbunge wa jimbo la Singida mjini,siku zote yupo karibu zaidi
na vijana. Amewasaidia mambo mengi makubwa ikiwemo kuwaendeleza
kimichezo na pia ametoa pikipiki kwa ajili ya vijana wa bodaboda
watakaojiunga katika vikundi”,alisema.

Awali
msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi,amesema msaada huyo wa vifaa,ni
mwendelezo wa Dewji kuhakikisha vijana wanatumia michezo kujiendeleza
kimaisha.

Kwa Hisani ya Sufiani Mafoto Blog

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa