DSC02141
Waziri wa afya na ustawi wa jamii,Dk.Seif Rashidi akifungua kongamano la tisa la baadhi ya waandishi wa habari lililoandaliwa na kufadhiliwa na mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Dodoma hotel mjini Dodoma.Dk.Rashidi aliwataka wanahabari kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kujiunga na mifuko ya afya,ili waweze kuwa na uhakika wakati wote hata kama hawana fedha.
Na Nathaniel Limu, Dodoma
HALMASHAURI ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imekusanya zaidi ya shilingi 1.2 bilioni kutoka michango ya wanachama wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) na vyanzo vingine vya huduma ya afya, kati ya mwaka 1996 na sasa.
Fedha hizo zimejumuisha pia mapato ya tele kwa tele ambazo ni zaidi ya shilingi 490 milioni,mapato ya papo kwa papo shilingi 160 milioni na CHF,shilingi 598 milioni.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Igunga,Elibariki Kingu,wakati akitoa taarifa ya mfuko wa afya ya jamii wilayani kwake kwenye kongamano la tisa la baadhi ya wanahabari kutoka mkoa yote nchini lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Dodoma hotel mjini hapa
Alisema baadhi ya fedha hizo,zimetumika katika ujamilishaji wa ujenzi wa majengo ya zahanati mpya saba zilizogharimuzaidi ya shilingi 35 milioni.
Aidha, Kingu alisema fedha hizo zimegharamia kazi ya kufunga umeme katika vituo viwili vya afya na zahanati tano,ununuzi wa gari Land Cruiser Hard Top na malipo ya motisha (asilimia tano) kwa wakusanyaji wa fedha za mfuko wa afya ya jamii.
DSC02153
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida,Yahaya Nawanda, akitoa taarifa yake ya maendeleo ya  mfuko wa afya ya jamii (CHF) katika wilaya yake. Amedai kuwa wanatarajia asilimia 85 za kaya wilayani humo,hadi mapema mwakani,zitakuwa zimejiunga na CHF.
“Tumenunua dawa za nyongeza kwa ajili ya zahanati na vituo vya afya.Pia tumenunua vifaa tiba vya maabara ikiwemo mashine ya U-tra soend na shilingi milioni sita,zimetumika kwa ajili ya zahanati 44 kufungulia akaunti za vituo”,alifafanua zaidi Kingu kwa kujiamini.
Kuhusu wananchama wa CHF,Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa juni mwaka jana wilaya hiyo ilikuwa na wananchama 3,920 na mapema mwezi huu,wanachana hao wameongezeka na walifikia 15,200.
Katika hatua nyingine, DChuyo alisema pamoja na mafanikio hayo makubwa,mwaka 2012,wilaya hiyo ya Igunga iliteuliwa kuendelea kuwa ya mfano ki-taifa,na ikamwezesha mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwenda ziara ya mafunzo nchini Japan.
DSC02161
Mkuu wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, akitoa taarifa yake ya maendeleo ya  mfuko wa afya ya jamii (CHF) katika wilaya yake.
Hata hivyo,alisema CHF inakabiliwa na changamoto mbalimbali na kubwa zaidi ikiwa ni baadhi ya wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta matibabu,jambo ni hatari hasa kwa aina mama wajawazito
Kwa mujibu wa Dc,Kingu,ili kuwa mwanachama wa CHF katika wilaya hiyo,kila kaya yenye mume,mke na watoto wanne walio chini ya umri wa miaka 18,kulipa ada ya shilingi 10,000 tu na kujihakikishia matibabu stahiki mwaka mzima bila kuongeza fedha zaidi.
DSC02171
Mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC), Abubakar Karasan,akizungumza kwenye kongamano la tisa la wanahabari lililoandaliwa na mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Dodoma hotel mjini hapa.
DSC02132
Baadhi ya viongozi na wanahabari waliohudhuria kongamoano la tisa la baadhi ya wanahabari lililofanyika kwenye ukumbi wa Dodoma hotel mjini hapa.Lengo la kongamano hilo,ni kuwajengea uwezo zaidi wanahabari,ili waweze kuhabarisha na kuhamasisha jamii kujiunga na mifuko ya afya.(Picha zote na  Nathaniel Limu).
DSC02144