Meneja
wa shirika la SEMA, Ivo Manyanku, akizungumza kwenye uzinduzi wa siku
ya kunawa mikono duniani, siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa
mazingira nchini uliofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba.
Kulia mwenye miwani ni mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda.
Na Nathaniel Limu, Iramba
SHIRIKA
lisilo la kiserikali la Sustainable Environment Management Action
(SEMA),linatarajia kutumia zaidi ya shilingi 396 milioni kugharamia
utekelezaji wa mradi wa usafi mashuleni na mazingira kwa ujumla,katika
shule saba ba kata saba za wilaya ya Iramba.
Fedha hizo ni ufadhili kutoka shirika la WaterAid Tanzania.
Hayo
yamesemwa na meneja wa SEMA,Ivo Manyanku, wakati akizungumza kwenye
uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani,siku ya choo duniani na wiki
ya usafi wa mazingirav nchini, iliyofanyika katika kijiji cha Tulya
wilayani Iramba.
Alitaja
baadhi ya malengo ya mradi huo, kuwa ni pamoja na kuhamasisha na
kuelimisha wanafunzi na jamii kwa jumla namna bora ya kunawa mikono.
Mkuu
wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda, akizungumza kwenye
hafla ya uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo dunia
na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika kimkoa katika kijiji
cha Tulya wilayani humo.
“Pia
kuwaelimisha wanafunzi wa kike waliopevuka (kuvunja ungo) njia bora
zitakazowasaidia kuwa wasafi kipindi chote cha siku zao za
hedhi”,alifafanua Ivo na kuongeza kwa kusema;
“Shughuli
zingine ni ujenzi wa vyoo bora na kuwahamasisha wanafunzi na jamii kwa
ujumla kuvitumia kikamilifu.Tutawaelimisha na kuwaahamasisha kunawa
mikono pindi wanapotoka chooni kujisaidia”.
Kwa
upnde wake afisa afya wa wilaya ya Iramba,Yohana Dondi,alisema kuwa
wilaya ya Iramba ina kaya zenye vyoo bora ni aslimia 42,vyoo kubalika
52,vyoo visivyokubalika asilimia 18 na bila vyoo,ni aslimia sita.
Kwa
mujibu wa afisa huyo,nchi zinazoendelea,asilimia 70-80 ya maradhi
yote,yanasababishwa na maambukizi yatokanayo na vinyesi,hivyo kuwa ni
kisababishi namba moja cha vifo.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu,ni Choo bora na mikono safi kwa afya bora,heshima na usawa”.
Spider
man kutoka Temeke jijini Dar-es-salaam akitoa burudani ya kutembea juu
ya waya kwenye hafla ya uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku
ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini iliyofanyika katika
kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba.
Mkuu
wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda (wa nne kutoka
kushoto) akitoa maelekezo juu ya ujenzi wa choo bora cha shule ya msingi
Tulya.Wa tatu kushoto ni meneja wa shirika la SEMA,Ivo Manyanku.
Baadhi
ya wakazi wa kata ya Tulya,waliohudhuria uzinduzi wa siku ya kunawa
mikono duniani,siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini
uliofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba.(Picha zote na
Nathaniel Limu).
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment