Waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu amemteua Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Paseko Kone kuwa Mwenyekiti wa Kikosi kazi kitachofuatilia uundwaji wa chama cha wafuga nyuki hapa nchini.
Nyalandu alimteua Mkuu wa Mkoa huo kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wafugaji wa nyuki katika mkoa wake wa Singida bila kuchoka.
Waziri Nyalandu alitoa uamuzi huo wakati akifuga kongamano la ufugaji nyuki la Afrika lililomalizika Jijini Arusha jana.
Wajumbe Wengine walioteuliwa katika kikosi kazi hicho ni Juma Shaban Mgoo ambaye atakuwa katibu wa Kikosi kazi hicho na pia ni Mtendaji Mkuu,wakala wa Huduma za Misitu Tanzania na ambaye alikuwa mkamu mwenyekiti wa Kongamano atakuwa mjumbe katika Kikosi kazi hicho,wengine ni Ester Mkwizu Mjumbe.
Wajumbe wengine ni mwakilishi wa wafugaji nyuki ,mwakilishi wa wasomi na watafiti ili kikosi kazi kiwe na mchanganyiko wa pande zote.
Walioteuliwa wote watapaa barua jumatatu kwa ajili ya kuthibitisha uteuzi wao,ambapo waziri nyalandu alieleza kuwa kuwa uteuzi huo wa wajumbe wanaounda kikosi kazi cha kushughulikia uundwaji wa chama cha wafuga nyuki ni agizo lililotolewa na Waziri Mkuu wakati wa ufuguzi wa Kongamano la nyuki kuwa ipo haja ya kuundwa kwa chama cha wafugaji nyuki ili kiweze kuwaunganisha wafugaji wote ndani ya nchi na kuwa na mtandao mmoja wenye nguvu na sauti.
Katika hotuba yake alieleza jinsi Tanzania ilivyojithatitia kuhakikisha inainua ufugaji nyuki na sekta ya nyuki ili kuwapita nchi ya Ethiopia ambayo ndiyo kinara cha nyuki cha Ufugaji nyuki Afrika.
Akasema kongamano hili ni la kwanza kufanyika katika ardhi ya Tanzania na limesaidia sana katikakuwafumbua macho watanzania hasa wafugaji nyuki hasa katika masuala muhimu yaliyosisitizwa katika mada zilizojadiliwa kwenye kongamano hilo yatasaidia kukuza sekta ya ufungaji nyuki hapa nchini.
Kongamano hilo lililojumuisha washiriki wapatao 550 kutoka katika mataifa ya Ghana,Ethiopia,Zimbabwe, Afrika kusini,Camerun,Sudani,Kenya,Uganda na Rwanda.
Washiriki wengine walitoka katika nchi ya Kanada,Marekani,Pakstan,Namibia,Misri, Zambia,Ubelgiji,Uturuki na mengine.limekuwa la kufana sana,mada 88 zilikuwepo,mada 45 zilijadiliwa,katiyake mada 26 zilihusu tafiti za nyuki,mada 17 zilijadiliwa kwa wafugaji nyuki.
Awali akimkaribisha waziri Nyalandu Mwenyekiti wa Kongamano hilo SelestinKisimba alieleza kuwa katika kongamano hilo wameondoka na mapendekezo sita mambyo wataenda kuyafanyia kazi mara moja ili kuinua sekta ya nyuki.
Baadhi ya Mapendekzo hayo ni kuwa ufugaji nyuki lazima uweb endevu kwa manufa ya wafugaji wote,,umuhimu wa ufugaji nyuki na maendeleo,tatizo la ukosefu wa mitaji,uendelezaji wa rasilimali zilizopo , kuongeza uzalishaji wa thamani ya asali,ambapo mapendekezo hayo yatasaidia kuboresha ufugaji nyuki.
Washiriki wamepata nafasi ya kutembelea maeneo ya ufugaji nyuki katika mikoa ya Singida,Dodoma na Ngorogoro Mkoani Arusha kuweza kujifunza na kuona hali halisi ya mazingira yalivyo hasa katika maeneo yanayofugwa nyuki.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment