Wananchi
wa kijiji cha Puma katika wilaya ya ikungi mkoani Singida wame mkataa
mwenyekiti wa kijiji hicho katika mkutano wake wa kwanza na kusababisha
diwani wa kata hiyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi kuingilia kati
na kufunga mkutano kabla ya wakati ili kumnusuru asipigwe na wananchi.
Wananchi hao waliokuwa na hasira wamesema hakuna sababu ya kuwa na
mwenyekiti ambaye wananchi hawamkubali kwa sababu katika uchaguzi
uliopita kulikuwa na udanganyifu katika upigaji kura,kutokana na hali
hiyo wamesema ni bora kuachana na vyama vya siasa wachague mwenye kiti
wa kimila ili kukisaidia kijiji cha puma kupata maendeleo.
Baada ya vurugu kuongezeka diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya
CCM,Bwana ramadhani kulungu ilibidi kufunga kikao hicho ili kuweza
kumnusuru mwenyekiti wa kijiji cha puma na kuwatuliza wananchi
ilikusitokee uvunjifu wa amani.
Mwenyekiti wa kijiji cha puma kwa tiketi ya CCM ,Bwana Sifa Joramu
awali ambaye alishindwa kabisa kuendesha kikao chake ,baada ya jeshi la
polisi kuingilia kati na kuamua kumsindikiza kwa ulinzi mkali huku
wananchi waki mzomea na kusema hawamtaki,amesema hizo ni fujo za vyama
vya upinzani lakini yeye atahakikisha kazi anafanya kwa sababu yeye
ndiye aliyeshinda na kuapishwa kwa kazi ya uwenyekiti wa kijiji cha
puma.
Kundi la watu waliamua kumfuata na kumbeba juu kisha kumzungusha
mitaani Bwana Hassan Chaimbo aliye gombea kwa tiketi ya CHADEMA na
kushindwa kwa kupata kura mianne arobaini na nne dhidi ya Bwana Sifa
Joramu alishinda uwenyekiti wa kijiji cha puma kwa tiketi ya CCM katika
uchaguzi uliofanyika mwishoni mwaka jana na kupata kura mianne hamsini
na saba.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KUELEKEA UCHAGUZI 2015: JE UNAPENDA NANI AWE KIONGOZI WAKO? JAZA FOMU HII FUPI HAPA
0 comments:
Post a Comment