Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, akitoa maamuzi mara baada ya
kuhojiana na TRA, alisema uingizwaji holela wa sukari una hatari kwa
ukuaji wa viwanda vya ndani.
“Tunataka taarifa ili tuweze kuwa na mikakati endelevu ya kuzuia
sukari ya magendo, unasababaisha sukari inayozalishwa na viwanda vyetu
na miwa ya wakulima ina kosa soko,” alibainisha.
Hivi karibuni, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene,
alipotembelea kiwanda cha sukari cha TPC mkoani Kilimanjaro, alielezwa
jinsi sukari ya nje iliyojaa sokoni na wao kukosa pa kuiuza.
Alisema watakutana na Wizara zinazohusika kujadili na kuanza
operesheni maalum kwenye maduka mbalimbali na kukamatwa sukari ya nje na
ya viwandani inayouzwa kwa wananchi kwa bei ndogo.
CHANZO:
NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment