Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na, Jumbe Ismailly, Manyoni        
CHAMA
 Cha ACT Wazalendo wilaya ya Manyoni Mkoani Singida kimezindua kampeni 
za ubunge wa jimbo la Manyoni mashariki kwa kumnadi mgombea ubunge wa 
jimbo hilo,Muttee John Henry na kuwatisha watendaji wa idara ya afya 
wanaouza madawa kwenye vituo vya kutolea huduma na hivyo kusababisha 
wananchi kukosa huduma katika vituo vya kutolea huduma hizo.
Akiwahutubia
 wananchi wa mji wa Manyoni na vitongoji vyake,mgombea ubunge wa jimbo 
la Manyoni mashariki kupitia tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo,Henry 
amesema vituo vingi vya kutolea huduma za afya vimekuwa vikikabiliwa na 
uhaba mkubwa wa madawa jambo linalowafanya wagonjwa wanaofuta huduma 
kutakiwa kwenda kununua dawa kwenye maduka ya madawa yaliyopo karibu na 
vituo hivyo.
Hata
 hivyo mgombea huyo alifafanua kwamba kutokana na kuwepo kwa tatizo 
kubwa la upatikanaji wa dawa,ni asilimia sita tu ya watanzania ndiyo 
wanaonufaika na mfuko wa afya ya jamii (CHF),hali inayoonyesha bado kuna
 idadi kubwa ya watanzania wanaopoteza maisha kwa kukosa huduma hizo za 
afya kwenye maeneo ya vijijini.
‘Ndugu
 zangu nchi hii asilimia sita tu ya wananchi wa Tanzania ndiyo 
wanaonufaika na mfuko wa afya ya jamii na asilimia 98 ya 
wakulima,wafugaji,bodaboda,mama lishe na wafanyakazi katika sekta 
isiyokuwa rasmi hawanufaiki na mfuko wa afya ya jamii(CHF)’’alifafanua 
Henry.
Kwa
 mujibu wa Henry,licha ya wananchi hao kupigania kuongeza uchumi kwa 
nguvu zote kwa kipindi cha miaka 35,wanapofikia umri wa miaka 60 huwa 
wamechoka na hivyo kujikuta wakisahaulika katika taifa lao 
walilolitumikia kwa kipindi kirefu katika maisha yao.
Aidha
 alisisitiza kwamba taifa linalowasahau wananchi waliolitumikia kwa 
miaka mingi ikilinganishwa na watumishi wa serikali ambao wanapostaafu 
hulipwa mafao yao ya kustaafu,hilo siyo taifa jema ambalo baba wa taifa 
alikuwa akijivunia.
Alisisitiza
 mgombea huyo kijana kwamba ni wakati muafaka sasa wa kuweka utaratibu 
wa kuwasaidia watanzania wanyonge  hao pale wanapochoka.
 Ili
 kukabiliana na hali hiyo ya ukosefu wa madawa kwenye vituo vya kutolea 
huduma,Henry alisema chama cha ACT Wazalendo kimetafakari sana na kuja 
na mpango mpya wa kuanzisha mfuko utakaowasaidia watanzania wanyonge.
“Najua
 fedha zetu tunazokusanya ni chache sana lakini mfuko wa wanyonge ambao 
utaweza kuhifadhi fedha kidogo kidogo ndiyo kimbilio la wanyonge 
wanaopata majanga ya kuugua basi wanapona kwa mfuko wa afya ya 
jamii”alifafanua.
Naye
 katibu wa Mkoa wa Chama Cha ACT Wazalendo,Lipu Loti Robert alisema 
idadi kubwa ya watendaji wamebainika kulihofia azimio la Arusha 
lililoachwa na baba wa taifa marehemu,Mwalimu Julius Nyerere na ndiyo 
maana waliamua kulivunja kwenye moja ya vikao vilivyofanyika Zanzibar.
Hata
 hivyo Roberti aliweka wazi kuwa ACT baada ya kubaini kutokuwepo kwa 
azimio la Arusha ndipo walipozindua azimio la Tabora ambalo lina mambo 
manne,ambayo ni pamoja na Hifadhi ya jamii,suala la uchumi 
shirikishi,sekta ya afya na sekta ya elimu.  
Mmoja wa wakereketwa wa chama hicho akipeperusha bendera kwenye mkutano wa uzinduzi
baadhi
 ya viongozi wa ACT waliohudhuria mkutano wa uzinduzi kumnadi mgombea 
ubunge wa jimbo la Manyoni mashariki.Picha zote na Jumbe ismailly
NA MO BLOG 
0 comments:
Post a Comment