Naibu
 waziri wa fedha na mgombe ubunge jimbo la Mkalama mkoa wa Singida, 
Mwigulu Nchemba (mwenye skafu), akiingia kwenye uwanja wa michezo wa 
kijiji cha Iguguno,kuhudhuria uzinduzi wa kampeni za ubunge na udiwani 
CCM zilizofanyika jana.Wa pili kushoto mrefu aliyenyanyua mkoano juu,ni 
mgombea ubunge jimbo la Mkalama, Alan Joseph Kiula. 
Mwigulu pamoja na mambo mengine,amewataka wakazi wa mkoa wa Singida,kuichagua CCM kwa madai ndicho chama pekee chenye uwezo wa kuwatumikia wananchi.
Naibu
 Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba, amewataka Viongozi/ watu wanaojifanya
 mabingwa wa kutumia baadhi ya hotuba za hayati Mwalimu Julius Nyerere 
kujinufaisha kisiasa, watumie pia hotuba za hayati Nyerere zenye 
mwelekeo wa kuwakosoa,ili waweze kuthibitisha ubingwa wao.
Amedai mabingwa hao wakiweza 
kutoa ufafanuzi hata kwa hotuba zinazowakwaza,kwa njia hiyo, watakuwa 
wanawajengea wananchi mazingira mazuri ya kutoa maamuzi stahiki Oktoba 
25 mwaka huu wakati wa kuchagua viongozi wanaowataka.
Mwigulu ambaye anatetea 
nafasi yake ya ubunge jimbo la Iramba kwa awamu ya pili mfululizo, 
ametoa wito huo juzi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za ubunge na 
udiwani, jimbo la Mkalama mkoani Singida.
Akifafanua,alisema hivi 
karibuni baadhi ya wagombea mbalimbali wakiwemo wa nafasi ya urais, 
wamekuwa wakitumia baadhi ya hotuba za hayati baba wa Taifa, wakilenga 
kuwaaminisha wananchi kuwa wawachague kwa madai watafuata nyayo za 
hayati baba wa faifa, na kwamba wanauchungu na wananchi.
“Wengi wa viongozi hawa 
wanajaribu kuwahadaa wananchi kwa kitendo chao cha kuhama CCM 
kimezingatia maneno yaliyowahi kutolewa na hayati baba wa taifa kuwa, 
mabadiliko usipoyapata ndani ya CCM, unaweza kuyapata nje ya 
CCM”,alisema.
Akifafanua alisema mabadiliko
 ya kweli yaliyokuwa akiyazungumzia hayati Nyerere, sio ya kuhama vyama,
 ni mabadiliko ya kiutendaji ambayo yatafanyika  ndani ya CCM na si kwa 
kukimbilia upinzani.
Mwigulu alisema kuwa 
itapendeza zaidi endapo mabingwa hawa watazungumzia pia maneno 
yaliyotolewa na hayati rais wa kwanza,Nyerere,kwamba ‘anayekimbilia 
kwenda ikulu kwa kutumia fedha,fedha hizo atazirejeshaje’.
“Kama wao ni mabingwa,basi 
wazungumzie maneno ya hayati Julius Nyerere ya ‘ikulu kuna nini pale 
hadi mtu apakimbilie,mtu aote rushwa hadi kwenye vyuo mbalimbali,hizo 
pesa amezitoa wapi na kama amekopa,atazirejeshaje. Wakizungumzia 
maneno hayo ambayo yapo kwenye hotuba ya hayati baba wa taifa na kutupa 
majibu ya kuridhisha,pengine kidogo tunaweza tukawaelewa”,alifafanua 
zaidi.
Katika hatua nyingine,Mwigulu
 alisema wana CCM waliokihama Chama cha Mapinduzi baada ya kushindwa 
kwenye kura za maoni, huko walikokimbilia kutimiza azma yao au tamaa 
zao  za kutaka uongozi, wasipopata wanachokihitaji, baada ya Oktoba 25 
mwaka huu, watarejea CCM.
“Wewe fikiria mtu kama 
Lowassa amelelewa na CCM takribani  miaka 40 sasa, kichwa chake chote 
hakina kitu kingine kimejaa CCM. Mambo ambayo atataka kuyaanzisha kwenye
 Ukawa yatakuwa na harufu kubwa ya CCM tu. Kwa hiyo, huko walikokimbilia
 kusaka uongozi njia yo yote ikiwemo ya matumizi ya makubwa ya rushwa, 
wamekwenda kuanzisha CCM (B) hakuna cha ziada”,alisema.
Akisisitiza, alisema upinzani
 kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu haupo kabisa, ni kilichopo ni CCM (A)na 
CCM (B ndizo zitakazochuana  kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Aidha, Mwigulu ambaye hotuba 
yake ilikuwa ikikatishwakatishwa kwa kushangiliwa, amewataka wakazi wa 
mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla, wasikubali hadaa inayotolewa na 
mgombea urais kupitia Ukawa, eti akichaguliwa serikali yake ataiendesha 
kwa kasi ya aina yake ambayo haijawahi kutokea nchini.
Mwigulu amesema mgombea huyo, yeye mwenyewe hana kasi aina hiyo anayoisema.
“Ongea ya mgombea huyo, ninyi
 ni mashahidi, anaongea kwa kasi inayofanana na mwendo wa kinyonga, 
hotuba zake hazizidi dakika tano, kunyanyuka kwake kutoka kwenye kiti, 
ni kwa kasi ya kinyonga vile vile,hapo alipo hana kabisa  kumbukumbu ya 
kitu cho chote kichwani mwake,na mbaya zaidi hawezi kusafiri kwenye 
barabara za vumbi kiuno kitamletea matatizo makubwa”,alisema.
Alisema chaguo la Watanzania 
kwa nafasi ya urais wa awamu ya tano, ni DK. John Pombe Magufuli, ambaye
 ni mtu asiyekuwa na makandokando, mwadilifu na mchapakazi wa kupigiwa 
mfano.
Mwigulu,alisema anayoimani 
kubwa kwamba Watanzania wote watampa DK. Magufuli kura ya ndio na 
watachagua wabunge na madiwani wote kutoka CCM A na si vinginevyo
0 comments:
Post a Comment