Tigo yafungua duka jipya mkoani Singida

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini, Saidi Amanzi(katikati) akikata utepe kuzindua duka jipya la Tigo mkoani Singida jana, Wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, George Lugata na Meneja huduma kwa wateja Tigo, Halima Kasoro.
Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini, Saidi Amanzi(kulia) akiangalia bidhaa mbalimbali mara baada ya kuzindua duka jipya la Tigo mkoani Singida jana. Wanaoshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, George Lugata na kushoto ni Meneja huduma kwa wateja Tigo, Halima Kasoro.

Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini, Saidi Amanzi(katikati) akiongea na mmoja wa wafanyakazi wa Tigo mara baada ya   kuzindua duka jipya la Tigo mkoani Singida jana, 
 Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, George Lugata akimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini, Saidi Amanzi mara baada  kuzindua duka jipya la Tigo mkoani Singida jana, 

Mkuu wa Wilaya ya Singida mjini, Saidi Amanzi(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa  Tigo mkoani Singinda  mara baada ya kuzindua duka jipya la Tigo mkoani Singida jana, 


Kampuni ya simu ya Tigo imefungua duka jipya Singida ambalo limepunguza adha kwa wateja wa kampuni hii ambao walikuwa wanatafuta huduma kwa wateja umbali mrefu toka kwa makazi yao  
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo Mkurungezi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Bw.George Lugata alisema uzinduzi wa duka hili ni moja ya mipango ya kampuni ya Tigo kusogeza huduma karibu na wateja wake.
"Kampuni ya tigo imeangalia fursa zilizopo katika eneo la Singida ambapo kwa pamoja tumeiona ni jinsi gani tunaweza kusaidiana na wakulima na wafanya biashara kuweza kufanya huduma mabalimbali za kibenki kwa kutumia simu za mkononi"Alisema Lugata. 
Lugata alisema kuwa duka hilo linategemea kuhudumia wateja wapatao mia tatu kwa siku wakipata huduma mbalimbali ikiwemo huduma za kuunganishwa kwenye intaneti, usajili wa laini za simu na kurudisha laini zilizopotea pia kununua simu za kisasa.
Kwa upande wa katibu wa mkuu wa wilaya ya Singida mjini Mhe.Saidi Amani alipongeza hatua za Tigo za ufunguzi wa duka hili kwa kuwa utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wa wilaya ya Singida.
Tigo Tanzania ina jumla ya maduka (46) nchini, na duka hili linamaanisha kwamba tunaongeza ubora wa huduma zetu katika maeneo zaidi. Wateja wetu watakao tembelea duka hili wataweza kufurahia na huduma zetu mbali mbali matumizi ya smartphones, modemu za intaneti, Tigo Pesa, Muziki wa Tigo na Facebook ya bure inayotolewa na kampuni.


WALIMU 447 WILAYANI MANYONI YADAIWA HAWAJAPANDISHWA MADARAJA KWA MUDA MREFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Ni Katibu wa TSD Mkoa wa Singida,Bwana Samweli Ole Saitabau(aliyesimama) akitoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa haki za walimu wa wilaya ya Manyoni ambao bado haapandishwa madaraja yao.

Ni Baadhi ya wanachama wa CWT Wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Katibu Muu wa CWT,Bwana Ezekiah Oluoch  .
WALIMU 447 wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida hawajapandishwa madaraja yao mbalimbali kutoka mwaka 2014/2015 mpaka sasa hali ambayo imepunguza ari ya utendaji wao wa kazi za kila siku.
Katibu wa Chama Cha Walimu (CWT) Wilaya ya Manyoni, Nelea Nyang’uye aliyasema hayo kwenye taarifa ya kamati ya utendaji ya chama hicho aliyotoa kwa Naibu katibu mkuu CWT,Ezekiah Oluoch aliyekuwa na ziara ya siku moja wilayani Manyoni iliyolenga kusikiliza kero pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Aidha Nelea alifafanua kwamba kati ya walimu hao,walimu 390 ni walimu wa shule za msingi na kwamba walimu 276 licha ya kuwa na sifa za kupandishwa madaraja lakini mpaka wamefikia hatua ya kugota na bila kupandishwa na walimu 114 wanastahili kupandishwa kwa utaratibu wa kawaida.
Kwa mujibu wa katibu huyo wa CWT,kwa upande wa idara ya elimu sekondari kuna walimu 9 waliogota na walimu 50 wanastahili kupandishwa kwa utaratibu wa kawaida lakini mamlaka zinazohusika zimeshindwa kushughulikia wilayani hapa.
Kuhusu malipo ya fedha za likizo,Nyang’uye aliweka bayana kuwa kwa kipindi cha mwezi disemba,mwaka jana Halmashauri ya wilaya ya Manyoni ilitarajia kupokea shilingi milioni 30 lakini fedha walizopokea ni shilingi milioni 21 na hivyo kuwa na upungufu wa shilingi milioni saba.
Hata hivyo msemaji huyo wa chama alisisitiza kwamba fedha hizo za nauli ya likizo hupelekwa kidogo sana na kibaya zaidi fedha hizo hupelekwa wakati likizo ikiwa imeshaanza au inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea walimu wwenye haki ya kulipwa kuanza kukopa.
“Nauli za likizo kuletwa kidogo mno na zinaletwa wakati likizo ikiwa imeanza au inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea walimu wenye haki ya kulipwa kuanza kukopa,kwa mfano nauli ya mwezi disemba,mwaka jana iliyoletwa kwa idara ya elimu ya msingi ni shilingi 23,000,000/= na idara ya elimu sekondari ni shilingi milioni saba”alisisitiza katibu huyo wa CWT.
Nyang’uye hata hivyo alionyesha masikitiko yake kutokana na Tume ya Utumishi wa Walimu(TSD) wilaya ya Manyoni kushindwa kushughulikia mashauri ya kinidhamu kwa wakati na hivyo kuchukua muda mrefu sana na kutoa mfano wa shauri moja la walimu wawili waliosimamishwa kazi tangu mwaka 2013 mpaka sasa hawajuia hatma yao.
Picha na Michuzi Media

Afungwa jela miaka 120 kwa kumiliki nyara za serikali

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


WASHITAKIWA sita waliokuwa wanakabiliwa na makosa mawili ya kumiliki vipande 53 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 149. 3 na uwindaji haramu kinyume na sheria wamehukumiwa kwenda jela miaka 120 na kulipa faini ya Sh bilioni 1.4 .
Waliokumbwa na adhabu hiyo ni Eliud Selema Mayunga (38) mkazi wa kijiji cha Kiombo, Ramadhani Said maarufu “Biladuka” (47) mkazi wa Itigi, na Leonard Oscar maarufu “Sunzu” (31) mkazi wa Karangari, wilayani Manyoni.
Wengine ni Philemon Michael maarufu “Kanyonga” (31) mkazi wa Kitaraka Itigi, Iddi Waziri au “Issah Ustadh” (30) mkazi wa kijiji cha Kiombo na Jimmy Charles Lyimo (39) mfanyabiashara wa Tabora.
Mwanasheria wa Serikali, Petrida Mutta alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida, Joyce Minde kuwa mnamo Machi 31 mwaka 2014 muda usiojulikana, washitakiwa walikamatwa wakiwa na vipande hivyo nyumbani kwa Iddi Waziri.
Mutta aliiomba Mahakama itoe adhabu kali kutokana na vitendo vya uwindaji na biashara za nyara za serikali kuendelea kushamiri.
“Vitendo hivi haviwezi kufumbiwa macho kwa sababu vikifumbiwa macho, fahari ya nchi hii ya kuwa na wanyama pori itatoweka.”
Washtakiwa ambao wakili wao Josephat Raphael Wawa hakuwepo mahakamani, kila mmoja kwa nafasi yake, aliiomba Mahakama impe adhabu nafuu kutokana na kuwa kosa lao la kwanza.
Akitoa hukumu, Hakimu Minde alisema kuwa upande wa Jamhuri umethibitisha bila kuacha shaka yoyote kwamba washtakiwa wanayo hatia kwa makosa yote mawili. Alisema, kwa kosa la kwanza kila mmoja atatumikia jela miaka 20 na kwa kosa la pili kila mmoja atalipa faini ya Sh milioni 248. 8 tu.
Chanzo Habari leo

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa