KAMPUNI YA BIA YA MABIBO KUPITIA BIA ZAKE ZA WINDHOEK LAGER NA WINDHOEK DRAUGHT YAJITOSA KUINUA UCHUMI WA MKOA KAGERA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr.James Rugemalira akizungumza na wadau mbalimbali wa mjini Bukoba wakati wa Promosheni ya bia za Windhoek Lager na Windhoek Draught katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo zilizofanyika Hoteli ya New Coffee Tree Inn mjini Bukoba leo usiku. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com simu namba 0712-727062)
 Fr.James Rugemalira (katikati), akisisitiza jambo
 kwenye promosheni hiyo. Kutoka kushoto ni Mganga
 Mkuu wa Halmsahauri ya Wilaya ya Bukoba, Hamza
 Mugura, Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya
 inayofanya shughuli zake mjini Bukoba ya KADETFU,
Yusto Muchuruza, Mshauri wa Fr.James, Enic Kashasha
 na Andrew Kailembo.
 Wadau wakiwa kwenye promosheni hiyo.
 Mrembo huyu mnywaji wa Windhoek naye
 alikuwepo kwenye promosheni hiyo.
Mshereheshaji wa Promosheni hiyo, Andrew Kagya,
 akiwajibika.

 Meneja Mauzo wa Kanda ya Ziwa, Godfrey Mwangungulu, akielezea ubora wa Bia za Windhoek.

Mdau wa Windhoek akifuatilia matukio yote kwa karibu.
 Hakika imependeza.

Fr.James Rugemalira (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali.  Kutoka kushoto ni Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali mkoani Bukoba, Sakina Husein Sinda,Mganga Mkuu wa Halmsahauri ya Wilaya ya Bukoba, Hamza Mugura, Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya inayofanya shughuli zake mjini Bukoba ya KADETFU, Yusto Muchuruza, Mshauri wa Fr.James, Enic Kashasha na Andrew Kailembo, Mmiliki wa Walkgard Hoteli, Adventina Matungwa na Dk.Julius Zelothe.


 Wanahabari wakiwa kwenye promosheni hiyo.
 Wadau wakiwa kwenye promosheni hiyo
Promosheni imenogaaaa.
 Wadau wakiwa kwenye promosheni hiyo.
 Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya inayofanya shughuli zake mjini Bukoba ya KADETFU, Yusto Muchuruza,akichangia mada katika promosheni hiyo.
Hapa Windhoe imependezaaa ni tamuuuuuuu
 Wadau wakipata kinywaji cha Windhoek katika promosheni hiyo.


 Meza kuu hiyoooo, wanachangamkia Windhoek.
Ma DJ wakiwajibika katika promosheni hiyooo.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com simu namba 0712-727062).

FR JAMES RUGEMALIRA AHIMIZA UWEKEZAJI MKOANI KAGERA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Katibu Mkuu mstaafu wa Shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi (ICFTU/AFRO), Andrew Kailembo(kulia), akiwa katika mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili maendeleo ya mkoa wa Kagera uliofanyika jana.


 Wakili wa Kujitegemea, wa IMMMA ADVOCATES, Protas Ishengoma akiongoza mkutano huo.




 REV.Fr Kamugisha (kulia), ambaye ni Mkurugenzi wa Hoteli ya Kolping akichangia mada. Kutoka kushoto ni Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr, James Rugemalira na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu, Fabian Masawe.
 Wanahabari wa mkoa wa Kagera wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Utawala wa Jumuia ya Afrika Mashariki, mstaafu, Abdul Katabaro naye alipata fursa ya kuchangia katika mkutano huo muhimu wa kuhimiza uwekezaji mkoani humo.


MSHAURI wa Kimataifa wa kujitegemea (International Independent Consultant) Fr. James Rugemalira, wa Mabibo Breweries, jana aliandaa hafla ya kuzungumzia fursa za maendeleo katika mkoa wa Kagera ndani ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Hafla hiyo ilihudhiriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali  Mstaafu Fabian Massawe, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi. 

Wengine waliohudhuria ni pamoja na wana Kagera wanaoishi na kufanya Kazi nje ya mkoa wa Kagera wakiwemo wakili wa kujitegemea Bw. Protase Ishengoma wa IMMMA Advocates, mfanyabiashara na Mshauri wa Fr. James, Bw. Abdul Katabaro ambaye amestaafu kutoka utumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mzee Andrew Kailembo kutoka Bruxelles, Rev. Fr. David na Kyabukoba, miongoni mwa wengi. 

Hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Kolping, mjini Bukoba, pia ilihudhiriwa na waandishi wa habari kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari.

Fr. James alisisitiza juu ya mkoa kuzitumia fursa nyingi za uchumi zinazotokana na jiografia ya mkoa wa Kagera kupakana na nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki, zikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya kwa maana hiyo kuufanya mkoa huo kuwa ndicho kiunganishi cha nchi zote (hub). 

Kwa sababu hiyo alisisitiza umuhimu wa mkoa wa Kagera kuwa na miradi mikubwa ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa uwanja wa Ki-mataifa Omukajunguti, ujenzi wa Bandari Kavu na maeneo huru ya Uzalishaji (EPZ) eneo la Kitengule na kilimo cha Matunda, mboga na mazao mengine ya chakula. Alisisitiza kuwa soko la mazao lipo katika nchi zinazouzunguka mkoa wa Kagera.

Fr. James aliitumia fursa hiyo kuelezea mipango ya kampuni ya Mabibo Breweries kuwekeza kwenye kiwanda cha kuzalisha bia aina ya Windhoek katika mikoa ya Kagera, Tanga na Kilimanjaro. 

Pia alizungumzia mpango wa kuanzisha taasisi ya ki mataifa ya uchunguzi na tiba kwa maradhi ya Kansa kitakachojulikana kama RUTAKWA BYERA INTERNATIONAL DREAM TANK CANCER CENTER ndani ya Manispaa ya Bukoba.

Naye Mkuu wa Mkoa alimshukuru sana Fr. James kwa moyo wa uzalendo wa kuhamasisha uwekezaji katika mkoa wa Kagera na yeye mwenyewe na Mabibo Breweries kuwa msitari wa mbele kwa vitendo. Kanali Massawe alimuhakikishia kwamba Serikali ya Mkoa itampatia yeye pamoja na wawekezaji wengine watakaojitokeza, ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha uchumi wa mkoa unapanuka na kuongeza ajira kwa vijana.

Kanali Massawe aliwaambia washiriki wa hafla hiyo kuwa alipofika kwenye mkoa wa Kagera miaka saba iliyopita, mkoa ulikuwa unashika nafasi ya tatu kutoka mwisho kati ya mikoa 25 katika uchumi lakini sasa mabadiliko makubwa yamekuwepo mkoa upo kwenye nafasi ya kumi na Sita. 

Aliongeza kusema kwamba kwa fursa zilizopo, endapo zitatumiwa vizuri, basi mkoa unaweza kufanya vizuri zaidi. Kanali Massawe, aliziainisha fursa nyingi zilizopo na ambazo hazijasisimiliwa kuwa ni pamoja na Utalii ambao mkoa unavyo vivutio vingi ikiwa ni pamoja na Ziwa Victoria, mto Kagera, watu na Utamaduni wao, historia, kituo cha hija cha Nyakijoga na Makanisa makubwa yaliyojengwa zaidi ya miaka mia moja iliyopita.

Waalikwa mbalimbali waliopata fursa ya kuongea walimpongeza sana Fr. James kwa jitihada zake na kuwahamasisha /kuwashirikisha wengine katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya mkoa wa Kagera.

 Naye mwakilishi wa waandishi wa habari waliohudhuria, aliahidi kwamba watatoa ushirikiano mkubwa wa kuihabarisha jamii kwa ufasaha juu ya jitihada zote za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo

DC MSAMBYA ATAKA WATAALAMU WA KODI MGODINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Manju Msambya, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya hiyo kupeleka wataalamu wa kodi na kuweka viwango vya ushuru katika mgodi wa machimbo ya dhahabu ya Muhintiri.
Akizungumza na viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo, Msambya, alisema ili kuiwezesha Halmashauri hiyo ni vema viongozi hao wakaweka wataalamu wa kodi watakaokusanya mapato ya ndani, ili waweze kukamilisha baadhi ya miradi badala ya kuendelea na utamaduni wa kutegemea fedha za Serikali kuu.
Aidha, alisema eneo la machimbo hayo lina mzunguko mkubwa wa fedha, hivyo kuhitaji kuangaliwa na kuhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao unakuwa wa uhakika na kuongeza kuwa, mgodi huo bado haujawa rasmi hivyo ni vema kufuatilia mapato.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Celestine Yunde, alimwagiza mkaguzi wa ndani kukagua miradi ya maendeleo iliyopo vijijini na kuwasilisha taarifa.
Chanzo:Tanzania Daima

UTUMISHI YAFANYA KIKAO KAZI KWA VIDEO CONFERENCE NA MIKOA YA SINGIDA,ARUSHA NA DODOMA


Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akifungua kikao kazi kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference)kilichojumuisha Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akifuatilia mada wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Sakina Mwinyimkuu akiwasilisha katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni viongozi wa Ofisi ya Ris Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Kielektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Afisa Utumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Magreth Ngondya (kushoto) akiwasilisha mada katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia Ki- elektroniki (video conference) katika kikao kazi kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni viongozi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WALIMU WAKOSA VYOO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Mandewa katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida hawana vyoo kwa miaka nane sasa, halia ainayowalazimu kutumia vyoo vya wanafunzi.
Kufuatia hali hiyo, Rais wa Shirikisho la Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina, ameingilia kati na kutoa sh. 500,000, lori 10 za mchanga na vifaa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo hivyo.
Akizungumza juzi kwenye mahafali ya nne wa kidato cha nne kwenye shule hiyo, Bina ambaye alikuwa mgeni rasmi alionekana kuguswa na hali hiyo na kuamua kuendesha harambee ya papo kwa hapo.
Mara baada ya Bina kuanzisha harambee hiyo, Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Tawi la Singida, Emmanuel Kingu alitoa mifuko 20 ya saruji, mwenyekiti wa kamati ya shule alitoa mifuko 10 ya saruji na Diwani wa viti maalum wa Kata hiyo, Sara Alute alitoa mifuko miwili.
Mapema katika taarifa ya shule, pamoja na mambo mengine mkuu wa shule hiyo, Magreth Misanga alisema shule hiyo inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa vyoo vya walimu.
Misanga alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2006 kwa michango ya nguvu za wananchi na hadi sasa ni miaka nane hawana vyoo vya walimu na hivyo kujikuta wakitumia vyoo vya kantini ya shule pamoja na watu wengine.
Shule hiyo ina wanafunzi 381, ambapo kati yao wavulani ni 204 na wasichana 177.
Chanzo:Tanznia Daima

MAAMBUKIZI YA VVU YAPUNGUA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

TANZANIA imefanikiwa kupunguza viwango vya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kutoka asilimia 26 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 15 mwaka 2012.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, wakati wa uzinduzi wa mpango wa ushirikiano ili kupunguza VVU na vifo vya wajawazito na watoto, iliyofanyika mjini Singida juzi.
Dk.Kone alifafanua kwamba pamoja na mafanikio hayo, serikali hivi sasa inalenga kutokomeza kabisa maambukizi hayo.
Mkuu wa Mkoa huyo pia alipokea msaada wa vifaa mbali mbali vilivyotolewa na Watu wa Marekani kupitia Shirika ka misaada la USAID kama sehemu ya Mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupambana na Ukimwi (PEFER).
“Ni katika utekelezaji wa mkakati huo wa kitaifa, leo nitazindua mkakati wa tokomeza maambukizi mapya ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa mkoa wa Singida,”alisema.
Kwa mujibu wa Dk.Kone, takwimu zinaonesha kwamba hapa nchini kati ya wajawazito 100,000 wanaojifungua, 454 hufariki kutokana na matatizo wakati wa mimba au uzazi na watoto 26 hufariki dunia kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa kila mwaka.
Awali, Mkurugenzi wa Tunawajali, Dk.Gottlieb Mpangile akitoa maelezo ya mradi huo, pamoja na kukabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 155, alivitaja vituo vitakavyonufaika na msaada huo kuwa ni hospitali za Mtakatifu Gasper, Caroluos, Misheni ya Kilimatinde na Kiomboi, Manyoni, Makiungu, Iambi, vitoa vya afya Ndago, Ikungi na Sokoine.
Alisema kuwa nia ya Tanzania ni kupunguza vifo vya akina mama wakati wa uzazi, jambo alilosema linawezekana.

Chanzo:Tanzania daima

FUNDI RADIO AFA BAADA YA KUZIDIWA GESTI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

FUNDI radio maarufu mjini hapa, Daniel Mosha (53), amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa baada ya kuugua ghafla akiwa anafanya mapenzi na mwalimu mmoja katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Cheyo.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11:00 alfajiri katika nyumba hiyo iitwayo Cheyo chumba namba nne, wakati fundi huyo akijivinjari na mpenzi wake huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Geofrey Kamwela, alisema fundi huyo alifariki Oktoba 14 mwaka huu saa 10.30 jioni katika hospitali ya Mkoa alikokimbizwa baada ya kuzidiwa akiwa gesti.
Aidha, Kamanda Kamwela alisema kuwa Oktoba 13 mwaka huu majira ya jioni, marehemu akiwa nampenzi wake wa muda mrefu, Serafine Lucian (56), mwalimu wa shule ya Msingi Manguanjuki manispaa ya Singida, walipanga chumba namba nne kwa ajili ya mapumziko ya usiku mzima.
"Ilipofika alfajiri saa saa 11 Oktoba 14 mwaka huu, mwanaume huyo alianza kuugua ghafla huku akikoroma na ndipo mwalimu Serafine, aliamka na kumwita meneja wa nyumba hiyo na kumweleza juu ya hali ya mpenzi wake," alisema.
Alisema meneja pamoja na mwalimu huyo, walifanya juhudi za kumkimbiza hospitali ya Mkoa ili kuokoa maisha yake lakini mambo yaliendelea kuwa magumu.
Hata hivyo, Kamanda Kamwela, alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa katika chumba walichopanga wapenzi hao, pamoja na vitu vingine zilikutwa paketi tupu za pombe kali aina ya viroba vilivyotumika.
"Tunaendelea na uchunguzi ili kujua kama kuna mtu au watu wanaohusika na kifo hicho cha fundi radio, lakini tunamshikilia mwalimu huyo kwa uchunguzi zaidi, ili pamoja na mambo mengine kuchunguza iwapo kuna mtu au watu waliohusika na kifo hicho,” alisema Kamwela.
Chanzo:Tanzania Daima

BAADA YA DIAMOND KUPANDA KWENYE STAGE NA NGUO ZA JESHI, JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) LATOA TAARIFA







JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E”            Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463       Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                        DAR ES SALAAM, 20 Octoba, 2014
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.
          Aidha,  kumeonekana matukio kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja kumiliki au kuvaa sare za JWTZ.  Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama kumiliki sare hizo sheria itachukua mkondo wake. 

  
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.


Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963


Chanzo: Pamoja Blog
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

TAARIFA FUPI YA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI MKOANI SINGIDA KIPINDI CHA 2005 - 2014‏

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.
Jengo la OPD katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Jengo la OPD katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Jengo la utambuzi wa Magonjwa katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Jengo la utambuzi wa Magonjwa katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Tamasha la Fiesta 2014 laiteka Singida, leo Jumapili kurindima mjini Dodoma


 Baadhi ya mwashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 wakishangilia kwa hisia,wakati shoo ikiendelea jukwaani ndani uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kampuni ya No Fake Zone,Linah Sanga ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Oletemba,akiimba jukwaani mbele ya umati wa watu wakati wa tamasha la Fiesta lililofanyika jana katika uwanja wa Namfua,kulia ni mmoja wa wacheza shoo wake akiwajibika jukwaani.
 Kundi mahiri la muziki wa kizazi kipya litambulikalo kwa jina la Makomando wakilishambulia jukwaa la Fiesta hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya Uwanja wa Namfua hapo jana mjini Singida.
 Mmoja wa mashabiki akishangilia huku akiwa amebebwa
 Msanii wa muziki wa bongofleva,Mr Blue a.k.a Kabyssal akiimba mbele ya umati wa wakazi wa mji wa singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua.
 Sehemu ya umati wa watu ndani ya tamasha la Fiesta mjini Singida hapo jana katika uwanja wa Namfua
10
 Ilikuwa ni shangwe tu ndani ya uwanja wa Namfua wakati tamasha la Fiesta likiendelea.
 Msaniii mwingine anaefanya vyema katika anga ya muziki wa bongofleva,kupitia kundi la WEUSI,Niki wa Pili akiwaimbisha mashabiki wake
 Shabiki kapagawa na yaliyokuwa yakijiri jukwaani.
 Badala ya kuwa watazamaji tu,nao pia walikuwa wakijimwaya mwaya taratiibu.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya vipaji ya THT,Rachael akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani),wakati wa tamasha la Fiesta likendelea ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
 Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes anaetamba na wimbo wake wa Togola akiwaimbisha mashabiki wake,kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
 Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kizazi kipya atambulikae kwa jina kisanii Mwana-FA akiimba mbele ya umati wa wakazi wa Singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2014,lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Namfua.
 Msanii Mwana-FA na Linah wakiimba kwa pamoja jukwaani,huku miluzi na makelele ya mashabiki yakiwa yametawala kila kona ya uwanja wakati wa tamasha la Fiesta likiendelea.
 Mashabiki wakishangilia
 
Wasanii mahiri wa muziki wa Bongofleva, Ney wa Mitego na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kupitia wimbo wao unajojulikana kwa jina la Huko kweni Vipi,ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Singida wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya tamasha la Fiesta.PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa