Baadhi
 ya mwashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 wakishangilia kwa hisia,wakati 
shoo ikiendelea jukwaani ndani uwanja wa Namfua mjini Singida.
 Msanii
 wa muziki wa kizazi kipya kutoka kampuni ya No Fake Zone,Linah Sanga 
ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Oletemba,akiimba jukwaani 
mbele ya umati wa watu wakati wa tamasha la Fiesta lililofanyika jana 
katika uwanja wa Namfua,kulia ni mmoja wa wacheza shoo wake akiwajibika 
jukwaani.
 Kundi
 mahiri la muziki wa kizazi kipya litambulikalo kwa jina la Makomando 
wakilishambulia jukwaa la Fiesta hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua 
mjini Singida.
 Sehemu
 ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la 
Fiesta ndani ya Uwanja wa Namfua hapo jana mjini Singida. 
 Mmoja wa mashabiki akishangilia huku akiwa amebebwa
 Msanii
 wa muziki wa bongofleva,Mr Blue a.k.a Kabyssal akiimba mbele ya umati 
wa wakazi wa mji wa singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 
lililofanyika hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua.
 Sehemu ya umati wa watu ndani ya tamasha la Fiesta mjini Singida hapo jana katika uwanja wa Namfua
 Ilikuwa ni shangwe tu ndani ya uwanja wa Namfua wakati tamasha la Fiesta likiendelea. 
 Msaniii
 mwingine anaefanya vyema katika anga ya muziki wa bongofleva,kupitia 
kundi la WEUSI,Niki wa Pili akiwaimbisha mashabiki wake
 Shabiki kapagawa na yaliyokuwa yakijiri jukwaani.
 Badala ya kuwa watazamaji tu,nao pia walikuwa wakijimwaya mwaya taratiibu.
 Msanii
 wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya vipaji ya THT,Rachael 
akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani),wakati wa tamasha la Fiesta
 likendelea ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana. 
 Msanii
 mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes anaetamba na wimbo wake 
wa Togola akiwaimbisha mashabiki wake,kwenye tamasha la Fiesta ndani ya 
uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana. 
 Mmoja
 wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kizazi kipya atambulikae kwa jina
 kisanii Mwana-FA akiimba mbele ya umati wa wakazi wa Singida 
waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2014,lililofanyika jana ndani ya 
uwanja wa Namfua.
 Msanii
 Mwana-FA na Linah wakiimba kwa pamoja jukwaani,huku miluzi na makelele 
ya mashabiki yakiwa yametawala kila kona ya uwanja wakati wa tamasha la 
Fiesta likiendelea.
 Mashabiki wakishangilia 
Wasanii
 mahiri wa muziki wa Bongofleva, Ney wa Mitego na Stamina 
wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kupitia wimbo wao unajojulikana kwa 
jina la Huko kweni Vipi,ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo 
ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Singida wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya tamasha la Fiesta.PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.




















0 comments:
Post a Comment