Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba (kushoto) na mbunge wa Viti
Maalumu Mkoa wa Singida, Martha Mlata wakikabidhi zawadi ya boga kubwa
lenye kilo zaidi ya 7 Balozi wa China nchini, Dk Lu Youqing. (Na
Mpigapicha Wetu).
DC MTATURU AKUTANA NA WAZEE WA WILAYA YA IKUNGI AWAAHIDI KUFANYA KAZI KWA BIDII
MKUU WA WILAYA YA IKUNGI ATANGAZA SIKU YA JUMATANO KUWA SIKU YA KAZI ZA PAMOJA
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwa ofisini mara baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye kwa sasa amestaafu Gishuli Charles.
NSSF yashauriwa kusaidia wasanii.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Meneja wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso.
Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii( NSSF) Mkoa wa Ruvuma limeshauriwa kuinua maisha ya wasanii kwa
kuwaunganisha na mfuko huo ili kuhakikisha maisha ya wasanii
yanaboreshwa.
Akizungumza katika kikao kati ya
wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara, Katibu
Mkuu wa Wizara Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel amesema kuwa
mfuko huo uangalie namna ya kukusanya wasanii na kuwaweka pamoja ili
waweze kujiunga.
“kwa upande wa wasanii wao ni
jeshi kubwa tutafute namana ya kuwasajili kama wanachama rasmi wa NSSF
ili waweza kutambulika katika ajira rasmi” alisema Prof Gabriel.
Prof Gabriel alisema kuwa
wasanii wanachangamoto nyingi zinazo wakabili ambazo zinarudisha nyuma
kada yao moja wapo ikiwa ni hiyo ya kutokuwa wanachama wa mifuko ya
Jamii.
Kwa upande wake Meneja wa NSSF
Mkoa wa Ruvuma Bw. Felix Wisso amesema lengo la mfuko huo ni kudumisha
maisha ya watanzania walio katika sekta zote hivyo basi kwa kushirikiana
na Ofisi ya Mkoa wanaangalia namna ya kuwainua wasanii hao kupitia
mikopo itolewayo na mfuko huo.
Ameongeza kuwa shirika lake
limejipanga kikamilifu kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu
ya tano hivyo basi elimu ya kujiunga na mfuko huo itaendelea kutolewa
kwa wananchi .
“Wasanii wanaweza kuitangaza nchi
yetu vizuri sana kama tu jamii itaamua kuwatambua na sanaa ikawa ni
ajira kamili kama ajira nyingine.”Alisema Bw. Wisso
Aidha aliwasisitiza viongozi wa
wasanii pamoja na Maafisa Utamaduni kuwahamasisha wadau wao kuingia
katika mfuko huo wa jamii kwani ni dhamana ya maisha yao.
WAZIRI NCHEMBA AAGIZA MAOFISA USHIRIKI SINGIDA KUCHUKULIWA HATUA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
| mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu (kulia) akimpokea waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba alipofanya ziara ya kikazi wilaya ya Manyoni jana |
| Waziri Nchemba akisalimiana na mbunge Nyalandu (kulia) |
| Waziri wa kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali kuingia ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima wa Tumbaku Manyoni |
| Mbunge Lazaro Nyalandu kulia akiwa na waziri wa Kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba wakati akisaini kitabu cha wageni ofisi ya mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida |
| Waziri Nchemba akiingia ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima wa Tumbaku manyoni |
| Wakulima wa Tumbaku wakisalimiana na waziri Nchemba |
| Baadhi ya madiwani wakulima wa Tumbaku manyoni wakimpokea waziri Mwigulu Nchemba |
| Baadhi ya wakulima wa Tumbaku wakiwa ukumbi wa mkutano kati yao na waziri Nchemba |
| Mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu akitambulisha viongozi mbali mbali kabla ya mkutano wa wakulima wa Tumbaku kuanza |
| Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akizungumza na wakulima wa Tumbaku wilaya ya manyoni mkoa wa Singida jana |
| Wakulima wa Tumbaku wakitoa kero zao kwa waziri Nchemba (hayupo pichani) |
| Wabunge wakisikiliza kero za wakulima wa Tumbaku |
waziri wa Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu wakati akieleza kilio cha wakulima wa Tumbaku wilaya ya Manyoni wakati wa mkutano wa waziri Nchemba na wakulima wa Tumbaku uliofanyika ukumbi wa CCM Manyoni jana
WAZIRI wa kilimo
,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu
Nchemba amefuta michango hewa
iliyokuwa ikichangiwa na wakulima wa Tumbaku kwa
UNION kwa kupitia kitengo
cha AMIS huku akiagiza serikali
ya wilaya ya Manyoni kuwachukulia hatua kali aofisa
ushirika mkoa Andru Msafiri na
afisa ushirika Wilaya hiyo Bw Alfred Sekiete iwapo
watabainika kuhusika deni la bilioni 7
ambalo wanadaiwa benki wakulima wa
tumbaku.
Waziri Nchemba
alilazimika kutoa maagizo
hayo baada ya
wakulima wa zao hilo la
Tumbaku kulalamikia utaratibu mbaya wa
baadhi ya viongozi wa UNION na APEX
pamoja na baadhi ya maofisa
ushirika kujinufaisha kupitia mgongo wa
wakulima hao.
Akitoa agizo
hilo jana mjini Manyoni wakati wa
mkutano wa pamoja kati yake na wakulima wa
Tumbaku na viongozi mbali
mbali wa Serikali ya
wilaya ya Manyoni na wabunge
wanaotoka wilaya ya Maeneo yanayolimwa Tumbaku mkoani
Singida.
Waziri Nchemba
alisema kuwa baadhi
ya mambo ambayo serikali ya Rais Dr John Magufuli haipendi
kuona ni pamoja na wakulima kubebeshwa mizigo mikubwa ambayo
kimsingi haiwasaidii kupiga hatua kimaendeleo
zaidi ya kuwatesa .
Alisema
inashangaza kuona wakulima
hao kuendelea kuumizwa na
viongozi wachache ambao wamegeuza
wakulima ni kichaka cha wao
kujificha kujinufaisha kupitia wakulima.
“ Mambo ya ajabu sana
hiki kitu kinaitwa AMIS ni
kuwatoza wakulima michango ya ajabu
ajabu eti wakulima
kutozwa dola 1200 kwa ajili
ya kusafirisha Tumbaku toka Dar
es Salaam kwenda UNION pia wanachangia dola 10 kwa kutunza
kumbukumbu zao ,dola 3 kupakia na kushusha mara mchango kwa ajili ya ADMIN mambo ya ajabu kabisa wakulima
wanahusika vipi na malipo maadmin yani
wanatumia lugha za kijanja kijanja kuwaibia
wakulima ADMIN wa makundi kama yale ya Whatsap kwa wakulima tena…sasa kuanzia leo natangaza kufuta michango hii isiyo na maelezo ya kutosha na
kuagiza kujipanga upya kwa kuwashirikisha wakulima na taarifa hiyo ndani ya siku 7 niipate “
Waziri chemba
alisema kuwa kabla ya kuanza
kuwatoza wakulima hao michango
ni vizuri makubaliano ya michango
hiyo yafanyike upya kwa
kuwashirikisha wakulima na sio
kuendelea kutumia taratibu za
zamani ambazo ni mzigo kwa
mkulima.
Kuhusu maafisa
ushiriki kudaiwa kukopa
benki kupitia mgongo wa wakulima
wa tumbaku na kupelekea
wakulima hao kudaiwa deni benki
la Tsh bilioni 7 aliagiza mkuu wa wilaya ya Manyoni kuagiza wakaguzi na wataalam wake kufanya
uchunguzi na iwapo itabainika kuwa maofisa
hao walihusika na deni hilo
hatua stahiki kuchukuliwa dhidi
Alisema ni kosa
kwa maofisa ushirika kukopa
kwa udhamini wa
wakulima wakati wao si
wazalishaji wa mazao hayo ya
kilimo na kuwa maeneo mengi
wakulima walikuwa wakiwalipia madeni
benki maofisa hao ambao huomba mikopo kupitia vyama vya msingi vya wakulima na wakati mwingine hushirikiana na
benki kutoa mkopo mkubwa ili nao waweze
kugawana .
Pia aliagiza
UNION kufanya kazi ya kuwasaidia
wakulima na sio
kuwakandamiza wakulima na kuwa maeneo
mengi nchini ambayo UNION wapo
kumekuwa na migogoro na kero nyingi kwa
wakulima na kuwa mazao ambayo wakulima hawana UNION kama Mahindi ,
mpunga na alizeti wakulima wanafanya
shughuli zao pasipo migogoro hivyo kuzitaka UNION zinazojihusisha na wakulima wa Tumbaku , Korosho ,pamba na mazao
mengine kujitathimini vinginevyo hazina maana kuwepo.
Aidha waziri Nchemba aliagiza benki ya CRDB kuwalipa pesa zao
zote wakulima wa Tumbaku ambao
wamemaliza madeni yao ya pembejeo na kuendelea
kuwadai wanaodaiwa na si vinginevyo .
Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro
Nyalandu alisema kuwa
kilio kikubwa cha
wakulima wa Tumbaku Manyoni ni uwepo
wa mtu kati katika kilimo hicho
hivyo kuwatesa wakulima hao na kuwa
UNION na APEX bado si ukombozi kwa wakulima wa
zao la Tumbaku kwani alisema wakulima wamekuwa wakilipwa asilimia 50 ya
mauzo ya mazao yao na benki ya CRDB na
asilimia 50 nyingine kushikiliwa na
benki kwa mkopo wa vyama vyao vya msingi hata kama mkulima husika hadaiwi.
Balozi asema Rais Magufuli ameipaisha Tanzania kimataifa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI ya China imeiunga mkono serikali katika mkakati wake wa
kutoa elimu bure, ikisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais John
Magufuli, Tanzania inasifika duniani.
Katika kuunga mkono elimu bure, ubalozi wa nchi hiyo nchini umetoa
msaada wa madawati 400 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 28 kwa shule
mbalimbali za msingi katika wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Balozi wa China hapa nchini, Dk Lu Youq’ng alisema msaada huo ni moja
ya juhudi za nchi yake kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kutoa
elimu bure. “Wakati mimi nimechangia madawati 300, Kampuni inayochimba
madini hapa ya Sun Shine Group imechangia madawati 100 ili kuniunga
mkono,” alifafanua.
Akikabidhi madawati hayo katika mikutano mitatu tofauti kwenye mji wa
Kiomboi, Shelui na Misigiri, Balozi Youq’ng alisisitiza umuhimu wa
Tanzania kuwekeza kwenye elimu kuwaletea wananchi wake maendeleo ya
kweli.
“Hata kama nchi ni maskini kiasi gani, lazima elimu itiliwe mkazo;
tena iwe ni elimu bora na elimu bora haiwezi kuja kwa wanafunzi kukaa
chini. “Madawati ni moja ya mambo ambayo yanamjengea mwanafunzi
mazingira mazuri ya kujifunzia,” alisema.
Aliongeza, “kutokana na umuhimu huo, ndio maana mbunge wenu
aliponijia na kuniomba msaada wa madawati, sikusita hata kidogo. Nilijua
anafanya hivyo ili kuisaidia jamii yake kuboresha elimu”. Aliyeomba
msaada huo ni Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Aidha, balozi huyo amewapongeza wakazi wa mkoa wa Singida kwa
kumchagua Dk Magufuli kuwa Rais na kuongeza kusema kuwa chini ya uongozi
wake sasa Tanzania inasifika duniani kote. “Nitahakikisha nchi yangu
inaendelea kusaidia maendeleo ya nchi hii kwa kuwa urafiki wetu ni wa
enzi na enzi,” alisema.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe alisema kuwa mkoa
unathamini msaada huo kwa kuwa umepunguza kwa kiasi kikubwa upungufu wa
madawati 4,016 ambayo wilaya hiyo ilikuwa nao.
Chanzo Gazeti La Habari Leo
UWANJA WA NDEGE SINGIDA NI 'JIPU' NANI WA KULITUMBUA?
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
| Hapa akielekea kuelekeza eneo la kutua |
| Hapa akimwelekeza rubani wa ndege hiyo huku kulia kifaa kinachotumika kama gari la zimamoto na uokozi likiwa limeegeshwa kulia |
| Ndege ikiwa imetua huku kifaa kinachotumika kama gari la zimamoto na uokozi kikiwa pembeni na mhudumu wa kifaa hicho kushoto |
| Rubani akimtazama mfanyakazi huyo mmoja anayefanya kazi tatu kwa wakati mmoja katika uwanja wa ndege Singida |
TAASISI ZA SERIKALI ZILIZOUNGANISHWA NA MFUMO WA SIMU ZENYE ITIFAKI YA INTANETI ZATAKIWA KUTUMIA HUDUMA HIYO KUPUNGUZA GHARAMA YA MAWASILIANO.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Serikali kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) imezitaka taasisi zote zilizounganishwa kwenye mfumo wa simu zenye itifaki ya intaneti (Internet Protocol (IP) ambazo zinatumia intaneti kuzitumia simu hizo katika mawasiliano yao kila siku ili kuboresha utendaji kazi na kupunguza gharama za mawasiliano Serikalini.
Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan Mshakangoto amesema kuwa Serikali imeamua kusisitiza matumizi ya simu hizo ili kuziwezesha taasisi za Serikali kuwa na mawasiliano yaliyo bora, salama na kupunguza gharama za mawasiliano.
Amesema kuwa Serikali kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) imeunganisha taasisi za Serikali 72 ambazo zinajumuisha Wizara, Idara zina zojitegemeana na Wakala za Serikali na kuongeza kuwa taasisi hizo zimeunganishwa na Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali yaani ‘Government Communication Network (Govnet)’ unaowezesha mfumo wasimu hizo kufanya kazi kwa ufanisi.
“ Kupitia mfumo wa simu hizi zenye itifaki ya intaneti mtumishi wa taasisi iliyounganishwa anaweza kupiga simu kwenda taasisi nyingine ya nje ikawa kama amepiga simu ya ‘extension’ ndani ya ofisi moja” Amesema Bi. Suzan.
Aidha,
amesema Taasisi za umma zitanufaika moja kwa moja na simu hizo kwa
kuwa, taasisi hizo zitaweza kubadilisha na taarifa kupitia mtandao mmoja
tuwa Mawasiliano wa Serikali kwa usalama na uhakika. Pia simu hizo
zitawawezesha watumishi wa taasisi mbalimbali kufanya mkutano kwa njia
ya simu wakiwa kwenye ofisi zao na hivyo kuokoa muda na gharama za
usafiri.
Hata
hivyo amesema taasisi za umma zilizopo katika mtandao wamawasiliano wa
Seikali zitaendelea kuwasilia na na taasisi zilizo nje ya mtandao huo
kwa kupitia mtoa huduma wa simu za mezani (PSTN Provider) kama vile
TTCL.
Tigo yatoa visima 12 vya maji kwa vijiji 12 Singida
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akikata utepe katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akifungua moja ya bomba katika kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia) akifungua bomba katika moja ya kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo pembeni yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
Singida, Aprili 27th 2016: Kampuni ya simu ya Tigo leo imekabidhi visima 12 vya maji vyenye thamani ya 174m/- kwa vijiji 12 mkoani Singida ikiwa ni kuchangia juhudi za serikali za kupunguza uhaba wa maji safi na salama uliopo nchini.Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye kijiji cha Mtinko wilayani Singida mkoani Singida, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata alisema ufadhili huo umo kwenye mikakati ya kampuni ya kusaidia jamii katika kunyanyua hali zao za maisha.Vijiji vitakavyonufaika kutokana na ufadhili huo pamoja na wilaya zake kwenye mabano ni Lulumba (Iramba), Kisana (Iramba), Kisonzo (Iramba), Songambele (Iramba), Kinyeto (Singida Vijijini) na Damankia (Ikungi). Vingine ni Muungano (Ikungi), Ighuka (Ikungi), Kamenyanga (Manyoni), Sasajila (Manyoni), Mtinko (Singida Vijijini) and Kinampanda (Kinampanda).“Msaada huu ni sehemu ya uwekezaji wa Tigo kwenye miradi ya kijamii ambayo inaleta tija kubwa kwa jamii. Tuna imani kwamba kupitia visima hivi, Tigo inasaidia kutatua uhaba mkubwa wa maji katika eneo hili la mkoa wa Singida ambalo kwa kiwango kikubwa limekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua katika kipindi cha miaka mine iliyopita,” alisema Lugata.Aidha aliongeza kuwa uhaba wa maji miongoni mwa wilaya nyingi za Singida umesababisha wakiazi wake kupoteza muda mwinmgi kutafuta bidhaa hiyo muhimu, jambo ambalo Tigo inaamini kuwa hivi sasa litafikia ukomo kutokana na upatikanaji wa visima hivyo.Makabidhiano ya visima hivyo yalihudhuriwa na kushuhudiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ambaye aliishukuru Tigo kwa ufadhili huo uliopatikana kwa wakati mwafaka akisema kwamba visima hivyo vitapunguza kwa kiwango kikubwa uhaba sugu wa maji uliolikumba eneo hilo na kuchangia kukua ustawi wa jamii kijamii na kiuchumi.Hata hivyo, alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuchangia kwenye juhudi kama hizo. Waziri Lwenge alisema, “Tunatoa shukrani za dhati kwa Tigo kwa kutuunga mkono kwenye juhudi zetu za kutatua uhaba wa maji uliopo Singida na hata kwenye mikoa mingine nchini. Tuna imani visima hivi 12 vitasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hili linaloikabili jamii kwa sasa”.
MWIGULU,SENDEKA WASHIRIKI MAZISHI YA CHRISTINA LISSU MKOANI SINGIDA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akitoa heshima zake za mwisho mapema leo kabla ya mazishi, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lisu,Wilayani Ikungi mkoani Singida.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida,Bi Martha Mlata akitoaa heshima zake za mwisho mapema leo kabla ya mazishi, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lissu,Wilayani Ikungi mkoani Singida.
Msemaji wa chama cha CCM,Ole Sendeka, Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba wakimpa pole Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA),Mh Tundu Lissu,ambao waliwasili wilayani Ikungi mkoani Singida kushiriki Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lissu.
Msemaji wa chama cha CCM,Ole Sendeka akimpa pole Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA),Mh Tundu Lissu kwa kufiwa na dada yake
Msemaji
wa chama cha CCM,Ole Sendeka akitoa neno la pole kwa Wafiwa,ndugu,jamaa
na marafiki kabla ya kufanya maziko, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA
(Viti maalum),Marehemu Christina Lissu,Wilayani Ikungi mkoani Singida.
Michuzi Media
Michuzi Media








