Home » » Club Ya Waandishi Singida Kukumbwa Na Mgogoro

Club Ya Waandishi Singida Kukumbwa Na Mgogoro


 Baadhi ya wanachama wa Singpress wakiwa mkutano mkuu na kufikia uamuzi wa kusamehe madeni kwa wenzao walioazima vifaa vya klabu
 Katibu mtendaji wa Singpress, Bw. Abby Nkungu akieleza kwa wadau wa habari safari ndefu ya kalbu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002
Singida
Desemba 12,2012.
MGOGORO mkubwa unaiandama Klabu ya wanahabari mkoa Singida (Singpress), kufuatia mwenyekiti wake Seif Takaza kuruhusu baadhi ya wanachama kufutiwa madeni yenye thamani ya Sh. 1,961,600.
Madeni dhidi ya wanachama hao ambao huko nyuma pia waliwahi kula fedha za waandishi, yametokana na kuazima vitendea kazi, vilivyotolewa masaada na baraza la habari nchini (MCT).
Vifaa hivyo vilivyotolewa kwa klabu zote nchini miaka minne iliyopita ni kamera aina ya sonny kwa ajili ya video na picha mnato (zote digitali), kompyuta za mezani na kinasa sauti kimoja.
Bei ya kukodi kwa siku ilikuwa Sh. 2,500 (kinasa sauti) Sh. 3,000 (picha mnato) na Sh.5,000 (video), wakati kompyuta haikuwa kwenye mpango wa kuazimishwa, lakini ilikuwa kwa mmoja wa viongozi, zaidi ya miaka miwili.
Kamera mbili ikiwemo ya video na picha mnato pia kompyuta, vilikuwa vipya wakati vinaazimwa, lakini viliporejeshwa vilikuwa havifai, wakati kinasa sauti mpaka sasa hakijulikani kilipo.
Katika mkutano huo, mwandishi wa jeshi la polisi mkoa Singida, Shabani Msangi, Paschal Tantau na wadaiwa sugu, walijipanga vema kudhoofisha jitihada ya uongozi uliotaka madeni hayo yalipwe.
Kufuatia mvutano mkali uliosababisha wajumbe wengi kutoka nje kwa hasira, mwenyekiti Takaza alivuruga zaidi alipoamuru upigaji kura na wajumbe wachache waliokuwa ndani, wakashinda.
Mkutano huo pia ulipitisha deni la Sh. 200,000 za pango alizokuwa anazodaiwa mwanachama Jumbe Ismaelly na Sh. 56,000 dhidi ya fundi mlango wa chuma Evarest Thomas, wazirejeshe mara moja.
Wanachama waliofutiwa madeni hayo na kiasi chao ni Doris Meghji (Sh. 90,000), Elisante Mkumbo (Sh. 25,000), Jumbe Ismaelly (Sh.1,231,600), Hillary Shoo (Sh. 615,000) na fundi mlango Evarist Thomas (56,000).
Waliofutiwa madeni hayo baadhi ni wadaiwa sugu, baada ya miaka ya nyuma kula fedha za rambirambi na mwingine kula fedha za umoja wa waandishi na wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini (AJM).
Aidha tabia ya wanachama wakorofi kupenda vurugu hadi kuchangia madeni hayo kufutwa, inaweza kuiingiza klabu kwenye mgogoro mkubwa, baada ya kutulia tangu uongozi mpya uingie madarakani 2011.



"Unaona sasa tabia ya kuingiza wanachama bila kufuatiliwa wasifu wao huko walikotokea imeanza kutugharimu...klabu ilishatulia, ona vurugu hizi, mtu anasema hadi anagonga meza utadhani amegombana, mimi najiuzulu ,"alisema mmoja wa viongozi wanaounda kamati ya utendaji.

1 comments:

Unknown said...

Andikeni ukweli kwa manufaa ya umma, sio kusema uongo katika mitandao Aibu sana kwa chombo hiki na mnauhakika kiasi gani na hayo mlioyaweka hapo.

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa