Home » » WALIMU 447 WILAYANI MANYONI YADAIWA HAWAJAPANDISHWA MADARAJA KWA MUDA MREFU

WALIMU 447 WILAYANI MANYONI YADAIWA HAWAJAPANDISHWA MADARAJA KWA MUDA MREFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Ni Katibu wa TSD Mkoa wa Singida,Bwana Samweli Ole Saitabau(aliyesimama) akitoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa haki za walimu wa wilaya ya Manyoni ambao bado haapandishwa madaraja yao.

Ni Baadhi ya wanachama wa CWT Wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Katibu Muu wa CWT,Bwana Ezekiah Oluoch  .
WALIMU 447 wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida hawajapandishwa madaraja yao mbalimbali kutoka mwaka 2014/2015 mpaka sasa hali ambayo imepunguza ari ya utendaji wao wa kazi za kila siku.
Katibu wa Chama Cha Walimu (CWT) Wilaya ya Manyoni, Nelea Nyang’uye aliyasema hayo kwenye taarifa ya kamati ya utendaji ya chama hicho aliyotoa kwa Naibu katibu mkuu CWT,Ezekiah Oluoch aliyekuwa na ziara ya siku moja wilayani Manyoni iliyolenga kusikiliza kero pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Aidha Nelea alifafanua kwamba kati ya walimu hao,walimu 390 ni walimu wa shule za msingi na kwamba walimu 276 licha ya kuwa na sifa za kupandishwa madaraja lakini mpaka wamefikia hatua ya kugota na bila kupandishwa na walimu 114 wanastahili kupandishwa kwa utaratibu wa kawaida.
Kwa mujibu wa katibu huyo wa CWT,kwa upande wa idara ya elimu sekondari kuna walimu 9 waliogota na walimu 50 wanastahili kupandishwa kwa utaratibu wa kawaida lakini mamlaka zinazohusika zimeshindwa kushughulikia wilayani hapa.
Kuhusu malipo ya fedha za likizo,Nyang’uye aliweka bayana kuwa kwa kipindi cha mwezi disemba,mwaka jana Halmashauri ya wilaya ya Manyoni ilitarajia kupokea shilingi milioni 30 lakini fedha walizopokea ni shilingi milioni 21 na hivyo kuwa na upungufu wa shilingi milioni saba.
Hata hivyo msemaji huyo wa chama alisisitiza kwamba fedha hizo za nauli ya likizo hupelekwa kidogo sana na kibaya zaidi fedha hizo hupelekwa wakati likizo ikiwa imeshaanza au inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea walimu wwenye haki ya kulipwa kuanza kukopa.
“Nauli za likizo kuletwa kidogo mno na zinaletwa wakati likizo ikiwa imeanza au inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea walimu wenye haki ya kulipwa kuanza kukopa,kwa mfano nauli ya mwezi disemba,mwaka jana iliyoletwa kwa idara ya elimu ya msingi ni shilingi 23,000,000/= na idara ya elimu sekondari ni shilingi milioni saba”alisisitiza katibu huyo wa CWT.
Nyang’uye hata hivyo alionyesha masikitiko yake kutokana na Tume ya Utumishi wa Walimu(TSD) wilaya ya Manyoni kushindwa kushughulikia mashauri ya kinidhamu kwa wakati na hivyo kuchukua muda mrefu sana na kutoa mfano wa shauri moja la walimu wawili waliosimamishwa kazi tangu mwaka 2013 mpaka sasa hawajuia hatma yao.
Picha na Michuzi Media

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa