Gasper Andrew,
Singida
KAMATI ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, imewataka wachimbaji wadogo wa dhahabu katika eneo la Sekenke wilaya humo, kufikia mwafaka baina yao na mwekezaji mwenye leseni, vinginevyo sheria ichukue mkondo wake.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Edward Ole Lenga, alisema agizo hilo linafuatia kushindikana kwa jitihada za kuzisuluhisisha pande hizo kwa njia ya mazungumzo.
Ole Lenga alisema kushindikana kwa jitihada hizo kumetokana na kitendo cha wachimbaji wadogo, kugoma kusaini makubaliano kati yao na mwekezaji John Bina, ambaye amekubali kuingia ubia na wachimbaji hao katika eneo la leseni yake.
Ole Lenga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Singida alisema hatua hiyo imeilazimisha kamati hiyo kuwataka wachimbaji hao, kufikia makubaliano nje ya mazungumzo rasmi.
Alisema vingine, Serikali itachukua hatua za kisheria kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria za madini nchini.
Kauli hiyo inakuja wakati Kamishina Msaidizi wa Madini katika Kanda ya Kati, Manase Mbasha, akiwa amesema wachimbaji hao wakiendesha shughuli zao kinyume cha sheria na kwamba wanapaswa kushtakiwa.
Wachimbaji wadogo katika eneo la Sekenke, amegoma kuondoka katika eneo hilo wala kuingia ubia na mwenye leseni,kwa madai kuwa leseni yake inataja eneo la Mgongo na si Sekenke.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment